Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Tayari yuko bandarini akiziba nafasi ya TICS
Sina uhakika kama tupo salama kama ameweza kuihujumu USA atashindwa third world kama TZ
 
Wewe ni Kafulira bila shaka

Shares of Adani Group firms fell more than 10% in Thursday morning trade with the group losing more than $20bn in market capitalisation. Adani Green Energy, which is the firm at the centre of the allegations, also said it wouldn't proceed with a $600m bond offering.
The conglomerate has been operating under a cloud since 2023, when US short-seller Hindenburg Research published a report accusing it of decades of "brazen" stock manipulation and accounting fraud.

Kwamba US wana vita ya kibiashara na Adani? Acha ujinga

Shares of Adani Group firms fell more than 10% in Thursday morning trade with the group losing more than $20bn in market capitalisation. Adani Green Energy, which is the firm at the centre of the allegations, also said it wouldn't proceed with a $600m bond offering.
The conglomerate has been operating under a cloud since 2023, when US short-seller Hindenburg Research published a report accusing it of decades of "brazen" stock manipulation and accounting fraud.

Kama unakubali kuwa na chuki hata hizo hoja zako hazina mashiko kwani ni sehemu ya chuki uliyonayo.

Uwekezaji wa DPW unawasaidia wafanyabiashara sio madalali wa siasa zetu za midomoni. Adani alipewa magati ayaendeshe pale bandarini baada ya wanasheria na wachumi kujiridhisha juu ya uwezo wake wa utendaji katika sekta ya bandari.
 
Ni wajibu wa kafulila kuhakikisha dhana ya PPP hailetei taifa janga au ajue atakuja wajibishwa. Kina Adani wanachotaka sio kuwekeza uzalishaji mpya. Wao wanawinda vile nchi zimewekeza waje kuvuna kwa kubinafsisha kijanja uwekezaji za umma. Tusikubali unyonyaji wa kizandiki wa wahindi na waarabu. Wao ndio zao hizo kuleta ukoloni Afrika. Wanajua vigogo wanapenda rushwa kwa hivyo wanauza dhana za kilaghai kunyonya na kupora nchi zingine hasa za kiafrika.
 
Kama unakubali kuwa na chuki hata hizo hoja zako hazina mashiko kwani ni sehemu ya chuki uliyonayo.
Ni nani, binaadam asiye na chuki?
Wewe hapo unajiona huna chuki, kwa vile tu unaigiza usiionyeshe bayana huko
Uwekezaji wa DPW unawasaidia wafanyabiashara sio madalali wa siasa zetu za midomoni. Adani alipewa magati ayaendeshe pale bandarini baada ya wanasheria na wachumi kujiridhisha juu ya uwezo wake wa utendaji katika sekta ya bandari.
Haya ni marudio ya yale yale tuliyo kwisha elezana mara nyingi tu. Sina sababu ya kuendelea kurudia tena. ndani ikikuunguza?
 
Tatizo haya tunayoyaandika hayafanani kabisa na ufanisi wa mashirika yetu yanayobinafsishwa. Tufanye uzembe na nchi yetu iwe unaumia kiuchumi halafu wanasiasa wakileta mashirika makubwa yenye uwezo tuanze kuyapiga vita kwa wivu wa hicho wanachokwenda kukivuna?.

Aliyeturoga keshakufa na hatujui kaburi lake lipo wapi.
 
Hawa ni wahongaji tu! hawana kitu ukisikia mkataba na hawa ni rushwa tupu.
 
Tumewahi kubinafsisha mashirika mengi tu toka huko nyuma kwa taasisi kubwa tu kutoka nje, je baada ya kubinafsisha ni shirika gani lilifanya vizuri?
 
Hivi hakuna kitu tunaweza endesha wenyewe kwa ufanisi?
Sera ya uwekezaji ni nzuri lakini tubakishe vingine tujifunzie hivyo. Au tugawe vipande vipande shirika kwenye
Uzalishaji
Usambazaji
Ukusanyaji
Then tuwekeze kipande fulani kwa PPP vingine tubaki navyo
Mashirika haya ni yetu tusiyagawe tu. Naomba kushauri
 
Tumewahi kubinafsisha mashirika mengi tu toka huko nyuma kwa taasisi kubwa tu kutoka nje, je baada ya kubinafsisha ni shirika gani lilifanya vizuri?
Zipo sababu nyingi za kutofanya vizuri kwa mashirika hayo, mbaya kuliko zote ni kuingiza siasa kwenye masuala ya ufanisi yenye kuhitaji utaalam.

Tukubali tukatae tunalo tatizo katika taasisi nyingi haswa katika suala zima la tija kuwa ndogo, ufisadi ni mwingi watu wanavizia fursa za kuchota pesa.

DPW alikuja pale TPA na mbinu tofauti na akaanza kupigwa vita mapema sana kwani wafaidikaji wa mianya ya upigaji ni wengi na wenye misuli minene.
 
Umezunguka tu. Ukweli kwa nchi zetu za dunia ya 3 wala hawana huo mpango wa kuja kukunufaisha, wanakuja kuja kuchukua zaidi kutoka kwako kuliko utachopata kwao hata akae miaka 100 story zitakua vile vile.

Kutoka hapo sio rahisi. Tuendelee tu kujipa moyo ila usitegemee maajabu yoyote. Waarabu, baadhi ya nchi asia na wazungu waliweza. Kwa huku Africa tulishakosea
 
Ina maana hatukufanya due diligence. Halafu mbona kama deals zinazohusisha watu wa aina hii huwa ni deals zenye rushwa?

Imekuwaje ghafla ameaminika hivyo? Haya mambo haya!!! Kuna watu yatawafuata mpaka makaburini. Hawatalala kwa amani hata siku moja.

Nilitegemea partner yoyote anayetaka kuwekeza kwetu, ili apewe fursa ni lazima awe na credibility kwanza. Tunafanya partership na matapeli πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚

US wameamua tujue tunasimama wapi. Inasikitisha mno
 
Inawezekana vipi tapeli akakunufaisha? Terrible. Sijui nani anayeruhusu mambo kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…