Sawa kabisa usemacho, nilisimamishwa karibu na Msimbazi center ya kwamba nadaiwa elf 30 kwa kosa la speed kwenye eneo la 30kph leseni inayosoma sio yangu,gari ikazuiwa nikaenda kulipa baada ya hapo nilienda trafiki makao makuu kuonana na RTO wakaangalia wakanishauli niende kitengo cha tehama makao makuu mtaa wa ghana na ohio, mwisho wa siku trafiki aliyeko Songea ndo aliyeandika faini hiyo na alikosea kusoma namba za gari nikapewa namba yake tukawasiliana akanirudishia pesa yangu na kuomba radhi kwa usumbufu nilioupata.
Hawa hawakujali umakini wowote. Lengo lao lilikuwa kukusanya mapato kuvuka malengo.
Kwa dhuluma zao wengi wamekuwa wahanga wa dhuluma zao.
Serikali ilipaswa kuwajibika na hasa kuwafidia wahanga wote wa dhuluma hizi wakiwamo wale wa faini za kwenye zebra crossing. Ikumbukwe madereva kinyume cha sheria walikuwa wakishurutishwa kusimama kabisa hata kama hakukuwa na mtembea kwa mguu aliyehitaji kutumia zebra husika.