Gaza ni mzigo uliojitwisha Israel na haiwezi kuutua, kilichobaki ni kuhangaika nao

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Ipo mikasa mingi ya wezi ambao baada ya kuiba hujikuta wametegeshewa na hawawezi kuutua tena mzigo wao mpaka makubaliano na mwenye mali yafanyike.

Iko mikasa mingine ya wazinifu na wachawi inayofanana na mikasa ya wizi. Gaza ni mfano wa mzigo Israel iliyojitwisha ikitaraji kuufikisha ilipotaka mapema na baadae wapumzike.

Hali imekuwa tofauti na mara Israel imejikuta imebeba mzigo wa tego ambao sasa wanatamani wautue na hawawezi kufanya hivyo. Wameporomosha majengo karibu robo tatu ya jiji la Gaza na hakuna kilichopatikana.

Baadae wakaanza kubomoa mahospitali yote makubwa na kupiga wagonjwa na bado hakuna tija yoyote iliyopatikana. Baada ya kushindwa kuutua mzigo upande wa Gaza kaskazini wakaelekea kusini ya Gaza wamefanya kama walivyofanya kaskazini na haikuwezekana kuutua mzigo wao wa Gaza.

Vizuizi walivyoweka Israel kuzuia watu wa maeneo tofauti wasitoke na kurudi wanakotaka navyo wameshindwa kuvilinda.

Israel ililpojaribu kuhamisha vikosi kurudisha nyumbani ili kuutua mzigo wa Gaza haikusaidia kabisa na ndipo mzigo ulipozidi kuielemea kwa kuongezeka mapigano.

Hatimae Israel ili kuutua mzigo wake wa tego inajaribu kufikia makubaliano ili kumaliza vita na kubaki huru wapate kupumua.
 
Hii imenikumbusha Kuna mwaka jamaa aliiba mkungu wa ndizi eseee tulimuonea huruma yaani ilikua kuranda nao tuu katka viunga vya kijiji. Daah waislaeli ndio kama mwamba Sasa...
 
Ngoja waje wale wayahudi weusi wa Ifakara na Nzega uone jinsi watakavyo ichambua hii mada,wao hua wanajua zaidi kumshinda hata Natanyahu na wayahudi wenyewe wa Tel Aviv.
 
Endelea kujifariji, kusema ukweli mayahudi ndio dawa ya magaidi wa kidini hadi ala na mtume wake mudi waliomba msaada kwa Mungu.
 
Hii imenikumbusha Kuna mwaka jamaa aliiba mkungu wa ndizi eseee tulimuonea huruma yaani ilikua kuranda nao tuu katka viunga vya kijiji. Daah waislaeli ndio kama mwamba Sasa...
Mimi sipendi kuangalia sinema.Lakini sinema moja ya Kidali na TV ya wizi niliipenda kidogo.Jamaa kaibeba vizuri kufika kwa mteja haitaki kushuka.
 
Hili Limekuwa Mzigo Maana Hata Hayo Usuluhisho Ni Mgumu Kupatikana Hadi Sasa Wote Wamepoteza Na Gaza Ndio Wamepoteza Zaidi.
 
Kuwepo Watu ktk familia na ukoo ni sehemu ya furaha wa mwanadamu ikatokea vita kama hiyo ya gaza 60% ya watu hao kufa wanaobaki hawawezi ona thamani ya maisha,watakachokiona ni heli nao waondoke wakaungane nao waliotangulia tusitegee vita vya ardhi kuisha ktk Israel na kitakachotokea ni Israel kurudi nyuma watapike ardhi waliyoila,wasifikiri watashinda ila muda ni mwalimu
 
Waliomba msaada kwa Mungu yupi? unajua kua Yesu aliuawa na kina nani kwa mujibu wa imani yako?
Judaism ina muamini Mungu yupi? na wewe una muamini Mungu yupi?

Yahwe ndio mungu wa wayahudi,mimi naabudu mizimu,yesu aliuliwa kwa sheria ya warumi kupitia ushahidi feki wa wayahudi.
 
Mungu ndio wa kuombwa msaada wakati wa shida na daima hakuangushi.
Wapalestina wameomba wenyewe na wamesaidiwa kuomba..Yahudi hawezi kushinda

Yahudi kashinda na anazidi kushinda ndio mana wanaopiga yowe ni wapalestina.
 
Tatizo lako unajadili hii mada kwa ushabiki kama vile una jadili muziki wa singeli,

Kushinda vita ni kutimiza malengo yaliyokufanya uende vitani,lengo la Israel ni kuifuta Hamas na kuwaokoa mateka,je wametimiza hayo malengo? Wewe unayesema Yahudi kashinda vita hebu tuambie kashindaje hiyo vita? Kumbuka vita sio kubomoa majengo au kuua watoto na wanawake.
 
Attachments

  • Screenshot_20240128-172023_Gallery.jpg
    Screenshot_20240128-172023_Gallery.jpg
    79.5 KB · Views: 3
Ipo mikasa mingi ya wezi ambao baada ya kuiba hujikuta wametegeshewa na hawawezi kuutua tena mzigo wao mpaka makubaliano na mwenye mali yafanyike.

Iko mikasa mingine ya wazinifu na wachawi inayofanana na mikasa ya wizi. Gaza ni mfano wa mzigo Israel iliyojitwisha ikitaraji kuufikisha ilipotaka mapema na baadae wapumzike.

Hali imekuwa tofauti na mara Israel imejikuta imebeba mzigo wa tego ambao sasa wanatamani wautue na hawawezi kufanya hivyo. Wameporomosha majengo karibu robo tatu ya jiji la Gaza na hakuna kilichopatikana.

Baadae wakaanza kubomoa mahospitali yote makubwa na kupiga wagonjwa na bado hakuna tija yoyote iliyopatikana. Baada ya kushindwa kuutua mzigo upande wa Gaza kaskazini wakaelekea kusini ya Gaza wamefanya kama walivyofanya kaskazini na haikuwezekana kuutua mzigo wao wa Gaza.

Vizuizi walivyoweka Israel kuzuia watu wa maeneo tofauti wasitoke na kurudi wanakotaka navyo wameshindwa kuvilinda.

Israel ililpojaribu kuhamisha vikosi kurudisha nyumbani ili kuutua mzigo wa Gaza haikusaidia kabisa na ndipo mzigo ulipozidi kuielemea kwa kuongezeka mapigano.

Hatimae Israel ili kuutua mzigo wake wa tego inajaribu kufikia makubaliano ili kumaliza vita na kubaki huru wapate kupumua.
Kila mtu atabeba msalaba wake [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG_20231105_185104.jpg

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lako unajadili hii mada kwa ushabiki kama vile una jadili muziki wa singeli,

Kushinda vita ni kutimiza malengo yaliyokufanya uende vitani,lengo la Israel ni kuifuta Hamas na kuwaokoa mateka,je wametimiza hayo malengo? Wewe unayesema Yahudi kashinda vita hebu tuambie kashindaje hiyo vita? Kumbuka vita sio kubomoa majengo au kuua watoto na wanawake.
Ubaya ni kuwa Israel iliyataja malengo yake na wakasema hakuna wa kuwazuia kuyatimiza.
Wangepigana bila kutaja malengo wangekuwa wajanja zaidi,Kwa sasa ni kufedheheka mbele ya washirika wake.
 
Back
Top Bottom