Gari zuri kati ya NISSAN X TRAIL na SUBARU FORESTER

Wakuu salaam.

Wako niko kwenye wazo la kutafuta usafiri. Mwanzoni nilikuwa nawaza kuhusu Mitsubishi Outlander, Hata hivyo, watu wengi wamekuwa na ushauri hasi kuhusu gari hilo. Kwa sasa nina mawazo mawili baina ya Nissan X traeil na Subaru Forester XT. Bajeti yangu 25 -30 M, Ni mtu wa kipato cha kati siwezi kushindwa ku-run, bajeti ya 200K ya mafuta kwa mwezi na 250K kwa mwezi za matengenezo.

Ninawasilisha wakuu wangu.
Acha Kufananisha Subaru Forester na vitu vya hovyo
 
Mm ninayo xtrail ya 2010 na sijaona huo usumbufu mnaousema(kuna mdau amekushauri uchukue subaru yenye turbo ila mm nakushauri usichukue maana nimetoka huko ndo nmekuja kupumzika kwenye xtrail)

Nisani sio gari nzuri kama umetoka kwenye IST direct lazma itakuliza tu
 
Hata Mimi sijawahi kusikia matatizo ya outlander sometimes wabongo waongo
Wabongo tulilogwa na toyota. Vijana wa Arusha wakatawala mji wao na subaru kwakuwa service walikuwa wakifanyia Kenya(Namanga mpakani). Baadae watu wengine ndo wakazizoea. Ikaja Xtrail wakadai zina sensor nyingi ila wabishi wakanunua na sasahivi kuna namba namba A na B barabarani. Sasa zimekuja outlander na Mazda CX5, wabongo kama kawaida watakuambia hizo gari hazifai na ukimuuliza una experience ya miaka mingapi na hizo gari hana, atakuambia nimesikia kwa mafundi. Mafundi wetu wa chini ya mwenbe hawayajui magari ya kisasa, wamezoea toyota za miaka ya 80, 90, 2000 na kidogo 2010 na subaru sasa wamezijua jua. Mdau usichukue gari ya turbo kama huna haja na mbio au kuweka ligi barabarani. Turbo bado kwa mafundi wa chini ya mwembe ni kubahatisha
 
Wabongo ni wajuaji Sana kuliko aliyetengeneza gari.
Shida kubwa iliyopo kwetu ni mafundi Tu ndiyo maana wenzetu Kenya wanatamba Sana na nissan
 
Mm ninayo xtrail ya 2010 na sijaona huo usumbufu mnaousema(kuna mdau amekushauri uchukue subaru yenye turbo ila mm nakushauri usichukue maana nimetoka huko ndo nmekuja kupumzika kwenye xtrail)

Nisani sio gari nzuri kama umetoka kwenye IST direct lazma itakuliza tu
Mimi natumia Subaru forester XT (turbo) sijaona tatizo lolote juu ya turbo kwasababu nazingatia masharti yake
) natumia Castrol Oli au Atlantic
2) oil filter ya BOCSH
3) Kia mwisho wa mwezi naenda kupuliza air cleaner kwa compressor
4) kila niwashapo gari nasubir DK 3-5 ndipo naanza safari
5) nikiwa njiani nasubir gari ichanganye yenyewe huku nikiwa nimekanyaga Kwa mbali accelerator ili kuipa nguvu turbo
.......hayo ni baadhi ya masharti ya magari yote ya turbo ........
Kilakitu kinahitaji umakini tu
 
Budget y mafuta km 200k kwa mwezi, ndugu chukua ist…

Au labda Km kazi kwako n mtaa wa nyuma hapo, Maana tukianzia subaru budget ya 400k fuel per month inaweza kuwa ndogo pia…

Note: engine yoyote inayoanzia Cc 2000 and above kwa week tena normal driving ni laki 1 to laki 40. ( 20k per day)
 
Mimi natumia Subaru forester XT (turbo) sijaona tatizo lolote juu ya turbo kwasababu nazingatia masharti yake
) natumia Castrol Oli au Atlantic
2) oil filter ya BOCSH
3) Kia mwisho wa mwezi naenda kupuliza air cleaner kwa compressor
4) kila niwashapo gari nasubir DK 3-5 ndipo naanza safari
5) nikiwa njiani nasubir gari ichanganye yenyewe huku nikiwa nimekanyaga Kwa mbali accelerator ili kuipa nguvu turbo
.......hayo ni baadhi ya masharti ya magari yote ya turbo ........
Kilakitu kinahitaji umakini tu
Masharti km kwa mganga…. Uo ni uoga tuu kuwasha na kuondoka sio mbaya mbaya kuizima ghafla wakati umetoka masafa…

Gari yenye turbo haibembelezwi hivyo uki accerelate inapokea yenyewe.

Au gari yako yakufugwa nn?
 
Wakuu salaam.

Wako niko kwenye wazo la kutafuta usafiri. Mwanzoni nilikuwa nawaza kuhusu Mitsubishi Outlander, Hata hivyo, watu wengi wamekuwa na ushauri hasi kuhusu gari hilo. Kwa sasa nina mawazo mawili baina ya Nissan X traeil na Subaru Forester XT. Bajeti yangu 25 -30 M, Ni mtu wa kipato cha kati siwezi kushindwa ku-run, bajeti ya 200K ya mafuta kwa mwezi na 250K kwa mwezi za matengenezo.

Ninawasilisha wakuu wangu.
Chukua NISSAN WINGROAD watatumia mpaka wajukuu.
 
Natumia Nissan xtrail Hybrid 2019 haina shida yeyote mwaka 2 huu zaidi ya kufanya normal service sijawah kuchange hata spare
 
Back
Top Bottom