Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Florens Luoga abadilishwe haraka

Gavana ni kama CAG au jaji... ukishamteua kumng'oa ni kazi
Hawa watu wanaibukaga tu bila kusoma security of tenure ya aliueteuliwa wanataka kutumia mabavu kama ambavyo ilivyokuwa hapo nyuma wakamtimua Prof. Assad bila kufuata utaratibu.
 
Toka lini mwanasheria ajue kusoma financials eg balance sheet ndo maana mambo yanajiendea tuu hapo bot. Akiona numbers anaona 'duble duble' tuu anasaini dokezo akiwa hajielewi.
Kusoma Balance sheet sio kazi ya gavana wa benki kuu. Yule ni mtawala tu na Sheria ya uteuzi imewataja wanasheria au mhasibu. Unless tuangalie duties zake ambazo zipo kisheria kama inahitaji mhasibu pekee.
 
Duuuh [emoji134][emoji134]
 
Nani kakwambia ni kazi yake? Hujiekewi wewe akijua kusona hizo sheets ni rahisi kutafsiri hali ilivyo hivyo kuja na sera za kiuchumu sahihi anakuwa well informed wakati anafanya maamuzi mana huyu pia ni bodi chair wa bot ana kura ya veto vikaoni sasa asipojua financials na uchumi inakuwaje? Tuna wachumi wengi wabobezi kwa nini wanaachwa? Huyu bot hafit anafit sehemu zingine za sheria mbona zipo wampeleke huko.
Kusoma Balance sheet sio kazi ya gavana wa benki kuu. Yule ni mtawala tu na Sheria ya uteuzi imewataja wanasheria au mhasibu. Unless tuangalie duties zake ambazo zipo kisheria kama inahitaji mhasibu pekee.
 
BOT Kuna wachumi wameajiriwa hapo na ndio wanafanya briefing kwenye Board unless huelewi kwamba BOT ni Corporate body. Tafadhali tusibishane sana elewa unavyoelewa kama hujaelewa.

Gavana anakuwa kama governing person wa management tu, kazi zote za uchambuzi hufanyika kwenye idara husika mzee. That's how corporate world runs.

Na kwenye Board Kuna governing committees ambazo hupitia then humshauri Mwenyekiti wa Board. Hapo Gavana anakuwa ameshapewa briefing na management na huwepo kujibu kama issues zitaibuka na wao hurudi kuandaa majibu kupitia idara husika.

Gavana is just the same as CEO ajue management na lawyers they fit into that position worldwide accepted.
 
Ngojeni dawa iwaingie. Mtapendekeza marafiki zenu hadi kiama. Tanzania ni ya Watanzania wote sio wachache tu wafaidi keki ya Taifa.
 
Hii ni muhimu sana watu kujua sio kuangaliua upande mmoja tuu, na usisahau inflation na mikodi msururu inavyotafuna faida za Bank
Mikopo chechefu inachangiwa na hayo mariba yao makubwa ambayo licha ya yote bado yanatengeneza faida kubwa kupindukia kwa maumivu ya wakopaji.
 
Ehe ndo mana anaandikiwa na kusaini tuu ndio sababu riba kwa wateja juu na mabenki riba chini. Hiyo communication kasaini tuu bila kufanyia kazi prudent economist asingefanya hivyo
 
Ehe ndo mana anaandikiwa na kusaini tuu ndio sababu riba kwa wateja juu na mabenki riba chini. Hiyo communication kasaini tuu bila kufanyia kazi prudent economist asingefanya hivyo
Well, nakuelewa Ila basi hakuna sababu ya kuajiri other prudent economists ambao wanapewa kazi ya kuongoza idara as directors. Basi ili kuondokana na hayo na gharama zote tumuajiri gavana ambaye ni mchumi awe kama mwalimu mkuu au unaonaje?

That being the case itabidi gavana awe anasahihisha kazi za director wa idara si ndio? Hiyo sio management brother I have experience ya miaka zaidi ya 14 sasa kwa management nielewe tu.

Yani gavana apokee wageni, apigiwe na Rais aangalie mishahara kama imelipwa, adeal na bunge, adeal na Treasury na bado ashike balance sheet??? I think huelewi nachoongea mzee. I beg to rest my pen.

Kumbuka gavana ni ofisi sio mtu ana wasaidizi pia including PA ambae lazima ni mchumi au mwanasheria so gavana akiwa mchumi hupewa PA mwanasheria ili amsaidie na akiwa Mwanasheria anapewa mchumi it goes that way mazee na bado Ile ofisi ya gavana Kuna wasaidizi wakiwemo assistant governors wanaitwa majina yao I think Yani ni chain ndefu mazee. Haipo hivyo Kama unavyosema.
 
Toka lini mwanasheria ajue kusoma financials eg balance sheet ndo maana mambo yanajiendea tuu hapo bot. Akiona numbers anaona 'duble duble' tuu anasaini dokezo akiwa hajielewi.

