Gari nimenunua Afrika Kusini Milioni 4, kodi Tanzania Milioni 18!

Gari nimenunua Afrika Kusini Milioni 4, kodi Tanzania Milioni 18!

Ndo maana siku hizi unakuta lundo kny mnada bandarini. Bora kupata maelezo ya kutosha kabla ya kuagiza au kuleta, na kuhakikisha unamudu.. Kweli 'hapa kodi tu'
 
Kwa nini mnajiingiza wenyewe matatizoni halafu mnaanza kulaumu????
Humu ndani kuna mmoja wetu aliwahi kutoa ushauri kuwa, kabla ya kuagiza/kununua gari nje hebu pelekeni hizo stats za gari hilo TRA waweze kuwashauri kuhusu kodi stahili.
Lakini kama kawaida yetu tunalalamika baada ya kujiingiza kwenye matatizo usiyotarajia.
Soma thread uielewe! Kwa hiyo mtu anaishi ulaya au Zambia akaulize kwanza gharama tra yaani huko aliko haruhusiwi kutembelea gari anayoitaka????? Hoja ni kwamba kodi zetu hapa ni kubwa mnoooo kuliko hata nchi zinazotumia bandari yetu! Hatulalamiki Leo tu tunataka kusolve tatizo kubwa happa
 
Inawe
Ulikaa nalo ughaibuni muda gani kabla ya kulileta? Kama ulitumia gari hilo kwa kipindi kilichozidi mwaka mmoja kabla ya kurudi nyumbani hulipi kodi. Hii ni pamoja na vifaa vyote vya nyumbani ambavyo ulikuwa unavitumia huko ughaibuni.
Inawezekana kuna tra 2 aisee nitaleta mrejesho hapa picha likiisha
 
Kama nimemuelewa vizuri ni kwamba jamaa ni kama alikua anaishi ZA for sometimes na hiyo gari aliinunua kwa matumizi yake huko huko ZA so kaamua kurudi nyumbani na ndio kakutana na hayo makitu! KWa ufupi, Tanzania bado inatenda miujiza.
Kwenye kampuni moja niliokua nafanya nayo kazi, jamaa mmoja kutoka West Africa huko alikujaga kwenye hiyo Kampuni yetu, nadhani alikua anatokea Guine huko (is one of the French speaking country in Africa ) so mimi pamoja na wenzangu tukawa tunatafuta magari USED from Japan, kuna PRADO moja hivi tulilipenda (tulikua tunafurahisha macho tu) lilikua linagharimu ka $ 5000 hivi kwa maana ya CIF,tulipokwenda kwenye calculator ya TRA ilionesha KODI kama Tsh 18M plus na change hivi, yule jamaa akatuuliza, "In Tanzania, are you having vihecle industries!?" Tukamuuliza, Why Mr Camara (Camara jina lakutunga). Yeye alishangaa kwanini KODI kubwa namna hiyo ilihali hatuna kiwanda/viwanda vya magari. Kwake yeye, KODI kubwa sometimes inawekwa iliku discourage importations ya vitu vinavyo weza kutengenzwa locally.
Point aiseee
 
Soma thread uielewe! Kwa hiyo mtu anaishi ulaya au Zambia akaulize kwanza gharama tra yaani huko aliko haruhusiwi kutembelea gari anayoitaka????? Hoja ni kwamba kodi zetu hapa ni kubwa mnoooo kuliko hata nchi zinazotumia bandari yetu! Hatulalamiki Leo tu tunataka kusolve tatizo kubwa happa
Nilichosema mimi ni kwamba kama ulikuwa unaishi nje ya nchi zaidi ya mwaka mmoja na hilo gari umekuwa ukilitumia huko uliko kwa kipindi chote hicho, wakati wa kurejea hulipi kodi [iwapo utathibisha kama hilo gari umelimiliki na kulitumia huko ulipo kwa kipindi hicho chote] Lau kama umenunua hilo gari kwa kipindi chini ya hapo, inabidi ulipe kodi. Kwa vigezo na masharti ingia kwenye website yao halafu uwaulize watakujibu hata ukiwa mwezini.
Wengi mnalalamika kwa kuwa mnanunua magari kwanza kabla ya kufahamu taratibu za kuingiza gari nchini pamoja na kodi zake. Kwenye website ya TRA kuna sehemu imeandika' Used Motor Vehicle valuation system, hii inakupa details za namna ya kukokotoa thamani ya gari ukiwa huko huko ulipo.
Humu ndani tunasaidiana ushauri tu
 
Jamani hii nchi Mungu tu aingilie kati!

