Gari yangu ya kwanza nimenunua, Nissan Dualis

Hapo kwenye namba 6 ndio changamoto. Unajua hizi gereji zetu za uchochoroni tunazotumia kufanya service ndogo wamiliki wake hawapo makini wanafanya kazi kimazoea na ndipo hizi gari huharibiwa sana.

Ipo hivi, unaenda gereji mfano unataka badili oil ya gear box kwa mara ya kwanza. Meneja anamwambia dogo tu "fulani mbadilishie oil mteja" dogo anakwenda dukani anachukua oil ya Total ya Automatic ya Kawaida anakuja anaitia kwenye Dualis, au Toyota Rumion, au Vits new model, au Passo new model, au Vanguard, au kwenye Wish New model, au kwenye Xtrail new model etc gari ambazo hazitumii gear box hydraulic ya kawaida maana zote hizi na nyingine nyingi zinatumia gearbox ya mfumo wa CVT ambao hydraulic yake ni ya tofauti kabisa kimaterial na hata components zake sababu ya utofauti wa functionalities kati ya CVT transmissions na Automatic transmissions za kawaida zenye counter gearbox.

Akiweka mtumiaji tena especially wamiliki wa magari kama wanawake, watu wazima wa umri mkubwa ambao wamezoea magari ya kizamani au mtu yoyote asie mfuatiliaji wa maswala ya magari na hana elimu nayo huwa hata hawana idea nini kianendelea, analipia na kuwasha gari na kuondoka. Mita chache gari inaanza kumiss gear.

Anawaza pengine gari ni bovu, anapeleka kwa fundi anayetumia tu uzoefu ila hana ufahamu wa magari ya kisasa especially ya umeme anaanza pewa sound mara ooooh hizi Nissan ni gari mbovu sana. Ndio maana tunashauri watu kununua Toyota maana ni imara hizi ni mbovu sana.

Matokeo gari itatukanwa na kuchafuliwa jina as if ni kweli kumbe kosa ni la m'miliki na fundi wasiojua wanafanya nini.

So kimsingi ni vema sana kuzielewa hizi gari kabla haujaanza kuzitumia. Mimi nilifuatilia sana hii gari taarifa zake maana watu wanasema ni mbovu mimi kuna dada jirani na maskani kwa washua alikuwa nayo tokea 2009 namba B. Nikikuonyesha hapa picha yake utasema ameeingiza mwaka huu namna inavyowaka na kuonekana bado mpya sababu ya matunzo.

Na ukisikia akiwa ameipaki hapo ikiwa idle mode, hautasikia muungurumo wa kuchukiza yaani inatoa sauti ya chini sana almost ipo kimya yaani silent jambo limalomaanisha engine ipo safi na ipo vizuri. Ni gari nilikuwa nikipita wakati naenda shule au town nakutana na dada ndio anatoka nayo basi naitazama tu kama gari kali sana ambayo sitakuja hata kuipanda.

But recently nilianza tena kuifuatilia this time kwa kuielewa na kupata Factory instructions zake na kuijua. Aiseee nikasema shida nini, wacha nijionee. So nimekuja jua kuwa watu wengi hawajui magari wanaenda kwa mkumbo. Gari nzuri sana hii. Ingekuwa mbaya watu wasingenunua.
 
Aiseee sio yule daktari amefariki mwaka huu nadhani kama sio mwaka jana. Alikuwa kama sio muhimbili hapo upanga basi ni muhimbili ile ya kule njia ya mkoa nimesahau jina.

Sio yule jamaa?!
 

Safi Mkuu.
 
Hizi gari zina handling nzuri sana. Sasa ukiendesha kizembe inajibu kwa namna unaendesha. Ipo flexible na very comfortable kuiendesha. Nimeona hata wadada wengi wanakimbilia huku sasa maana wanaona comfortability na urahisi wa kuitumia.
 
Fundi ngongo ndo atakuharibia hilo gari. Pale litakapowasha check engine ukampelekea akapima na mashine uchwara software ipo outdated akakuambia limeua coil na valves na themostat ni ya kutoa sababu iliwekwa kwa ajili ya nchi zenye barafu.
 
Hizi gari zina handling nzuri sana. Sasa ukiendesha kizembe inajibu kwa namna unaendesha. Ipo flexible na very comfortable kuiendesha. Nimeona hata wadada wengi wanakimbilia huku sasa maana wanaona comfortability na urahisi wa kuitumia.
Mkuu Vitz new model recommend oil, ni ipi ?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23] kisahani ni speedometer wazee wa kulala kwenye kona na 120km/H wanaelewa. Anyway maneno yasiwe mengi kumaliza kisahani ni kutembea hadi mshale wa speedometer ufike mwisho
Kwakweli ata mimi nisingemaliza hicho kisahani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…