Gari gani zuri la kuanzia maisha?

Gari gani zuri la kuanzia maisha?

Umesikia dogo.

Mshikaji anahitaji kujua gari ipi ya kuanza nayo maisha itamfaa kutokana na kipato chake.

Hajasema tumshauri either anunue gari au asinunue. Akinunua akaona linamshinda si ataliuza tu?
Muda mwingine kushauri kupo maana anaweza ananunue sawa ila akauza kwa masimango mm mwenyewe basi tu sikuletaga mawazo yangu humu japo pia alikuepo wa kuniambia usinunue kwanza ila nilishupaza shingo nikajuta na yakapita. Vipato vimekua vigumu tujiwekezeni kwanza gari iwe kifaa kama vifaa vingine kikiwa na umuhimu kamatia ila kwa malipo ya 400k aloo gari bado sioni kama linaumuhimu kwake mawazo yangu tu haya.
 
Sisi wa laki 6 vipi tuendelee kusubir....
Subiri gari iwe kitu cha lazima ila kama unanunua gari ili ukimbilie kazi ya boss aloo safari ipo na usikubali kuwa mmoja wao ww jibane pambana ujitoe kwenye 600k au hata kama utakua hapo ila uwe na vitu vinavyofanya uvikimbilie na gari hapo utaweza nunua gari na kulifaidi matumizi yake.
 
Mwamba gari lolote linafaa kuanzia maisha
Ila kama kipato ni laki 4 ningekushauri suala la gari achana nalo kwa sasa
Ushauri huu utaonekana sio ushauri mkuu watu watakuona ww mbaya kama vipi tumwambie akamatie crown majesta nissan fuga au akamatie hata lc300 maana 400k ukatafute gari mafuta kwa mwezi ngoja nicheke tu na hapo ni kazi za kumkimbilia boss ukiachishwa gari unaona baya
 
Gari ni liability kama hauna necessary and stable financial resouces. I wont advise you to venture into that. Invest to diversify and increae your income stream. Baadae utajikuta tu unanunua gari kama kifaa cha lazima cha kufanyia shughuli zako.
Kuna watu wanahitaji gari hamna namna nyingine..
Mfano
Photographer,
Camera 2.2M
Lens mbili 3.5M
Strobe 1.5M
Stand& soft box 350k
Trigger 150k
Card 1200k
Laptop 1.5M

Hapo lazima gari,ukikabwa ni msiba.
 
Iko zanzibar
4.5M
Haimjui fundi
20230420_133359.jpg
20230420_133736.jpg
20230420_133645.jpg
20230420_133413.jpg
 
Nunueni fekon au kinglion[emoji16][emoji16]
Sinoray mkuu sijawahi kujuta kabisa Vijana wenye kipato kidogo msikatishwe tamaa gari ni muhimu sana kwa maisha ya sasa ila jitahidi uwe na pikipiki pia ... Gari unatumia Mara Moja moja kama kuna issue za kifamilia na mnalazimika kusafiri wote au kuitoa familia out... Usikubali kuishi kiboya hata kama huna pesa nyingi maisha ni haya haya
 
Sinoray mkuu sijawahi kujuta kabisa Vijana wenye kipato kidogo msikatishwe tamaa gari ni muhimu sana kwa maisha ya sasa ila jitahidi uwe na pikipiki pia ... Gari unatumia Mara Moja moja kama kuna issue za kifamilia na mnalazimika kusafiri wote au kuitoa familia out... Usikubali kuishi kiboya hata kama huna pesa nyingi maisha ni haya haya
Kweli mkuu piki piki muhimu, hasa Kama una gari ambayo sio off-road, pikipiki zinasaidia Sana
 
Carina ni gari nzuri hasa kwa wanaoanza kumiliki ndinga. Alafu bei zake sio kali sana na hakina mambo mengi
Ina maana hakunaga gari nyingine nzuri kwa mtu anayeanza kumiliki gari? Maana miaka nenda rudi ushauri wa JF haubadiliki ni Carina tu
 
Wakuu habari,

Naombeni ufafanuzi natamani nipate gari la kuanzia maisha nitakalokaa nalo muda mrefu kidogo, ninakoishi kuna milima ya wastani na vumbi la kati.

Je, ni gari gani inanifaa Mimi, kipato changu ni cha chini kwa mwezi napata laki 4?
Kwa kipato hiki sikushsuri umiliki Gari..
 
Kama ana uwezo wa kununua hawezi shindwa kulihudumia.

Wanaosema kipato hakiruhusu watamwambia asinunue hata TV, sub ufa.

Kwani ukiwa na gari lazima Kila siku liingie barabarani?
Ushauri wangu. Kama unahisi gari litakupa furaha nunua, siku huna pesa ya wese paki tumia usafiri unao tumia kwa Sasa.
Baada ya mwaka tuone hao ambao hawakununua gari Wana kitu gani Cha ziada.
 
Back
Top Bottom