Gardner G. Habash: Sina ugomvi na Jaydee, nimemkojoza miaka 15, Naibu Waziri aingilia kati

Gardner G. Habash: Sina ugomvi na Jaydee, nimemkojoza miaka 15, Naibu Waziri aingilia kati

Mkuu kama umegoma kuelewa hata kwa mfano niliokupa wacha tuufunge mjadala. Mwenye macho haambiwi tazama....

Bado sijaona wala kusikia alipotajwa mtu jina.

Kilichopo ni speculation tu.

Ni kama vile watu wanavyodhani ule wimbo wa ndi ndi ndi katungiwa Gardner ilhali mtu hata hajatajwa. Na vivyo hivyo kwenye wimbo wa Yahaya ambao kuna watu walidhani Gardner ndo alikuwa akizungumziwa.
 
kuna wanawake wa kuwastahi.
. not that evil .
Mwanaume kushindana na mwanamke ulieachana nae hasa kwa maneno ( mipasho ) ni kujidhalilisha mwenyewe. Mwanamke akiongea mwanaume fanya kwa vitendo maana wanawake wameumbiwa kuongea na ni wepesi kutoa ya moyoni. Lakini mwanaume mtimilifu tumeumbiwa kifua na uwezo wa kuchuja tunachotaka kusema.

Kama alikuwa na akili zake timamu na alidhamiria kusema hayo AMEKOSEA. Kuna kila dalili za mhusika kutoa kauli hiyo akiwa amelewa.

Kauli za KIUME za kuonyesha huna bifu na X wako:-
1. Sina tatizo naye ndio maana nyumba niliyomjengea nimemuachia abaki nayo.
2. Na muheshimu kwa 1,2,3, aliyonifanyia japo tumegombana
3. Naendaga kusalimia na kuwa hudumia watoto kwake kama mmejaliwa kupata watoto enzi zenu.

Na mambo mengi ambayo hata mimi kijana nikisikiliza naona kweli jamaa KIDUME hana tatizo na X wake.

mimi naona kwa kauli kama hii, ni dalili kuwa mwanaume hakuna na jambo lolote la msingi analoweza kujivunia amelifanya kwa X wake zaidi ya kilichosemwa.

"ooohhh nimem............",
sasa unatafutiwa, unapikiwa, unatengewa, unanawishwa mikono na mara nyingine kulishwa ili iweje????? au alafu huduma ikushinde?

yaani Ng'ombe uilishe alafu isitoe maziwa .............. tupa kule

Hata hivyo shukuru Mungu kwa huo uwezo maana hiyo huduma ingeshindikana hata miezi sita isingefika....
 
Kitendo cha Jide alichomfanyia gadner kama gardiner angemfanyia Jide hapa ungesikia tasisis zote za kutetea wanawake zingepiga kelele na vipindi maalum kwenye TV vingeandaliwa.
 
Jukwaa la nini na wandaaji walikuwa kina nani?

Make najua Gadna anafanya kazi clouds, jukwaa lolote la clouds halipigi nyimbo ya Jide
Hiyo ni juzi tu mkuu, ilikuwa kwenye miss TIA pale Bills.
So Gadna alikuwa ndo mc...hilo jukwaa halikuandaliwa na clouds.
 
Wale kina mama waliozalilishwa pale bungeni Dr.Kigwangala alifanya jitihada zozote kuwasitiri?
 
Kumbe Gadner anajua kumkojoza mwanamke? Hongera zake maana wanaume wengi wa Dar hawawezi kumkojoza mwanamke sababu yakula chips mayai na kuku wa kizungu, shame on you wanaume wa Dar

Usipeniki!
Huu mchezo hauhitaji hasira!
 
Gadner G Habash ni miongoni mwa watangazaji wa redio ninaowaheshimu katika muda wote. Si tu kwasababu ni mtangazaji mkongwe, bali pia ni mtangazaji mwenye sauti ya pekee hewani na mwenye busara inayoweza kuhamisha milima. Anapokuwa anaongea jambo, mamlaka anayoyaweka kwenye sauti, hukufanya kila neno limtokalo mdomoni likuingie vyema masikioni.

