King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Sailensa ipo juu waambie waipunguze.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haaa!!! Unahangaika na starlet! !!!! Tupilia hukooooo. Nunua nyingine. Tatizo kwisha kabisa.
Hiv zimefika bei gan sasa hiv maana nilishauliza sana lakin sipati jibu la uhakika, naomba unisaidie mkuu!!!
Kutetemeka kwa gari mara nyingi hutokana na mambo mawili. Kwanza ni engine mounting or exaust mounting na kama sio hivyo basi tairi pia huwa ni sehem ya pili ya tatizo hasa kama hazijajazwa upepo sawa na ama tairi ikiwa ina nundu au uvimbe na ama kama haijafanywa wheel allignment
And balance vinginevyo ni kuangalia inatetemeka all timea au ni baada ya speed flan
Mkuu mie sio fundi lkn nilipata hilo la kutetemeka kwa gari few weeks ago...Nilidhani ni Engine Mounting maana pia huwa inasababisha mtetemo wa gari ikiwa imeisha au nuts kulegea...lakini nilipopeleka kwa mafundi sema ndo hivyo tena niko nchi za watu, wakaweka kwa computer na kukuta kitu kwenye engine so wakakitoa na sasa mambo yako fresh, Je, ukiendesha usukani huwa hutetemeki, kama unatetemeka jaribu kufungua tairi na kusafisha maybe kuna matope yameingia kwa rims...Au peleka kwa mafundi wenye computer waconnect then kila tatizo litaonekana na kuwa solved mkuu...
Kaka ukiwa unatembea imetulia kabisa. Ukisimama na ukiwa parking ndio steering inatetemeka
Pole sana broo, mimi pia nilianzia maisha na hiyo Glanza V, ina mvuto mzuri, inatembea sana, inatulia road, ni potabo kiukweli ilifanya maisha ya ujana wangu kwa kuanzia nijiskie raha.
Hilo tatizo linalokusumbua mimi pia lilinipata, actuaaly watumiaji wengi wa glanza wanalia na hicho kitu. nilitumia wataalamu kibao na kutumia hela kibao lkn liliendelea ingawa sikufika TOYOTA, niliendelea kutumia mpaka alivojitokeza wa kunivua kwa mkwanja mzuri tu maana Glanza inauzika. Hongera kumiliki Kiglanza bana achana na kejeli za wadau hawajui utamu wake na hilo tatizo lisikuumize kichwa.
pole mkuu. Je iliwahi kupata ajali, kama haijawahi basi nenda kafanye wheel balancing. Ila ni vizuri ukifanya na wheel allignment
Wadau wamesema mengi ya muhimu,nami naomba kuongezea japokuwa mimi siyo fundi magari,niliwahi kupata tatizo kama hilo japokuwa gari haikuwa inatetemeka sana lkn nilipoenda kwa fundi akabadilisha spark plugs na tatizo likaisha.
Kama gari yako inatumia petrol,wakati likiwa kwenye silence jaribu kuangalia kama zote zinachoma,kwa kuchomoa moja baada ya nyingine.
Dah ahsante kwa kunipa moyo na kidude changu. Kiukweli nakienjoy sana kiasi kwamba sitaki kukiuza japo jamaa wanafika bei zaidi ya niliyonunulia. Ni kigari kizuri sana. Tatizo kilikuja nalo toka nakichukua japan mwezi wa tisa mwaka 2012 hadi Leo. Ninatamani tu kulitoa hili tatizo.... Wewe lilianzia kwako au ulilikuta?
Dah ahsante kwa kunipa moyo na kidude changu. Kiukweli nakienjoy sana kiasi kwamba sitaki kukiuza japo jamaa wanafika bei zaidi ya niliyonunulia. Ni kigari kizuri sana. Tatizo kilikuja nalo toka nakichukua japan mwezi wa tisa mwaka 2012 hadi Leo. Ninatamani tu kulitoa hili tatizo.... Wewe lilianzia kwako au ulilikuta?
Hili tatizo liliwahi kunitesa sana kwenye MAZDA PREMACY nilibadilisha plugs sijui cables,lambwa sana hela na mafundi lakini tatizo likawa pale pale.
Kuna jamaa yangu akashauri tufungue sensa ya air cleaner kufungua tukakuta maji kibao,kumbe wakati wa kuosha injini yaliingia.Tuka kausha maji kurudishia mpya !! sijajua kama glanza ina hiyo sensa !!
Labda
1 - kutakuwa na na plug hazichomi vizuri au zimekufa
2 - mounting
3 - mfumo wa umeme
4 - valves
5 - nk
Mkuu kilikuja kikiwa shwari tu nikapigia msele kama miezi saba after there ndo kikaanza huo mchezo, lkn kumbuka ukikweka neutral mtetemo unapotea ama ukishusha silensa pia mtetemo unapotea kiujumla epuka kudanganywa na mafundi kua spea fulani imeisha, maana mimi niliambiwa engine mounting nikachenj, ikawa vilevile, nikaambiwa plugs -ikawa no, nikaambiwa rims nikabadili so nilijikuta nafanya kila nililoambiwa na mafundi bila mafanikio. mwisho niliamua kukaaa nayo hivohivo na hata niliyemuuzia yuko Tbt anayo iko hivohivo inachapa mwendo hadi leo na hata akinipita road huwa ananipita kama nimesimama kiukweli kinakimbia na exhaust inamakelele so hua natamani nikirudishe but kishatoka. so we tulia nacho ukifika foleni put on neutral then engage D unasepa broo. Pamoja sana we kikikuchosha nisukumie bado natamani kiwe kwenye himaya yangu, i like it and i enjoy its move and size so keep it.
Wadau naomba mnisaidie na mimi pia. gari yangu ikifikia speed 90 inatetemeka lakini ukivuka hiyo speed inatulia. je tatizo lawezakuwa nini?
Gari Kutetemeka ni wheel Balancing mkuu,cheki na tairi zako za mbele kama zinalika upande mmoja wa ndani zote mbili ujue na wheel alignment inatakiwa Hapo!nenda mobile clinic pale opposite na TX Market kinondoni wheel aligment elfu 20 na wheel balancing elfu 20 jumla elfu 40!ALL THA BEST MKUUHabari wanajamii. Nina tatizo wandugu. Gari yangu imekuwa na tabia ya kutetemeka engine kiasi kwamba hadi stealing inatetemeka. Hii hutokea hasa nikiwa nimesimama. Gari ikitembea haitokei. Nimejaribu kucheki na baadhi ya mafundi ila hamna mafanikio. Gari niliagiza japan na tatizo lipo toka nimelinunua. Naomba msaada wenu kama kuna ameshapata masaibu haya na vilevile labda Fundi ambaye anaweza nisaidia.
Ahsanteni wandugu