Gari wanazohitaji waTanzania hazipatikani dunia nzima

Gari wanazohitaji waTanzania hazipatikani dunia nzima

Mtanzania anahitaji gari moja yenye sifa zifuatazo.

1-isiwe inakula mafuta, ikiwa inakula mafuta utasikia (jini hilo).
2-Gari ambayo ikiharibika vipuri vipatikane kwa bei nafuu.
3-Gari ambayo ina acceleartion kubwa na top speed kubwa mfano 220km/hr....300km/hr
4-Muonekano mzuri na imara.
5-Yenye gharama nafuu katika utengenezaji.
6-Iwe na uwezo wa kupita off-road.
7-Isiwe old model.
8-isiwe na mifumo na sensors nyingi za umeme (mfano bmw).

Na kinachonimaliza kabisa...

9-Iwe na bei nafuu.

Utabaki kuendesha ist na vitz mpaka unazeeka..

Ushauri kwa waTanzania wenzangu, tutabaki kuwapigia makofi na kuwasifia wanaume wenzetu wanaomiliki range rover na discovery,bmw x6,v8, benz n.k...
Huwezi hata siku moja kupata gari yenye hizo sifa zote thats why bara bara zimejaa ist, wish, crown, harrier n.k

Kumbuka unapokwenda kununua gari fahamu gari haitumii mtori wala uji, gari inatumia mafuta, brevis tu zimewashinda kila siku mnapiga kelele, mtamiliki gari gani nzuri yenye kasi, luxury, comforatable na speed kama mnakimbia majukumu?

Badilikeni ndugu zangu, acheni maisha ya kukariri, kwa East Africa naona sisi ndio tunamiliki gari za kishamba kuliko wote.




1200px-2018_BMW_X6_xDrive30d_M_Sport_Automatic_3.0_Front.jpg


2021-Tundra-1-copy.jpg


USC90JES052F021001.jpg
Tunaenda na uchumi wa kati ulivyo, we ni Mtanzania wa wapi na hatuna uraia pacha
 
Dunia hii ni sehemu ipi TOYOTA hakubaliki????? 25 Best-Selling Cars, Trucks, and SUVs of 2020 Kutoka makampuni makubwa yote ya magari katika gari 25 zilizoshindanishwa na kuingia top 25 USA, TOYOTA kaingiza gari sita na Japan kwa ujumla [emoji627] kaingiza gari 14. karibia 50+% ya soko la magari kaliteka Mjapan na Mjerumani [emoji629] sijamuona hata kwa gari moja.


1. Ford F-Series (787,422 units sold)
2. Chevrolet Silverado (586,675 units sold)
3. Ram Pickup (563,676 units sold)
4. Toyota RAV4 (430,387 units sold) [emoji627]
5. Honda CR-V (333,502 units sold)[emoji627]
6. Toyota Camry (294,348 units sold)[emoji627]

7. Chevrolet Equinox (270,994 units sold)
8. Honda Civic (261,225 units sold)[emoji627]
9. GMC Sierra (253,016 units sold)
10. Toyota Tacoma (238,806 units sold)[emoji627]
11. Toyota Corolla (237,178 units sold)
[emoji627]
12. Nissan Rogue (227,935 units sold)[emoji627]

13. Ford Explorer (226,217 units sold)
14. Toyota Highlander (212,276 units sold)[emoji627]
15. Jeep Grand Cherokee (209,786 units sold)
16. Jeep Wrangler (201,311 units sold)
17. Honda Accord (199,458 units sold)[emoji627]
18. Ford Escape (178,496 units sold)
19. Subaru Forester (176,996 units sold)[emoji627]
20. Subaru Outback (153,294 units sold)[emoji627]
21. Mazda CX-5 (146,420 units sold)[emoji627]
22. Nissan Altima (137,988 units sold)[emoji627]

23. Jeep Cherokee (135,855 units sold)
24. Ford Transit (131,556 units sold)
25. Toyota 4Runner (129,052 units sold)[emoji627]

