Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Dp world ni mafia zaidi ya huyo lakini amepewa tenda hakuna kitakachobadilika hapo.
Wakenya wamebadili mawazo. Rutto ametangaza kuwa dili ya kumwachia huyo Adnan AirPort yao aiendeshe kwa miaka 30 imesitishwa baada ya hiyo kashfa kule Marekani.

Ikumbukwe huyu tycoon, anatengeneza drones ambazo anawa supply IDF.
 
Kwisha
View attachment 3157928


Imeisha hiyo.

We unafikiri zile milioni mia saba saba anazogawagawa ovyo kwenye mpira na zile milioni mia, mia hamsini anazogawa makanisani/misikitini zote ni pesa za walipa kodi?
 
Hili halina ubishi.
 

Attachments

  • Screenshot_20241121-211712.jpg
    Screenshot_20241121-211712.jpg
    275.6 KB · Views: 3
Usipotoshe.
Kinacho pingwa ni ufisadi. Miradi inayo ingiwa gizani kwa kuficha kila kitu ili madudu yasionekane.
Wewe mwenyewe humu ulisha sema na kumhimiza Samia kila kitu afanye gizani, watu wasijue kinacho endelea!

Sasa mnageuza stori na kulalamikia watu na makundi yanayo pigania maslahi ya wananchi.

Sasa wewe tueleze, ni waTanzania wangapi wanajuwa kwamba gesi ya Mtwara (Ntor) Samia alikwisha wagawia Omani; ni waTanzania wangapi wanajuwa Adani huyo huyo alisha pewa mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe. Huko bandarini, nani anaye juwa ni makubaliano gani huyo Adani aliingia nayo na serikali yetu.
Kila kitu mnafanya gizani, halafu mnawaona waTanzania kama majuha!
Hii nchi kwa Sasa ipo mikononi mwa wahuni
 
Tusiogope wezi jamanii kuuza mashirika yetu. Watu waadilifu wapo kabisa wapo tena wengi tu. Tatizo letu ni kuchagua rangi ya paka wakati kazi tunayotaka aifanye ni kukamata panya bila ya kujali rangi yake.
Vyuoni tunao wataalam wazuri tu na waadilifu wanaoweza endesha hayo mashirika kwa ufanisi. Tusiogope
Huwezi mwigopa mwizi kwa kugawa shamba lako kwa jirani hiyo sio sawa
Tulikuwa na akina Mchechu walioshika mashirika yaliyojufia na yakafufuka. Watu wa aina hiyo wapo wengi tu
Tangu 1961 tunapata uhuru wasomi wetu wanazo akili za wizi tu, ni kwa bahati mbaya sana kila mwaka CAG anapotoa report ya mwaka inajaa uchafu mtupu.

Na hao wanaochafua hiyo report mawazo yao wanapopewa nafasi ya kujenga hoja yanafanana na haya ya kwako hapo juu. Ya kuisikitikia ni nchi yetu.
 
Back
Top Bottom