Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Florens Luoga abadilishwe haraka

Naunga mkono hoja,haiwezekani uchumi wa mabenki ukue huku wakopeshwaji wakinyonywa kwa mariba makubwakubwa,huu ni uwizi kabisa,inawezekana anakula na wakurugenzi wa mabenki wasitoze riba sahihi,nchi hii riba za mikopo yote hazikutakiwa kuzidi 10%,wakopaji wananyonywa sana
 
Huyu ni gavana ma ta ko

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kwa inflationa inayo average 5%, riba 20%, tax 30% na matozo msululu, corruptions kila kona, umeme unreliable and very expensive etc hivi bongo watu wanafanyaje biashara? ndio maana bora mtu aagize mafuta ya kula kutoka nje auze kuliko kufunga kiwanda bongo azalishe, ukiangalia vizuri matatizo mengi ni ya kujitakia tuu na hizo number zisipobadilika umaskini bongo ni forever
 
Unajua mikopo chechefu inagharimu kias gan banks??? Tueleze in figures hasara wanayopata banks kutokana na mikopo chechefu ndipo turud kwenye riba sasa
Hii ni muhimu sana watu kujua sio kuangaliua upande mmoja tuu, na usisahau inflation na mikodi msururu inavyotafuna faida za Bank
 
Gavana wa benki kuu ilibidi akiteuliwa akathibitishwe na bunge au kamati inayohusu uchumi.Katiba mpya.
Bunge lenyewe ni hili la Ndugai sheria zinapitishwa pale pale yamekaa kama mazuzu kugonga gonga meza hovyo kama mandondocha mengine yamesinzia zikija mtaani zikawa na athari wanashangaana tena wenyewe kwamba ilikuwaje mpaka sheria hizo zikapita wakati wao wapo?

U know,hii nchi ilibidi tuachwe tujiongoze wenyewe maana nikipima ufahamu wangu na walionizunguka kisha nikaupima na wengi wa wanaojiita wataalamu serikalini huwa najiona nipo smart kuliko wao kiasi hata wasipokuwepo still tuta-survival tu.
 
Mara ngapi serikali imetoa bei elekezi ya sukari au mafuta ya kula na haikushuka?

Nchi hii hii au mwenzetu umesahau haya?

Anyway, ngoja tuone mamlaka ya uteuzi kama haimwoni Gov. Luoga anakidhi matarajio as per job restriction.
 
K
Nikukumbushe tu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka ya kwamba mtu akiishakuwa CAG HAWEZI TENA kuteuliwa kufanya kazi nyingine ndani ya serikali na taasisi zake. Labda umpendekeze alhaj mwingine!
 
Nafikiri CRDB Chief atakuwa ndie facilitator wa fedha za mikopo kutoka nje kwa ku-bypass BOT.

Tatizo bado lipo tokea March, hivyo "headhunters" bado wapo kazini.

Tujikumbushe wajibu wa benki kuu ya nchi:

1. Kudhibiti mfumuko wa bei na kuweka kiwango riba ambacho hakipandi wala kushuka kiholela.

Hivyo, kila mwezi BOT ina wajibu wa kuweka kiwango cha riba ambavyo ni lazima vifuatwe ili bei ya bidhaa zilipande hadi kufikia wananchi kulalamika.

2. Kuuangalia na kuuchunga mfumo wa fedha au financial system. Hapa kuangalia zile risks za wakopaji kwa mabenki.

3. Kuzisimamia benki mbalimbali, hapa kuhakikisha mabenki hayajiwekei riba watakavyo bila ridhaa ya BOT na kulingana na hali halisi ya uchumi wa nchi.

Kwa kifupi kwa sasa nchi ipo njia panda maana kukopa kumezidi na hatuambiwi dei halisi la ukopaji limefikia kiwango gani na litalipwa kwa muda gani na kwa kiwango kipi.

BOT ieleze umma kwanini riba za mikopo inafikia 24% na nini sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…