Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba akiwa anazungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Florian Kaijage amekiri kuwa deni la taifa hilo linazidi kukua ila bado lipo chini ya ukomo wa uwiano wa deni la taifa na pato la taifa unaokubalika kimataifa wa asilimia 55%.

‘’Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’

‘’Deni letu ni himilifu kwa muda mfupi wa kati na mrefu na lipo ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa.’’


Your browser is not able to display this video.
 
 

Attachments

  • Screenshot_20250216-182754_1.jpg
    363.2 KB · Views: 1
Mambo ya ajabu kweli
 
ni jambo la kawaida sana kwa mataifa kukopa na kua na madeni,

nadhan jambo la maana na muhimu zaidi ni kwamba, miradi ya maendeleo inafanyika kwa uwazi na inaonekana bayana ikinufaisha na kubadili hali za maisha ya waTanzania na kua bora zaidi.

Kama Taifa tutaendelea kukopa ili kufadhili maendeleo kwa maslahi mapana ya wananchi na waTanzania wote, kwasabb deni ni himilivu na stahimilivu na bado mahitaji ya maendeleo ya wananchi ni makubwa 🐒
 
ASANTEEEEEEEEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…