Unaweza ukafurahi ukiwa ugenini dakika unagonga tu kibali kukanyaga Ardhi ya bongo na vimizigo vyako ulivotokanavyo kuhemea huko unakutana na ngumi za USO!

Yaani Toyota Hilux nimenunua Milioni 4.5 Afrika Kusini calculator ya TRA hapo bila kupepesa macho mzee baba anataka Tsh. Milioni 18.4!

Kurudi nalo nilikotoka ni issue! Wakati Afrika Kusini nimetembelea gari hiyo bila mushkeli kabisa! OMG!

Hapa kazi tuu
Ndio hivyo chief. Hiyo ndio Tz. Karibia familia zote zingekuwa na magari kodi ingekuwa rafiki kama nchi jirani kama malawi hivi. Mfano unaweza kupata corola Dubai kwa milioni 2.7 Tsh pamoja na usafiri. Lakini kufika hapa utaambiwa kodi ni Tsh. Milioni 8. Lakini kwa gari hilo hilo ukienda Malawi wanalipia milioni 2+ kodi. Kwanza gari sio anasa kama wengine wafikiriavyo,(jama viongozi huko juu wanavyotafsiri gari) ,gari ni kitendea kazi. Mfano kazi ya kuifanya kwa mizunguko ya masaa ma5,usipokuwa na gari utaifanya hata kwa siku 3 na ikiwezekana gharama itaongezeka. Nimesema karibia kila familia ingekuwa na usafiri ksbb Watz ni wachakarikaji sana sana. Huwezi kuwaringanisha na nchi kama Zambia na Malawi. Ila tu tunabaniwa sana kwenye kodi na serikali yetu
 
Nilichosema mimi ni kwamba kama ulikuwa unaishi nje ya nchi zaidi ya mwaka mmoja na hilo gari umekuwa ukilitumia huko uliko kwa kipindi chote hicho, wakati wa kurejea hulipi kodi [iwapo utathibisha kama hilo gari umelimiliki na kulitumia huko ulipo kwa kipindi hicho chote] Lau kama umenunua hilo gari kwa kipindi chini ya hapo, inabidi ulipe kodi. Kwa vigezo na masharti ingia kwenye website yao halafu uwaulize watakujibu hata ukiwa mwezini.
Wengi mnalalamika kwa kuwa mnanunua magari kwanza kabla ya kufahamu taratibu za kuingiza gari nchini pamoja na kodi zake. Kwenye website ya TRA kuna sehemu imeandika' Used Motor Vehicle valuation system, hii inakupa details za namna ya kukokotoa thamani ya gari ukiwa huko huko ulipo.
Humu ndani tunasaidiana ushauri tu
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
 
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
Kama ni hivyo basi aidha nunua hapa nchini au fanya kama tufanyavyo wengine-mwendokasi
 
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
Kodi kubwa sio kwa magari pekee..

Waganda wanaagiza mizigo ya biashara nje, wanapitishia bandari ya Dar, inasafirishwa kwa barabara umbali zaidi ya km elfu 1 hadi kwao.. Cha ajabu wafanyabiashara wa K'koo wanasafiri hadi uganda, wananunua huko, wanasafirisha hadi K'koo Dar wanauza na kupata faida..