Na kwa hakika tangu aachane na mke wake, Lady Jaydee, amekuwa akijibu maswali yanayowahusu kwa werevu mkubwa. Miongoni mwa interview yake iliyonivutia sana ni ile aliyofanya na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV.

“Siwezi kusema najuta kwamba [Jaydee] alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia,” alisema Gardiner.

“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.

Pia nilipenda majibu yake ya maswali kuwa Ndindindi ni wimbo alioandikiwa na ex wake huyo.

Hadi hapo niliendelea kuamini kuwa mtangazaji huyo ameufunga ukurasa wake na Lady Jaydee kwa amani na kila mmoja ameangalia hamsini zake, maisha yanaendelea. Sishangai kabisa kama ukweli halisi ni kwamba wawili hao wanachukiana baada ya kuachana kwasababu ni kitu cha kawaida. Na mara nyingi chuki huwa kubwa pale pendo linapochanganyikana na chuki na hasira ya kutendwa au kwasababu yoyote ile inayomfanya mmoja wapo kukatisha uhusiano kwa kosa la mwingine.

Lakini nashangaa sana kwa mtu smart kama Gardiner kutamka maneno ya kumdhalilisha ex wake mbele ya kadamnasi. Kuna video imesambaa na naamini itakuwa viral sana wiki hii inayomuonesha mtangazaji huyo akiwa jukwaani kama mshereheshaji wa tukio moja jijini Dar es Salaam akiongea maneno makali kumhusu ex wake ambaye licha ya kutomtaja inajulikana wazi alikuwa anamuongelea nani.

“My name is Captain Gardiner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana,” anasikika akisema kwenye kipande hicho cha video. “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi,” anasema Gardiner na kisha Dj anaucheza wimbo wa Lady Jaydee, Ndindindi. Mtangazaji huyo anaonekana kuucheza pia wimbo huo jukwaani huku watu wakimshangilia.

Nimependa ujasiri wa Gardiner katika kulisema jambo hilo na kudhihirisha kwa mara nyingine tena kuwa hana tatizo na ex wake lakini sijapendezwa na uchaguzi wake wa maneno. Kimsingi ni clip ambayo kwa namna nyingi inamdhalilisha ex wake lakini pia inamuondolea Captain ile busara ambayo najua anayo.

Sijachachagua kuiweka clip hiyo hapa kutokana na kilichosemwa lakini ningemshauri kaka yangu Gardiner kuendelea kusimamia busara yake aliyonayo siku zote na kujiepusha na kauli tata kama hizi ambazo mara nyingi huwa zina madhara kwenye brand. Video hiyo haijamdhilisha Jide tu bali wanawake wote ambao kwa hakika kwa kauli yake inawaelezea kama ni vyombo vya starehe tu.

Na utashangaa jinsi ambavyo video fupi kama ile ikaondoa heshima ya Gardiner aliyoitengeneza kwa muda mfupi. Matusi anayotukanwa sasa kwenye ukurasa wake wa Instaram yanatoa jibu la ni kwa kiasi gani watu hawajapendezwa na kauli zake. Pia ni kauli mbaya katika kipindi hiki ambacho amerejea kwa kasi Clouds FM kukalia kiti chake kilichoshindikana kukaliwa na watangazaji wengi.

Bahati nzuri binadamu husahau mapema, yataisha tu lakini ni vyema Captain akawa mwangalifu na kauli zake katika siku za usoni sababu ‘kile kinachotokea au kusemwa kwenye starehe hakibaki hapo tu.’
 
