Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Mama anatafuta fedha za kuhonga!
 
Mawazo yale yale ya kimaskini, ya kudhani kila mtu anataka kukuibia!, Kujiona wewe tu ndio mwenye utajiri unaoonewa wivu unaotaka kuibiwa na wenye nacho.

Dunia hii ukimletea mwenye teknolojia maringo anaondoka kwako mchana huo huo na kwenda kufanya uwekezaji kwa mwingine.
 
Tusiogope wezi jamanii kuuza mashirika yetu. Watu waadilifu wapo kabisa wapo tena wengi tu. Tatizo letu ni kuchagua rangi ya paka wakati kazi tunayotaka aifanye ni kukamata panya bila ya kujali rangi yake.
Vyuoni tunao wataalam wazuri tu na waadilifu wanaoweza endesha hayo mashirika kwa ufanisi. Tusiogope
Huwezi mwigopa mwizi kwa kugawa shamba lako kwa jirani hiyo sio sawa
Tulikuwa na akina Mchechu walioshika mashirika yaliyojufia na yakafufuka. Watu wa aina hiyo wapo wengi tu
 
Watu washakula hela sasa wanaangalia upepo unavyoenda.
 
Unauzungumza umaskini sehemu ambayo haihusiani. Nimekueleza kama unasubiri mwekezaji aje Africa kukupa zile ndoto tunaota kufika basi hatutafika kwenye hizo ndoto. Mwekezaji ataweza kukupa ndoto iliwa tayari wewe mwenyewe umeanza kuzitimiza

Dunia hii ukimletea mwenye teknolojia maringo anaondoka? Huu ni uongo, Hakuna mtu atataka kuondoka kirahisi sehemu anayopata sawa na bure. Ndio maana unaona hadi leo ExxonMobil, Equinor wanabembeleza serikali isaini haraka mkataba wa gesi Lindi. Fikiria tu kwa miaka 8 sasa tunawapiga chenga lakini bado wanabembeleza. Kwa maneno yako wangekua washaacha kutaka huo mradi
 
Unaushahidi wowote jombaa
All circumstantial evidence points to that.

Hiyu jamaa Adani ndoyo tabia yake kutembeza pesa na viongozi wa Watanzania wanapenda sana pesa.

Sasa unafikiri watampa contract burebure bila kupiga pesa?

Unataka waweke wazi hii hapa rushwa katoa tumeifurahia sana?

Serikali ina wajibu wa kuweka mambo wazi, kwa nini haikuweka?
 
Kafulila hawezi kukubali rushwa ya aina yoyote namfahamu vema tuwe watulivu tu
 
Kafulila hawezi kukubali rushwa ya aina yoyote namfahamu vema tuwe watulivu tu
Angekuwa hawezi kukubali rushwa ya aina yoyote asingetuletea huyu mtu anayenuka rushwa.

Kutuletea huyu mtu na kampuni yake maana yake hakufanya due diligence ya kutosha.

Sasa hakufanya due diligence ya kutosha kwa sababu gani?

Unataka kusema Kafulila ni mjinga hivyo hakujua kwamba huyu mtu na kampuni yake wananuka rushwa?

Haya mambo mbona yameandikwa kirefu miezi mingi tu na whistleblowers wa Kenya.

Kafulila hakujua tuhuma hizi?
 
Kafulila ndio maana Jesca alimwacha kisa hajui kupiga pesa, Kafulila ni mwadilifu sana hata hivyo
 
Kafulila ndio maana Jesca alimwacha kisa hajui kupiga pesa, Kafulila ni mwadilifu sana hata hivyo
Uadilifu wake haukumfanya afanye due diligence ya kutosha kuepukana na watu waliogubikwa na rushwa. Hivyo hautoshi.

Katika sheria kuna msemo kwamba "Justice must not only be done, it must appear to be done".

Mtu muadilifu hatakiwi tu kuwa muadilifu, anatakiwa kuonekana kuwa muadilifu.

Sasa mnasema Kafulila muadilifu, halafu hapo hapo anampigia debe huyu mtu anayejulikana kwa kugawa rushwa popote anapokwenda. Hapo tukiangalia tunahitimisha kuwa Kafulila naye ama kapewa rushwa, ama ni mjinga sana hakujua kuwa huyu mtu ananuka rushwa despite all the press.

Sasa Kafulila ni mjinga sana hivyo kweli?
 
Kwani tuliingia mkataba na yeye au kampuni zake?

USA siwaamini sana linapokuja suala la maslahi yao, wanakuundia zengwe tu.

Tanzania tutazame maslahi ya nchi kwanza kabla ya yote.
 
William Ruto amekwisha vunja kandarasi ya huyu mtoa rushwa kuendesha uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta
Hapa Tz kunanuka uvundo.
Madame FaizaFoxy sijui waziri na Abdul ukwasi wao umetokana hapa au la ila huyu muhindi ni mtoa rushwa mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…