Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
Gari namba MT 0128 Mali ya Jeshi la Magereza ,ikiwa na Wafungwa inatumika kupandisha Bendera za CCM katika nguzo za barabarani hapa Dodoma Mjini Leo 7.07.2020. Jeshi la Magereza limegeuzwa nguvu kazi ya CCM

 
Kuelekea mkutano wa ccm hapo kesho jijini Dodoma leo hii zimetumika mali za umma kupandisha bendera za chama hicho kama inavyo onekana hapo chini.

Kwa wajuzi wa mambo ya kisiasa tunaomba mtuelekeze kama ni sahihi chama cha kisiasa hasa kwenye mfumo wa vyama vingi kutumia rasilimali za umma kufanikisha shughuli binafsi kisiasa.
 
Hao wafungwa watakuwa ni wanaccm!
 
kwa watu walio nyuma kwenye human civilization and democracy hawana uwezo wa kuseparate kati ya shughuli za chama na serikali kwao ni kitu kimoja!! shame on us!! kulazimisha mambo ya wazungu kumbe uelewa wetu ni ziro!!!unaweka sheria za vyama vingi halafu unaua wapinzani!! aibu sana!!
 
Ngoma ikivuma sana ujue inakaribia kupasuka, ndiyo wanamalizia malizia utukufu wao, soon Taifa litarudi kwenye misingi ya Utawala Bora na ustaarab ambapo tofauti za kiitikadi hazitaonekana ni uhasama, tutafoutiana kwenye hoja lakini tutabaki kuwa wamoja kama Taifa.
 
Viongozi wa CCM wamejisahau sana. Kila kitu wanaamini kuwa ni chao. Wasome historia ya anguko la dola la kirumi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…