Gari ipi pasua kichwa kati ya hizi?

Gari ipi pasua kichwa kati ya hizi?

Brevis ya cc 2000 haipo,haijawahi kutengenezwa na haitakuwepo kamwe.

Engine zilizoko kwny brevis ni hizi tu(2.5L 1JZ-GE,2.5L 1JZ-FSE ,3.0L 2JZ-GE na 3.0L 2JZ-FSE ).

Haya hebu tuwekee aina ya engine yako tuone ni ipi.
Mkuu hivi engine ya Verosa ikoje?
-six cylinder au four cylinder
-inakula wastani wa km ngapi kwa lita
-msaada plz

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wengi tuna kipato cha kawaida. Brevis, xtrail si magari yetu maana yanahitaji utunzaji mzuri na ni gharama.

Nunua rav 4 old model, gx 100, 110 hayo hata ukikosea ukaweka oil chafu hakuna tatzo litaenda tu. Esp rav 4 old Halina masensor mengi. Binafsi silipendi maana lipo kama upo kwenye sufuria, sio comfortable kabisa ila nakushauri nunua hilo hata mjukuu utamrithisha.

Mm ningenunua xtrail au brevis nipambane maana nataka nafasi na utulivu ndani ya gari. Gharama nitapambana na gari ni mkono wangu tu.
Brevis mchanganyo wake ni hatari, raha ipo kwenye 6 cylinder bana asikwambie mtu kitu. Chuma ikiwa silencer tu ni burudani...

Au 1G-FE uikute imepigwa straight pipe kama kwenye gx80 utaipenda.
 
Wanasema rough road inatembea kwa 1l/4km ina ukweli!!?
Ukiona gari imefikia hapo ujue oxygen sensor,fuel filter au plug zina shida. Lazma ukague mfumo wa uchomaji ukirudishia vipuri vipya inarudi kama ilivyotoka kiwandani. Itakupa 8-10km/l ukiwa town trip na highway inaenda 11km/l au zaidi.
 
Wabongo sio wabahili ila wabongo wapenda starehe!
Mbongo anakunywa pombe kila siku 15000 kiwango cha chini,
Ila kwenye mafuta ya gari anakwambia gari inakula mafuta.

Kila kitu kina hasara na faida, cha msingi kipaumbele chako!

Maana huwezi kuwa na gari dar! Lakini ukitakwa kwenda katavi unajiuliza kama gari utarudi nayo.

Achana nakitu inaitwa GX110 au 100 mzee!
Mafuta ni mfuko wako tu.

Kama unaogopa mafuta nunua pikipiki.
Waoga wa kwenda Sheli hao! 🤣🤣🤣
 
Kwa matumizi ya daily mjini na foleni labda ndo wengi wanalalamika mafuta ila kama ulivosema ni gari moja unaenjoy kuendesha ...kwa safariiii unaenjoy zaidi
Brevis gari ya safari, inakupasa uwe na baby walker moja na mnyama. Ukiwa mjini endesha kigoda tu kama Swift au Vits ili kuepusha lawama.
 
Back
Top Bottom