Kumbe Gadner anajua kumkojoza mwanamke? Hongera zake maana wanaume wengi wa Dar hawawezi kumkojoza mwanamke sababu yakula chips mayai na kuku wa kizungu, shame on you wanaume wa Dar
Na yeye ni hao hao, jinga sana huyu jamaa ati naye anasimama kujisifia miaka kumi na tano halafu anaondoka na nguo zake kwenye rambo, wenzake madakika tu binti anatemea mate begani baada ya miezi tisa mzigo unashushwa,
 
Nimeitazama hiyo clip nikahisi kama hayo maneno katamkiwa dada yangu wa tumbo moja, sio ww tu mkuu uliyekuwa na heshima kwa Gadner, mimi mmojawapo na ninaamini jamii nzima kwa ujumla, ila kwa kitendo hicho wallah sitakaa nisikilize huyu jamaa akiwa radioni.
Ila kwa tafsri yangu ya haraka inaonyesha Gadner anaumwa sana na roho kuachana na Jide, ama bado anampenda au anatamani mali zake, akiwaza kuna mwingine anapata raha zote za maisha alizokuwa anapata yy toka kwa Jide.
Nimalizie kwa kumsihi Jide kutofanya lolote la kuleta malumbano na huyo mpumbavu, huu mchezo hautaki hasira, yote hii ni sehemu ya maisha.
 
What is"ndi ndi ndi" sielewi maana ya huu wimbo nikahisi labda ndii
 
Inawezekana alikuwa ashapiga mitungi, tumsamehe tu, unajua sis wanaume bana sometimes unaweza piga vyombo ukabugi.

Ogopa sana; kuendesha ukiwa umelewa
Ogopa sana; kutoa ufafanuzi wa tatizo la muda mrefu ukiwa umelewa.
Ogopa sana; kureact mambo ya kifamilia ukiwa umelewa
Ogopa sana; kupost Twitter, au hata JF ukiwa umelewa (japokuwa uzoefu unaonesha, wengi humu huwa ni kawaida yao)
Ogopa sana; kutoa PLEDGE zozote zinazohusu hela ukiwa umelewa.
UTAAIBIKA BAADAE.
 
Rejea kichwa cha habari hapo juu...

Kwa mnaosema jide kadhalilishwa kijinsia nawakumbushia hili,Wiki kadhaa zilizopita Mbunge fulani wa eneo fulani la Ulanga aliwatukana Wabunge wa chama fulani kuwa mpaka wapate nafasi ni lazima waitwe baby,cha ajabu hawa wanaojiita watetezi wa feminism hawakuliona hili kuwa ni udhalilishaji watu wakalifungia macho na kulipuuza,lakini jide alipoambiwa kuwa anakojozwa(Who knows??) na G basi watu wakawaka na kuwa upande wake directly kumtetea na kukemea kwa kusema ni udhalilishaji,swali langu ni kwamba mtu maarufu pekee akidhalilishwa ndio watu watatoka kwenye mapango waliyojificha na kuja kusema kadhalilishwa kijinsia?vipi hao wengine wanaodhalilishwa lakini mnakaa kimya bila kuwatetea?

Kwangu mm hii ishu ya gardner na jide nipo NEUTRAL kila mtu kashamdhalilisha mwenzake,mwngine kwa NYIMBO mwingine kwa live RANT...

ACHENI UNAFIKI.
 
hili jambo kumbe kila mtu humu
anatakiwa awe na upande?
nilikua sijui
 
Inawezekana alikuwa ashapiga mitungi, tumsamehe tu, unajua sis wanaume bana sometimes unaweza piga vyombo ukabugi.

Ogopa sana; kuendesha ukiwa umelewa
Ogopa sana; kutoa ufafanuzi wa tatizo la muda mrefu ukiwa umelewa.
Ogopa sana; kureact mambo ya kifamilia ukiwa umelewa
Ogopa sana; kupost Twitter, au hata JF ukiwa umelewa (japokuwa uzoefu unaonesha, wengi humu huwa ni kawaida yao)
Ogopa sana; kutoa PLEDGE zozote zinazohusu hela ukiwa umelewa.
UTAAIBIKA BAADAE.
Umesema kweli kaka Gadner anaonekana alipiga tungi
 
Bahati nzuri mambo kama haya huwa sifatilii Nahisi maisha ya wengine hasa wasanii yataniumiza akili

Ninachojua na kupenda toka kwake ni muziki wake tu

Hayo mengine yanipite kwa kweli
 
Ukiona watu wanajikita kujadili mambo trivial kama hili ujue ni ...........
 
Watanzania tuna matatizo tunahangaika na watalaka baadala ya kuhangaika na maisha yetu.
 
Back
Top Bottom