JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Hizi engine za kisasa za toyota ambazo zimekuja na Aluminium block ni nzuri ikiwa haijawahi pata shida ya kuchemsha.
Ila kama ikitokea ikachemsha halafu ukarekebisha bado matatizo ya kuchemsha yakaendelea, nakushauri achana kabisa na hiyo engine sababu vinginevyo hakuna rangi utaacha kuona.
NZ, ZZ, AZ, GR, na engine zingine zote za toyota zenye aluminium blocks ni za kipuuzi mno zikishaanza kuchemsha.
Yaani gari inachemsha matundu ya bolt ya block yanatanuka halafu Bolt za Cylinder head zinaruka thread kwenye Block. Baada ya hapo bolt hazifungi tena. Wajapani wanajua wenyewe walivyodesign blocks zao.
Usije kujidanganya kwamba utaenda kusurface cylinder head au kuchonga thread za Block utumie bolt nyingine. Majanga hayatoisha kwenye hiyo gari.
Mjerumani anatumia block hizo hizo za aluminium kwa sasa tena mpaka kwenye engine za diesel. Lakini zikichemsha hutokutana na hicho kinachotokea kwenye toyota.
Mjerumani alitumia akili, Block Aluminium ila sehemu za kufunga Bolt kaweka cast iron. Miaka 800 hakuna Bolt itaruka thread.
Sijajua kwa gari zingine za kijapani. Ila kwa Toyota hali ndio hiyo.