Ungefikiri kwa kuwa Tz ndo kuna bandari waganda wangekuja kununua Dar, lkn sivyo, ni kinyume chake..
"hapa KODI tu"
 
Kodi kubwa sio kwa magari pekee.. Waganda wanaagiza mizigo ya biashara nje, wanapitishia bandari ya Dar, inasafirishwa kwa barabara umbali zaidi ya km elfu 1 hadi kwao.. Cha ajabu wafanyabiashara wa K'koo wanasafiri hadi uganda, wananunua huko, wanasafirisha hadi K'koo Dar wanauza na kupata faida.. Ungefikiri kwa kuwa Tz ndo kuna bandari waganda wangekuja kununua Dar, lkn sivyo, ni kinyume chake.. "hapa KODI tu"
Hiki kitu ndio inatakiwa serikali yetu kufikiri na kuja na majibu; nadhani tunaishi kwenye ulimwengu wa ushindani, is not practical kwa Mtanzania kwenda kufata mizigo Kampala, zaid ya 1300KM, nashukuru na wewe umeliona, wafanya baishara wengi wa Mwanza hasa wa spear za magari, nguo nk hufata bidhaa zao Uganda na kuja kuuza Mwaza, Shinyanga, Tabora nk na Waganda walivyo ona fursa hiyo, hadi mabasi yao wanaleta Mwanza Daily to Kampala!
 
Kuna jamaa hapa majuzi ameagiza gari bila kuhakiki gharama za bandari, ameshangaa madeni yaliyomuandama badala ya gari kufika.....
 
Mkuu hujachelewa kama unaweza nenda SA Pretoria Sunnyside,Ministry of Export and Trade utapeleka documents za hiyo gari zote kama gari imetengenezwa SA kwa Nchi za SADC wana makubaliano ya kupunguziana kodi utalipa nusu ya kodi uliyoiona kwenye calculator ya TRA ipo kisheria ila TRA ilitakiwa watoe Elimu hiyo mnaosafiri mjue ukikaa kimya ulinalipa zote Mimi Toyota Land cruiser hard top pick up ya 2013 ilisoma 47 Million kodi nilipokuja na documents za SA ikapungua mpaka nusu yake na kule hivyo vibali unapata ndani ya siku tatu...hiyo ni kwa gari zote mpya na used ilimradi iwe ni SA brand sio nao waagize huku upate unafuu hapana...
Hapo umenipa elimu mkuu, nilikuwa napiga hesabu namna ya kuagiza gari South Africa maana kwanza ni karibu, pili unaweza enda mwenyewe ukachagua gari physically, gari zao zimeandikwa kingereza kwenye system zao, zaidi naweza drive kuja Tz , mkuu ubarikiwe kwa kutufungua!
 
Kodi kubwa sio kwa magari pekee.. Waganda wanaagiza mizigo ya biashara nje, wanapitishia bandari ya Dar, inasafirishwa kwa barabara umbali zaidi ya km elfu 1 hadi kwao.. Cha ajabu wafanyabiashara wa K'koo wanasafiri hadi uganda, wananunua huko, wanasafirisha hadi K'koo Dar wanauza na kupata faida.. Ungefikiri kwa kuwa Tz ndo kuna bandari waganda wangekuja kununua Dar, lkn sivyo, ni kinyume chake.. "hapa KODI tu"
Kungekuwa na waandishi wa habari smarter wangefanya documentary ya namna hivi vitu vinafanyika yaani bidhaa kutoka bandari ya Dar hadi uganda na watanzania wanaoenda Uganda kununua bidhaa na kuzileta Kkoo na wakauza kwa faida.
Then wairushe jamii na serikali waone na kujifunza!
 
Mkuu ishu ya korosho tuachie tu, maana vichwa vinauma tu na wala hatujui hiyo pesa itapatikana mwaka gani
Sera tuliyonayo dhidi ya wananchi ni pasua kichwa .
Mpakani cement ya Kenya ni 16,000/= Lakini ole wako uitumie !! Unatakiwa ununue ya Tz 21,000/=.

Huwa najiuliza ni lini watu wote watachukuliwa kama wakulima wa korosho ?!. Kama mwingine anahangaika na mahindi mwaka mzima, leo wa korosho na jeshi lisaidie 😳 😀
 
Haya wadau za Christmas jamani! Naleta mrejesho! Baada ya kulia sana sana juu ya kodi mwisho nimelipa mil 13.4
 
Kazi ipo hawa tra huwa hawafanyi research ya hizi kodi zao wao wanapenda kuona figure insoma milions tu.
 
Hilo ulipaswa kuingiza kama mtalii kisha ukiwa bongo unatafuta plate no ya hilux kama hiyo unadunda mtaani
 
Back
Top Bottom