Carasco Putin
JF-Expert Member
- Apr 23, 2022
- 10,644
- 32,375
Picha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo ni kuingiza kwa maji, imeathiri kiasi gani, fundi atasema baada ya uchunguzi.Nilikuwa nataka kujua hayo maji yanaweza kuwa yameleta madhara gani kwenye gari mpaka ikawa hivo??
Maji yakiingia kwenye control box suluhisho lake ni nini mkuu?Usingewasha hiyo gari ilitakiwa kutoa betri na kuita fundi waangalie wwpi kuna shida. Inawezekana maji yameingia kwenye spark plug na kufanya hiyo missing.
Pia kwenye control box hapo ni shida nyingine.
Ita fundi akufanyie tathmini na kukushauri vyema.
Kuibadili.Maji yakiingia kwenye control box suluhisho lake ni nini mkuu?
Kaka yangu gari yake ikizingua anampigia simu fundi wake anampa maelekezo anamtumia hela (nauli na matengenezo) fundi anaenda kucheck anamalizana nayo kisha maisha yanaendelea.Ahsante mkuu ushauri mzurii huu
Tulia waya nikauke. Sometimes wiya zikiingia maji huwa ni kimbembe.Habari za majukumu wakuu?
Gari yangu aina ya Toyota RAV 4 miss TZ jana ilinasa kwenye dimbwi la maji kwenye kina kirefu kidogo ikabidi mpaka tuite watu yale magari ya breakdown waje waitoe baada ya juhudi zetu kugonga mwamba..
Sasa wakuu kwanza gari baadae ikagoma kuwaka kabisa tukachaji betri ndo ikawaka.. Sasa baada ya hapo ikawa ina mis gia na kupoteza nguvu kabisa na sasa imezima kabisa na haiwaki..
Naombeni msaada wa kitaalam hapa shida itakuwa ni nini maana mimi sina uelewa sana kuhusu magari..
Natanguliza shukrani ndugu zangu
dracular ushauri mwingine huu hapa.Gari ikiingia maji usijaribu kuiwasha unatengeneza matatizo makubwa mtafute fundi wa umeme na Engine uone baada ya kufungua na kufuta futa vitu inakuaje hasa sehemu za plug na fuse box...watumie mashine ile ya upepo kukausha kausha...Rav 4 itawaka haina umeme mwingi ila mafundi wahusike msilazimishe kuwasha wakati gari halijachekiwa vizuri...
Maji yakiingia kwenye fuse inachukua mda. Inachukua hadi siku tatu kukauka. Vuta Subira.Tumeitoa tangu jana saa 5 mchana itakuwa mpaka saivi haijakauka tu?
Siku nyingine ukiwa na Gari lako ukafika sehemu kuna Maji usiingize Gari subiri chambo mmoja apite upime kina cha Maji ndio uingize Gari lako ukiona kina ni kirefu usiingize Gari kwenye Maji rudi ulipotoka nenda kapaki Gari lako panda Mwendokasi subiri Maji yapungueNilikuwa nataka kujua hayo maji yanaweza kuwa yameleta madhara gani kwenye gari mpaka ikawa hivo??
RAV 4 miss TZ spear zake huwa zimechangamka. May be laki 3 sina uhakika. Niliwahi kuprogram tu control box walinilamba laki unusu.oooh kumbe na tayota RAV 4 control box inaweza kuwa sh ngap japo kwa makadirio tu mkuu
ahsante sana rafiki anguRAV 4 miss TZ spear zake huwa zimechangamka. May be laki 3 sina uhakika. Niliwahi kuprogram tu control box walinilamba laki unusu.
But all in all ita fundi aangalie gari kwanza mitandaoni huku utakuwa misleaded.
hahaha 😂😂 eti nisubiri chambo mmoja.. ahsante kwa ushauriSiku nyingine ukiwa na Gari lako ukafika sehemu kuna Maji usiingize Gari subiri chambo mmoja apite upime kina cha Maji ndio uingize Gari lako ukiona kina ni kirefu usiingize Gari kwenye Maji rudi ulipotoka nenda kapaki Gari lako panda Mwendokasi subiri Maji yapungue
Ndio wenzio wanachofanya hivyo km kigari chako kipo chini sana subiria chambo aingie hata bodaboda au Bajaj kaa pembeni mwangalie anavyoitia Majini ukiwa pembeni ndio utajua wapi pa kupita SIO unalizamisha tu Gari linapiga vikombe wewe tukuzamishe baharini haujui kuogelea utapona?hahaha 😂😂 eti nisubiri chambo mmoja.. ahsante kwa ushauri