Gari kutetemeka

Gari kutetemeka

Litakuwa limewekewa vibration ya tecno+itel +huawei! Km cjakosea. Suluhisho waone mafundi simu watoe hizo vibrations
 
Yap. Kunasimama lakini ukirudi kwenye D mtetemo unarudi
Pole sana hii itakuwa ni Engine Mounting na hata check GearBox mounting
kwani Crankshaft inayobeba pia piston huwa na mzunguko mkali hivyo ukiweka Free unatenganisha mawasiliano na hivyo vitu (Engine,Gearbox na Flywheel) ila unapoingiza (engage) gear D (drive) ina maana unaunganisha na mtetemo unaotoka katika Engine na Bodi zima la gari yako.
Cha kufanya Fungua Boneti (kifuniko cha Engine hapo mbele) umwambie dreva mwenzako awshe gari na kuongeza mafuta utauona huo mtetemo na jinsi unavyopishana na Bodi la gari
 
Tatizo mafundi wengi tunaowatumia ni mafundi wa chini ya miembe na kwa hakika wengi wao wanafanya kazi kwa kufundishana hapohapo gereji. Wengi wao wanafanya kazi hizi kwa kubahatisha na hawana muda wa kuingia darsa kujielemisha licha ya mabadiliko ya kila kukicha ya teknolojia matokeo yake unampelekea kitu kidogo tu ona fundi anavyohaha! Mimi niliwahi patwa na tatizo kama hilo lilinisumbua kwa muda mrefu kabla sijapata suluhisho kwa njia hizohizo za kubahatisha. Unaenda kwa fundi huyu anakuelezea tatizo ni hili anakorokochoa gari bila mafanikio unaacha nae na kwenda kwa mwingine. Nashukuru tatizo liliisha japo ni vigumu kuamini nikisema sijui liliisha vipi na kwa fundi yupi. Ila maelezo yao yalikuwa ni kama hayo yaliyoelezwa na wengi hapo juu kama plug, mounting, mafuta kuzuiwa nk...
 
Walio sema wadau hapo juu ni muhimu sana bt me nashauri pia fundi ajaribu kuangalia silencer.kwani inaweza ikawa chini sana so anaongeza kidogo.

Exactly,shida ikO apo tu ila watu Hawajui, ndio mafundi ulia ela....
 
Duh, kuna watu hawajatulia kabisa, aani nimeishia kucheka ka mwehu
 
Mkuu hapo SOLN IKO JAPAN RUDISHA ULIPOLIPATA WAKATI. TYKISUBIRI MAJIBU YA. UONNGO NA NAMBA ZA S.......
 
Mimi nakushauri vilevile tatizo likiendelea nenda kwa mganga akapige ramli itakua kuna mtu kaliroga sio bure-LMAO
 
Ushauri wangu...peleka sehemu ambapo wana car diagnostic tool.....wataweza kukwambia tatizo hasa ni nini.
 
Wadau naomba mnisaidie na mimi pia. gari yangu ikifikia speed 90 inatetemeka lakini ukivuka hiyo speed inatulia. je tatizo lawezakuwa nini?
 
Wadau naomba mnisaidie na mimi pia. gari yangu ikifikia speed 90 inatetemeka lakini ukivuka hiyo speed inatulia. je tatizo lawezakuwa nini?

pole mkuu. Je iliwahi kupata ajali, kama haijawahi basi nenda kafanye wheel balancing. Ila ni vizuri ukifanya na wheel allignment
 
Habari wanajamii. Nina tatizo wandugu. Gari yangu imekuwa na tabia ya kutetemeka engine kiasi kwamba hadi stealing inatetemeka. Hii hutokea hasa nikiwa nimesimama. Gari ikitembea haitokei. Nimejaribu kucheki na baadhi ya mafundi ila hamna mafanikio. Gari niliagiza japan na tatizo lipo toka nimelinunua. Naomba msaada wenu kama kuna ameshapata masaibu haya na vilevile labda Fundi ambaye anaweza nisaidia.
Ahsanteni wandugu

Ni starlet glanza mkuu. Yenye turbo. Fundi wengi walioiona walisema hivyo ila wakitizama wanasema sio

Haaa!!! Unahangaika na starlet! !!!! Tupilia hukooooo. Nunua nyingine. Tatizo kwisha kabisa.
 
Back
Top Bottom