alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu ili kila amwaminiye asipotee, haimaanishi kwamba yeye alishakufa kwahiyo hata ukitenda dhambi leo au kesho hautahukumiwa adhabu inaenda kwa Yesu. mnajidanganya, na hii ndiyo injili anayohubiri mzee wa neema wale wanaosapoti ushoga na wamefungiwa kanisa.ndio ilikuwa theme yao kwamba kwasababu Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi basi hata ushoga fanya tu.
ishi ukijua una wajibu wa kutenda mema ama la utaenda motoni.
WAGALATIA 6:7 INASEMA: 7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
jua leo wewe na mzee wa neema na mkewe grace vipodozi kwamba, sio kwamba neema ipo hivyo tutende tu dhambi kwasababu adhabu ni ya Yesu, NO, utaondolewa dhambi kwa kuzitubia kwake na kuziacha. pia Mungu hadhihakiwi. pia, neema ya Mungu inatutaka tuache chambi.
TITO 2:11 INASEMA: Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Moyo wangu umepokea sana huu mstari, Mungu anataka tukaishi kwa kiasi, haki, na tuishi kwa utauwa yaani ucha Mungu, huku tukilitazamia/tukilisubiria tumaini lenye baraka ambalo ni la ujio wa Yesu Kristo au thawabu ile tuliyowekewa kwa kutenda mema. tukihubiri hivi mnatutukana kwamba walokole hua tunajiona wasafi na hampendi kurekebishwa ati tunawaona ninyi wachafu, basi acheni kubishana na sisi, bishaneni na vifungu hivyo, laumuni vifungu hivyo vya Biblia, mwulizeni Mungu kwanini vipo.
NB: hayo mafundisho yenu ya mashetani mnapotosha watu, adhabu yenu itakuwepo siku ya mwisho.