Gavana wa Benki KUU Tanzania!

Kumbe ni mwepesi hivi! Unajua MBA siyo academic qualification! Hivyo ana advanced diploma tu! It’s and it was a shame kuwa PST
 
Kumbe ni mwepesi hivi! Unajua MBA siyo academic qualification! Hivyo ana advanced diploma tu! It’s and it was a shame kuwa PST
MBA is an elite professional qualification, na hiyo Advanced Diploma ya Mzumbe ilikuwa equated na BA by then kabla ya Mzumbe kuwa University. Academic Masters degrees can prepare students for PhD study. But remember BOT or Treasury alikokuwa Tutuba siyo teaching institution.

Wacheni choyo Watanzania
 
Kwa taarifa yako hata Bachelors ya Tanzania siyo automatic kutambulika na kila chuo duniani kwa ajili ya kufanya Masters au ajira. Lazima upigwe post graduate diploma ndipo u proceed kwenye Masters yao
 
Mambo ya equivalent ni ya kipuuzi! Degree na diploma wapi na wapi? Bila PhD huyo Gavana ni mwepesi tu. Najua unatetea vilaza wenzako ati equivalent!
 
Tutulie sindano ituingie. Yani tulieni kabisa kiluo ndio kitaijuza Dunia wapi tumepigwa kitu kizito
 
Kwa kweli hamna dogo. Mnampima mtu kwa jinsi anavyoimudu lugha ya King Charles. Mnataka Nyani Ngabu apate stroke!

Amandla...
 
Kwa taarifa yako hata Bachelors ya Tanzania siyo automatic kutambulika na kila chuo duniani kwa ajili ya kufanya Masters au ajira. Lazima upigwe post graduate diploma ndipo u proceed kwenye Masters yao
Dah

We jamaa aisee kukusaidia tu mtu mwenye ‘post graduate diploma’ maana yake amesoma masters na kufaulu modules zake zote sema ajaandika masters thesis.
 
Ni kweli usemayo. Lakini hatupaswi kuweka monetary policy ya nchi mikononi mwa mtu ambae hajabobea katika masuala ya uchumi au sera zinazohusu uchumi. Ubobezi sio lazima uwe wa vyeti lakini experience ni muhimu. Nafasi hii inapaswa kukaliwa na creme de la creme maana ina impact kubwa katika uchumi wa nchi yetu na hali ya maisha ya wote wanaoishi ndani yake. Huyu sio glorified CEO wa CRDB.

Amandla...
 
CV ya Tutuba haitoshi kwa nafasi aliyopewa, ni nafasi nyeti na ndio uti wa mgongo Kwa Tanzania, nafiri Manager au Director ingekuwa nafasi yake sio nafasi ya Benki Kuu Gavana. CV aliyonayo vijana wengi wanayo na wapo mtaani hawana kazi.
 
Mambo ya equivalent ni ya kipuuzi! Degree na diploma wapi na wapi? Bila PhD huyo Gavana ni mwepesi tu. Najua unatetea vilaza wenzako ati equivalent!
Wewe ni nani ukatae equivalent? Mbona Serikali ilitupa same entry level position na mishahara sawa wahitimu wa UDSM na MzumbeI IDM, IFM na Ardhi Institute miaka yote Ile ya 1970s to early 2000s?
 
Kwani huko Hazina alipokuwa Katibu Mkuu alikuwa hahusiki na monetary policy.

Prof Luoga mwenyewe alikuwa PhD wa sheria za Kodi huku akitokea kufundisha sheria na hakujua lolote kuhusu fiscal au monetary policy yaani hata Income Statement hakuijua na ka survive more than 5 years pale, sembuse ya Tutuba mchumi mwenye elimu ya biashara anayetokea Hazina kama KM au Paymaster General?

Acheni wivu vijana
 
Ngoja tuamini kamati ya uteuzi, muda utasema.Inawezekana yote haya yanayoongelewa kabla ya kuteuliwa wahusika walijua, na pia hatuwezi jua wamejipangaje kumsaidia chinichini huko ( Teamwork)....na pia kuna sababu za msingi zilizopelekea akawekwa pale.
Utawala/ uongozi na mamlaka vina mambo mengi sana ( behind the scene).
All in all kama akili yake ipo sharp, na ka-experience alikonako atamudu..ukiachilia mbali ukomavu wa institution yenyewe...Haya mambo haya sio kama daktari wa kupasua moyo kuwa akikosea tu mgonjwa anakufa...nop..
Lile jumba lote limejaa watu ambao lengo kubwa kumsaidia huyo bwana...

Ataweza tu...hamna jipya chini ya jua

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu Luoga hakutosha kwenye hiyo nafasi haimfanyi huyu kutosha.
 
Kwa kweli hamna dogo. Mnampima mtu kwa jinsi anavyoimudu lugha ya King Charles. Mnataka Nyani Ngabu apate stroke!

Amandla...

Tena hapo ktk video clip ya Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB (Group) alikuwa anasoma kile kilichoandikwa na kuonekana anapata wakati mgumu sana.

Wakati wasomi wote wa Tanzania huwa hawana changamoto katika kuandika na kusoma lugha ya kigeni.
 
Nyie mkoje mbona mnashabikia uongo na kuuipigia misumari.Alewa tofauti ya diploma na advanced diploma.Hii advanced diploma ni equivalent na degree.Na ndio maana mwenye hiyo akitoka hapo anaenda kusoma masters moja kwa moja.Yaani mtu anapindisha hoja makusudi na kuishadadia tu kwa lengo la kuleta nguvu hasi/ kumpaka matope mtu.
 
Katibu Mkuu Hazina haandai monetary policy za nchi. Yeye jukumu lake sio kupambana na inflation na pressure nyingine katika currency yetu. Mwenye jukumu hilo ni Gavana na anapaswa kutimiza jukumu hilo bila kujali serikali inapendelea nini. Ndio maana anatakiwa mtu astute, anaejiamini na ambae yuko tayari kusema ukweli wake kwa mamlaka ya juu.

Wapi nimemsifia Luoga? Ulivyosema kuwa ame survive ni ushahidi tosha kuwa ile haikuwa nafasi. Hatutaki mtu ambae ambition yake ni ku survive. Tunataka mtu ambae atakuwa tayari kupoteza ajira yake pale anapoona ushauri wake hauthaminiwi kiasi cha kuipeleka nchi kubaya.

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…