Tuache kumlinganisha Mjapani na vitu vya kijinga, Wabongo wenzangu mpo sawa kabisa TOYOTA ndio ndugu yetu wa damu kabisaaa








View attachment 1696661
Miaka mingi humu Jf nimeshuhudia mijadala yenye kuiponda Toyota na hali hiyo ikapelekea ionekane magari ya Ulaya ndiyo bora.
Kwa mara ya kwanza leo hii Wajerumani wa Jf nashuhudia wakiachwa uchi tena kwa fact za kisomi kabisa. [emoji16][emoji16]
 
Unakutwa wajerumani wanafungana mota 😂😂😂 wakati anaeshauri yeye kipato cha uhakika kuna wale wana kondoo wanaswagwa tu na upepo,,,

"Aisee chief vuta Volvo XC90 iko vizuri sana comfortably achana na Toyota Rav 4 spea zipo!"

Baada ya miezi 4 mtu anadondoka humu na ID mpya,,, "Natafuta fundi ni swap engine ya Volvo niweke ya Rav 4" 😂😂😂 unajiuliza hizi tabu za nini jamani!
Volvo ni mswidi mzeeiya! Halafu Volvo haina hayo makitu.
 
Sasa inakuaje hata huko US ambako kuna matajiri kwny top 15 ya gari zinaouza kwa sana Bmw,Benz,VW ndio za mwisho kwa kuuza gari chache huku Toyota ikiwa ni ya 2 kwa kuuza gari nyingi?

Au wamarekani nao hawana uwezo wa kumiliki hizo Germany machines?
Americans like them big! Mzungu kashindwa kubadilika; mjapani kaweza kucheza na akili za wamarekani kwa kutengeneza Japanese models ambazo ni kubwa kuliko kawaida. European makes sizes ni zile zile kama za kwao Ulaya. Hii ni moja ya sababu
 
Waambie TRA watuache tuyanunue waweke kodi zao kwenye mafuta tu uone jinsi ambavyo vitu vingeshuka hapa hadi barabar ziongezwe upana kupunguza foleni.
Hao hao washamba wanataka kuleta hadi treni zinazotumia barabara ila wanaogopa TRA na kuambiwa ati "Wanaosha pesa" na "Kuzipiga pasi".
Serekali iweke kodi kwenye mafuta uone jinsi watu watashusha vitu hap bongo.
 
Waambie TRA watuache tuyanunue waweke kodi zao kwenye mafuta tu uone jinsi ambavyo vitu vingeshuka hapa hadi barabar ziongezwe upana kupunguza foleni.
Hao hao washamba wanataka kuleta hadi treni zinazotumia barabara ila wanaogopa TRA na kuambiwa ati "Wanaosha pesa" na "Kuzipiga pasi".
Serekali iweke kodi kwenye mafuta uone jinsi watu watashusha vitu hap bongo.
TRA Wana msemo wao wanakuambia gari chakavu zenye zaidi ya miaka 10 Kodi yake ni kubwa kuliko gari mpya.
Sasa wewe jichanganye fatisha maneno yao ununue gari iliyotengenezwa mwaka 2019 utalia na Mungu wako
 
TRA Wana msemo wao wanakuambia gari chakavu zenye zaidi ya miaka 10 Kodi yake ni kubwa kuliko gari mpya.
Sasa wewe jichanganye fatisha maneno yao ununue gari iliyotengenezwa mwaka 2019 utalia na Mungu wako
Hawa ndio wanatunyima kununua mkoko wa kileo. Wanaikosesha serekali yetu kodi sana. Kama magari ni mengi na huwa yanakula mafuta sasa hapo wakiongeza kodi ya mafuta si wangepata zaidi??
 
Hawa ndio wanatunyima kununua mkoko wa kileo. Wanaikosesha serekali yetu kodi sana. Kama magari ni mengi na huwa yanakula mafuta sasa hapo wakiongeza kodi ya mafuta si wangepata zaidi??
Wanachukulia magari ni anasa viongozi wetu wenyewe ni kizazi cha mwaka 1950 ambacho waliambiwa Tv ni anasa ,unadhani watakuelewa kwenye magari?
 
Back
Top Bottom