Gari nimenunua Afrika Kusini Milioni 4, kodi Tanzania Milioni 18!

Ndo maana siku hizi unakuta lundo kny mnada bandarini. Bora kupata maelezo ya kutosha kabla ya kuagiza au kuleta, na kuhakikisha unamudu.. Kweli 'hapa kodi tu'
 
Soma thread uielewe! Kwa hiyo mtu anaishi ulaya au Zambia akaulize kwanza gharama tra yaani huko aliko haruhusiwi kutembelea gari anayoitaka????? Hoja ni kwamba kodi zetu hapa ni kubwa mnoooo kuliko hata nchi zinazotumia bandari yetu! Hatulalamiki Leo tu tunataka kusolve tatizo kubwa happa
 
Inawe
Ulikaa nalo ughaibuni muda gani kabla ya kulileta? Kama ulitumia gari hilo kwa kipindi kilichozidi mwaka mmoja kabla ya kurudi nyumbani hulipi kodi. Hii ni pamoja na vifaa vyote vya nyumbani ambavyo ulikuwa unavitumia huko ughaibuni.
Inawezekana kuna tra 2 aisee nitaleta mrejesho hapa picha likiisha
 
Point aiseee
 
Nilichosema mimi ni kwamba kama ulikuwa unaishi nje ya nchi zaidi ya mwaka mmoja na hilo gari umekuwa ukilitumia huko uliko kwa kipindi chote hicho, wakati wa kurejea hulipi kodi [iwapo utathibisha kama hilo gari umelimiliki na kulitumia huko ulipo kwa kipindi hicho chote] Lau kama umenunua hilo gari kwa kipindi chini ya hapo, inabidi ulipe kodi. Kwa vigezo na masharti ingia kwenye website yao halafu uwaulize watakujibu hata ukiwa mwezini.
Wengi mnalalamika kwa kuwa mnanunua magari kwanza kabla ya kufahamu taratibu za kuingiza gari nchini pamoja na kodi zake. Kwenye website ya TRA kuna sehemu imeandika' Used Motor Vehicle valuation system, hii inakupa details za namna ya kukokotoa thamani ya gari ukiwa huko huko ulipo.
Humu ndani tunasaidiana ushauri tu
 
Ndio hivyo chief. Hiyo ndio Tz. Karibia familia zote zingekuwa na magari kodi ingekuwa rafiki kama nchi jirani kama malawi hivi. Mfano unaweza kupata corola Dubai kwa milioni 2.7 Tsh pamoja na usafiri. Lakini kufika hapa utaambiwa kodi ni Tsh. Milioni 8. Lakini kwa gari hilo hilo ukienda Malawi wanalipia milioni 2+ kodi. Kwanza gari sio anasa kama wengine wafikiriavyo,(jama viongozi huko juu wanavyotafsiri gari) ,gari ni kitendea kazi. Mfano kazi ya kuifanya kwa mizunguko ya masaa ma5,usipokuwa na gari utaifanya hata kwa siku 3 na ikiwezekana gharama itaongezeka. Nimesema karibia kila familia ingekuwa na usafiri ksbb Watz ni wachakarikaji sana sana. Huwezi kuwaringanisha na nchi kama Zambia na Malawi. Ila tu tunabaniwa sana kwenye kodi na serikali yetu
 
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
 
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
Kama ni hivyo basi aidha nunua hapa nchini au fanya kama tufanyavyo wengine-mwendokasi
 
Hiyo calculator ya TRA sio siri, malalamiko ya watu sio kujua au kutokua, issue ni kwamba KODI za magari Tanzania zipo juu mno!
Kodi kubwa sio kwa magari pekee..

Waganda wanaagiza mizigo ya biashara nje, wanapitishia bandari ya Dar, inasafirishwa kwa barabara umbali zaidi ya km elfu 1 hadi kwao.. Cha ajabu wafanyabiashara wa K'koo wanasafiri hadi uganda, wananunua huko, wanasafirisha hadi K'koo Dar wanauza na kupata faida..

Ungefikiri kwa kuwa Tz ndo kuna bandari waganda wangekuja kununua Dar, lkn sivyo, ni kinyume chake..
"hapa KODI tu"
 
Hiki kitu ndio inatakiwa serikali yetu kufikiri na kuja na majibu; nadhani tunaishi kwenye ulimwengu wa ushindani, is not practical kwa Mtanzania kwenda kufata mizigo Kampala, zaid ya 1300KM, nashukuru na wewe umeliona, wafanya baishara wengi wa Mwanza hasa wa spear za magari, nguo nk hufata bidhaa zao Uganda na kuja kuuza Mwaza, Shinyanga, Tabora nk na Waganda walivyo ona fursa hiyo, hadi mabasi yao wanaleta Mwanza Daily to Kampala!
 
Kuna jamaa hapa majuzi ameagiza gari bila kuhakiki gharama za bandari, ameshangaa madeni yaliyomuandama badala ya gari kufika.....
 
Hapo umenipa elimu mkuu, nilikuwa napiga hesabu namna ya kuagiza gari South Africa maana kwanza ni karibu, pili unaweza enda mwenyewe ukachagua gari physically, gari zao zimeandikwa kingereza kwenye system zao, zaidi naweza drive kuja Tz , mkuu ubarikiwe kwa kutufungua!
 
Kungekuwa na waandishi wa habari smarter wangefanya documentary ya namna hivi vitu vinafanyika yaani bidhaa kutoka bandari ya Dar hadi uganda na watanzania wanaoenda Uganda kununua bidhaa na kuzileta Kkoo na wakauza kwa faida.
Then wairushe jamii na serikali waone na kujifunza!
 
Mkuu ishu ya korosho tuachie tu, maana vichwa vinauma tu na wala hatujui hiyo pesa itapatikana mwaka gani
 
Haya wadau za Christmas jamani! Naleta mrejesho! Baada ya kulia sana sana juu ya kodi mwisho nimelipa mil 13.4
 
Kazi ipo hawa tra huwa hawafanyi research ya hizi kodi zao wao wanapenda kuona figure insoma milions tu.
 
Hilo ulipaswa kuingiza kama mtalii kisha ukiwa bongo unatafuta plate no ya hilux kama hiyo unadunda mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…