Gari ipi nzuri kati ya Harrier240G na Klugger

Gari ipi nzuri kati ya Harrier240G na Klugger

Kluger V au L? Mi Kluger aisee, kwenye safari iko vzr halafu ni nzito barabarani hazina historia ya kupinduka kabisa
 
Mandolini mwisho wa yote,spare unachonga hata mwenyewe, ikigoma kuwaka huna haja ya kuita watu wasukume,unashuka,unachukua chuma chako unapiga hendeli, ukiona umechacha, unashusha injini unafunga kinu cha kusagia mahindi, au kupigia mahindi.
 
harrier kaka, iko poa imara haitumii mafuta sana
me nina harrier mwaka na nusu sasa na kila weekend naenda nayo moro na kurudi na badoo ipo poa kabisaa.
 
Mi gari Harrier bhana, gari ya uhakika hako ka Kluger utadhani saloon car? Hata nadia inaonekana kubwa zaidi ya hicho ki-Kluger.
 
Hakuna tofauti kwenye engine wala bei ya spare wala ulaji wa mafuta. Engine ni hizo hizo lakini li-Harrier liko comfortable sana.

Chukua Harrier, hutasumbuka spare, spare ni rahisi kuzipata na kwa bei poa pale Ilala used na new one, mafundi wa Harrier mtaani ni wengi kuliko Klugger
 
Nimenunua hivi karibuni ya 2006. Nimefurahia sana comfort, pamoja na build quality. Bila ya shaka zina nguvu ya kutosheleza barabarani kiasi cha kwamba overtaking haikupi shida kabisa. Ila cha kushangaza zaidi ni kuwa matumizi ya mafuta ni wastani. Hayatofautiani na gari zenye engine za lita 2. Clearance ni nzuri sana kwa barabara zetu. Mashimo madogomadogo inafunika vizuri. Na engine ukiitunza ndio mnakwenda nayo mpaka kilomita laki tatu bila ya shida. Ina drive chain. Ktk gari niliowahi kuwa nazo(honda crv, nissan xtrail, na toyota 4runner)mi naona hii ndio best. Nimejaribu kukuekea links zenye specification ila nashindwa kwa ushamba...unaweza ukani pm for more info
Hata kwa honda crv? Coz nimewahi miliki Honda niliikubali kuliko gari zote!!
 
Hata kwa honda crv? Coz nimewahi miliki Honda niliikubali kuliko gari zote!!
Mkuu, sijui kuhusu crv model mpya bila ya shaka maana nazo ni gari nzuri sana. Mi nilikuwa na model ya zamani ya 2000. Nilitamani sana kununua model mpya ila niliogopa baadae resale. Maana watu wana midomo mibaya!!!
 
Kweli mkuu ukisikiliza sana watu unapotea!! Watu waziogopa Honda but ni gari nzuri na ngumu sana!! Honda yenye mileage 200,000 kms ni sawa na Toyota yenye less than 50,000 kms!! Yaani ilifika mpaka 250,000 kms but haikuwahi sumbua engine kabisa!!!!
 
Tatizo sio gari ama mm mkuu. Tatizo uuzaji. Kila mtu ndio ameshaamua kuwa gari ni mbovu na haina spea basi. Utachanganyikiwa kumpata mteja.
 
Tatizo sio gari ama mm mkuu. Tatizo uuzaji. Kila mtu ndio ameshaamua kuwa gari ni mbovu na haina spea basi. Utachanganyikiwa kumpata mteja.
Kweli mkuu!! Honda.... Nissan Mazda haziuziki!! Wengi wanaogopa kwa kujazwa ujinga!! But ni gari nzuri kushinda Toyota!!
 
Back
Top Bottom