Gari kutetemeka

Huu ufundi umu ndani siukatai ila usilogwe ukashika spana kwa maelekezo ya jamvi
 
Hiyo ni system ya mafuta au mounting au silencer.Siyo kufunga plugs tu,hakikisha hizo plug ni geniune.Na usisahahu kuteremsha tenki la mafuta na kulisafisha na pipes zake zote.Kama tenki ni chafu na kuwa na maji,hata ukifunga plugs mpya,ni bure zitachafuka tena.Kama unatumia AC hakikisha vacuum silencer yako inafanya kazi vizuri
 
Nimegundua kuwa wabongo wengi ni mafundi au idea ya ufundi,na hii imesababishwa na wengi wetu kuwa na magari used ambayo yanafanyiwa maintanace mara kwa mara hivyo kumfanya mmiliki wa gari kuwa na uelewa fulani wa matatizo ya gari.Big up,ni nzuri sana kufahamu matatizo ya gari kwa kiwango fulani kuliko wale wenye mahela ambao wana nunua magari mapya na yakianza kusumbua kidogo wanayauza hawataki kuumiza vichwa na mafundi...
 

usisumbue kichwa wala gari lako kuchokonolewa. hiyo engine mounting tu wala si vinginevyo. hakikisha umebadilisha na kuweka genuine
 
hilitatizo la ball joint lilishawahi nitokea tena kidogo nisababishe ajali bahati nzuri sikuwa katika mwendo kasi
Mara nyingi ball joints zinakupa noma mtu ukiwa kwenye speed ndogo na hasa kwenye matuta au bonde kidogo ndio zinaitika...ukiwa kwenye speed kubwa walaa,sijui kwa nini...hebu mafundi mliomo humu mtuambie kwanini
 
Umeona eh...magari mabovu yanafaida zake mkuu...
 
Mara nyingi ball joints zinakupa noma mtu ukiwa kwenye speed ndogo na hasa kwenye matuta au bonde kidogo ndio zinaitika...ukiwa kwenye speed kubwa walaa,sijui kwa nini...hebu mafundi mliomo humu mtuambie kwanini

ball joint ukiona inasumbua sana bora ubadilishe ununue mpya aisee unaweza jikuta unaendesha gari bila tairi hahahahaaaaa
 
ball joint ukiona inasumbua sana bora ubadilishe ununue mpya aisee unaweza jikuta unaendesha gari bila tairi hahahahaaaaa
Kabisa maana zikiisha mtu unajua kabisa sema ubishi wetu kusogeza siku wakati unajipanga matokeo yake ndo vile zinatupa noma ambapo hujategemea...tena gx100 ndio sana haka kamchezo
 
Mkuu tatizo la hilo gari lako ni kifaa kinachoitwa 'Oxygen Sensor'.
Ili kulitatua tatizo hilo nenda pale Ilala nyuma ya jengo la TRA kuna fremu za used spares. Waambie waifungue Oxygen Sensor ya gari lako na waipime. Gharama ya kufungua na kuipima ni kama Tshs. 10,000. Wanauza pia used Sensors kwa bei ya kati ya Tshs. 40,000 mpaka 90,000 kulingana na mwonekano wako!
Tafadhali tujulishe yatakayojiri.
 
Mi langu limeleta taab u hiyo Mara baada ya fundi lupunguza sailensa ya injini. Nikiwasha na nikipaki kabla ya luizima inatetemeka sana, ila ukopngeza moto kiasi hutulia. Labda jaribu kuajasti ekseleta umaweza on a matokeo.
 

Ebwana ahsante kamanda. Nitaleta majibu haraka baada ya kuwaona. Ahsante
 
Kuna jamaa yangu mafundi wamemlia hela mpaka ameamua kukomaa nayo hivyohivyo. Ukiwa umesimama ukiweka Neutral kutetemeka kunapungua, ndivyo anavyofanya.

Gari yangu ilikuwa na tatizo kama hilo nilitatuaje vile? ... Niliuza!
 
aisee..mbona hukuleta mrejesho?..mi gari ilikuwa ikizima nikaambiwa nianze na kubadilisha plugs, nimebadilisha, kuwasha check engine light imewaka, wakatoa betri kama lisaa limoja, ikazima ila sasa silencer ipo juu naambiwa nikafanya diagnostics, ebu nipe ushauri, nimechoka
 
Habari mkuu niliwahi pata tatizo kama lako gari ilikua haina nguvu na ilikua ikitetema sana. Tena nimewahi pata mara mbili shida hii. Mara ya kwanza ilikata piston ling ikaruhusu mafuta kuingia ktk turbo ikawa inavibrate sana na kutoa moshi mweupe. Siku nyingine ikaja kichanganya oil na maji ikawa inatetema sana. Kama gar yako ni ya turbo nikuelekeze mafundi wazur ambao ndio wanatengeneza gar yangu amini ikitoka hapo tatizo linakata
 
Kutetemeka kwa gari inatokana na yafuatayo kwa experience yangu.
1-misi gari inakua haichomi vizuri mafuta. Kama ni ya petrol check kuanzia spark plugs hadi fuel pump inaweza kua chafu.
Kama ni dizeli cheki sehemu inayopitisha upepo fuatilia mfumo wa inlet na outlet ya mafuta mpaka kwenye pump.
2-clutch ikiwa haitenganishi vizuri gari hutetemeka.
 
Inaweza kuwa engine mountain (sijui nimepatia ndivyo inaitwa).
Gari lakl ni passo 3 pistons?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…