Sio kazi yake hiyo.. CEO wa Toyota amezaliwa ukoo wa Toyota ila hajui hata engine inatengenezwaje na wala balance sheet inatengenezwaje ila ndie bosi wa Toyota dunia nzima. Gavana wa Bot sio kazi yake.. idara husika itazisoma hizo balance sheet na kumwelekeza
 
Huyu ndio yule aliyeshiriki wizi wa fedha kwenye Bureu De Change uliosimamiwa na jeshi ?
 
Now you are coming to my premise, CEO hajui hata business trend yeye pia ana washauri (consultants) ukiacha waajiriwa wa kwenye management ambao nao ni wataalamu.

You don't have to be a professional wa uchumi kuweza kuongoza bank as long unajua banking business au umekulia kwenye any business. You can manage a business as long una utaalamu wa management ya biashara so inategemea ni aina gani una utaalamu nayo hata kama sio mtaalamu that's why wasomi wote na utaalamu wa business administration au management au any other na wengine hawana hata elimu Ila wanakuwa CEO wazuri sana .

Nakupa mfano wa matajiri wa malori na mabasi au mahoteli, unamjua marehemu mzee Mfugale alikuwa owner na CEO wa Peacock Hotels? Yule mzee ni standard seven Ila aliweza kujenga Mali kutoka kwenye umoja wake akaingia kwenye mabasi ya Kwacha na baadae akaondoka akahamia kwenye biashara ya leisure na akafanikiwa sana mpaka kifo chake . Alimuajiri mwanae ambae alikuwa anafanya UN bwana Vitus Mfugale kama mkurugenzi mkuu na akamlipa same amount ya mshahara wa UN Ila ni mwanae na akawatosa wanae wengine but simply hakutaka waingie kwenye biashara yake lakini walibaki kwenye supply na Mambo mengine wakisubiri urithi tu. Alikuwa anatumia utaalamu wa Vitus tena lately sio wakati anachuma hela.

So haihitaji kuwa mtaalamu wa hiyo sekta ili uweze kuongoza uongozi ni kitu kingine otherwise hata Rais angekuwa anasomea Urais
 
Huyu profesa si tu apigwe chini bali tuende mbele zaidi asomewe mashtaka mahakamani ya makosa ya uhujumu uchumi
 
Sasa wewe naona unaongea vitu usivyovijua, Gavana ni mtu wa utawala tu. Na sehemu hiyo kwa taaluma yake, ni anastahili. Hizo kazi unazompa ahusiki nazo kabisa, kama ulikutana na magumu huko kwenye kukopa basi ilaumu serikali na sera zake na si yeye.

Hizo benki kunufaika ingekuwa ni kinyemela, basi hatua kubwa ingeshachukuliwa. Ila kama kumekaliwa kimya basi elewa serikali ina baraka zake huko, pia inanufaika kupitia kodi wanazozitoza kwa taasisi hizo. Kimaana nyingine nao ni wanufaika kwenye mafaidiko hayo. Jambo jingine la kujiongeza ni kuangalia na hizo benki zinatozwa vipi hivi sasa, ndiyo uje kuhitimisha na kusema wananufaika wao. Na si kukandamizwa ukimbilie kutoa uzi ukiishia kulaumu.

Hebu jaribu kutumia akili yako pia, unawezaje kujua hili wewe wa huku chini na wao wasifahamu lolote lile. Umelionea kwenye ramli?
Haiwezekani hii, wana data za kutosha kuliko wewe. Ukiona hivyo ujiongeze tu, usilaumu asiyehusika na kumpendekeza mtu kisa mtazamo wa kisiasa.

B.O.T haijiendeshi kihuni hadi ifikie kujiwekea tu taratibu zake, bali ni kwa sera maalum za serikali. Gavana hawezi kuhusika hapo kwani hapangi yeye hayo mambo, ni kiongozi pekee kulingana na taaluma yake ya sheria ndiyo anafaa kuwa kiongozi. Watu wa uchumi sehemu hizi za uongozi si wazuri sana, labda watu wa waliyobobea kwenye Business administration.
 
Nashangaa sana watu kusifia Uzi huu ambao haukidhi Vigezo vya Uweledi.
Kama tatizo ni Taaluma ya Gavana, tueleze TOFAUTI ya Utendaji wa Ma-Gavana waliomtangulia, waliokuwa Wachumi wabobezi, kuhusu RIBA za Mabenki zilivyobadilika baada ya Mwanasheria Nguli kuwa Gavana.
Hali ya Riba za Mabenki tangu tupate Uhuru zimeendelea kuwa juu.
Kwa nini hivi sasa zinahusishwa na Taaluma ya Gavana?
Au Wachumi wanafikiria kuwa nafasi ya Gavana ni mali yao?
 
Mtoa mada Pooote umepatia, lkn ulipomtaja ASSAD tu ndio umeteleza. Yule Bw.Mropokaji, Mtatata, Asiye siri, Ana Visasi na Vinyongo kibao. Kwa kifupi msiba wa Jiwe umefanya tuuujue Wasifu wa Viongozi wetu wengi akiwemo Assad. Huyu Bw.kazi pekee inamfaa akawe Mwalimu wa Madrassa au akarithi mikoba ya Maaalim Seif kule Zenjiber
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…