Gazeti la Jamhuri: Siri ya ugomvi wa Dk. Kigwangalla na Profesa Mkenda hadharani

Ile wizara ni ngumu mno! Imejaa titan fitna! Ni muhimu kuwa makini na tuhuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakubwa walio katika serikali wataamua nani mkweli kati ya muandishi wa story hii, katibu Mkuu Prof. Mkenda na Waziri Kigwangala.

Sidhani kama kuna makosa kutumia hela kufanya promotion ya Utalii. Suala je taratibu zimefuatwa, kama hzijafuatwa nani anahusika kumdhibiti anaechukua hela kama kweli kachukua ili afanya kwa mujibu wa utaratibu.

Kubwa kuliko vyote, kwa hayo ambayo Waziri Kigwangala kafanya, je yanaweza kuwa na return on investment. Kama dude au Stive Nyerere wakuwa kwenye media platform za utalii, watavutia Watanzania wangapi kutalii??

Au kwanini Waziri asinge-focus kama Kagame walau akapata mkataba na moja ya timu EPL tukawa na campaign visit Kilimanjaro au Visit Serengeti ili kuvutia wanadunia wanaofuatilia EPL waje Tz.

Kagame project yake na Arsenal ya visit Rwanda in positive projection kwenye return on investment. Assuming waziri katumia hela kwa kufuata utaratibu, uwepo wa akina Ebitoke na wakina wanaFA kwa gharama za TANAPA zina-project vip Return on that investment??

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
Hili linafahamika kama wanagombania fedha zetu za umma.

Kigwangalah anajaribu kupromote Utalii kupitia wasanii. Anastahili pongezi lakini haya inabidi yafuate utaratibu wa fedha na iwepo kwenye mipango ya wizara sio zimamoto pap paaap.

Hapo atamponza hata Katibu mkuu kwa magu.

Binafsi sizani kama kina Le mutuz, shilole watatushawishi watu kama sisi kwenda kutalii wakati hakuna Salary increment, small bizness zinakufa watu hatuna ongezeko la kipato huwezi kupata hela ya kutalii.

Kwa hiyo wale wadada wa mjini wote walioenda kutalii walilipiwa na kodi zetu hii ni hatari zaidi ya umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya matumizi yanayofanywa na mleta hoja yana tija kwenye kuutangaza utalii; hata Coca Cola pamoja na kujulikana na kila mtu hawajawahi kuacha matangazo. Shida ninayoiona hapa hilo ni jukumu la Tanzania Tourist Board na siyo shughuli inayohitaji kusimamiwa na waziri moja kwa moja. Waziri angeelekeza hizo taasisi zipeleke michango hiyo TTB ili kuimarisha juhudi za kuvitangaza vivutio vyetu
 
Alikataa kupokea simu habari imetoka anasema amechafuliwa anataka milini 500, Kigwangala mjanja sana ameona sasa ulaji unakata wizarani anataka apate jamuhuri, jamaa anafanya kazi kishamba sana.
 
Napendekeza tufanye kama Rwanda tuandike "Kilimanjaro" kwenye jezi za Barcelona.
Itatugharimu pesa lakini outcome yake itakua kubwa sana.
Tutafute na timu ndogo za Hispania na Uingereza ila tupromote utalii wa mbuga zetu na vivutio vingine.
Utalii wa ndani tuwaachie Safari Chanel.
 
By the way usipokubali kuliwa huli.....biashara ua utalii inahitaji utumie fedha kuitangaza utalii hivyo hizi pesa kama zinatumika kutangaza utalii shida ipo wapi

Asubiri baada ya miaka 5 asipoona matokeo chanya alalamike kwangu me naona sasa hivi kumekuwepo na mwamko mkubwa sana kwa utalii wa ndani hivyo si mbaya


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa namna tunavyokwenda kipindi hiki sidhani kama yanayoandikwa kwenye bajeti zetu ndio yanayofuatwa,naona kila mmoja anajikurupukia tu kufanya mambo. Twendeni tu hivyo hivyo si ndio tulivyoamua tutafika tu yakiharibika tutarekebisha mbele ya safari.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kutoa habari hii kiungwana na kitaaluma ya uandishi wa habari makini na wenye weledi walitakiwa wahakikishe wamempata Kigwangala kwanza ilk kubalansi stori.
Kinachoonekana ni mkakati wa Balile na Adolf Mkenda kummaliza Kigwangala kisiasa,
Huyu Balile pia alitumika na kina Nape Nnauye kummaliza Makonda alichemka.

Naona anarudia yaleyale aliofanya kea Makonda.
,Ninavyofahamu Kigwangalah ni kijana mtiifu wa rais Magufuli,na anafanya kazi zake kwa nidhamu ya hali ya juu.

Angalizo,
Kuhusu Adolf Mkenda Rais Magufuli siku anamuapisha kuwa katibu mkuu wa hiyo wizara alimwambia nakupeleka huko nako ukafanye yako,ukivurunda ndio basi tena.

Ngoja tuone nani ataibuka kidedea,Uzuri wa vyanzo vya taarifa vya Rais Magufuli huwa makini sana.
Mwisho ,
Balile toka usifiwe na rais Magufuli kipindi kile kwenye sakata la mafuta kuhusu kodi ulivimba kichwa ,muda mwingine unaitumia kalamu yako vibaya.

Na mwisho kabisa si kwa umuhimu, wasanii ni muhimu sana kuwa nao karibu kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, si kwa Kigwangalah tu ,hata Rais Magufuli anawahitaji sana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vema mtu unapozungumza jambo uwe una uhakika nalo,Jamhuri imetoa tuhuma kama izo,Wazir yupo na Katibu yupo wasijifiche wajibu hoja!

Unapoanza kumtetea mtu kwamba lengo ni kumchafua,aende Mahakamani.

Na umesema Balile ametumika kumchafua Makonda hebu weka wazi hapa tujadili kama hizo tuhuma ni za uongo?na Makonda alishaenda mahakamani kuhusiana na tuhuma hizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wazi kwamba vijana bado hatuko tayari kupewa uongozi wa juu katika nchi. Vijana wote wakipewa nafasi wanafanya vibaya. Huyu nae anaingia kwenye list ya viongozi vijana wasio na vision wala charisma kama nilivyoeleza hapa chini

 
Umri ni kigezo muhim sana kuwa katika nafasi kubwa za maamuzi.

Vijana bado wanahitajo kuwa monitored,mihemuko bado ipo juu ya kuwa na utajiri na tamaa za madaraka makubwa. Hivyo wapo tayr kwa gharama yoyote kuona wanafikia hayo malengo.

Mojawapo ni hii ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nakubaliana na wewe. Katiba inabidi iseme

ilikugombea urais lazima uwe na miaka 50
Ili kuwa waziri, naibu waziri au mkuuwa mkoa lazima uwe na miaka 45
 
Yule ni kiwanda cha pombe aina ya Spirit inaitwaga .....shim nani na maji ya habari unajua ushuru wa spirit upo juu sana? Pia biashara ya pombe inalipa sana? Kitimoto ndio the best Baddest Animal?
Ok ila JAMHURI mie nawaomba mfuatilie na lile sakata la mfanyabiashara wa Shinyanga aliyewaachisha kazi RPC na Meneja wa TRA mkoa huo!

Hiyo kesi ilianza upya? Jamaa ni nani? etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah...! Siasa zina pesa jamani asikuambie mtu. Sasa hizi hela zote zinatolewa bila mpangilio milioni 170,hapa zinatumika milioni 20,150 mfukoni mwa wajanja ,mara 100,zinatumika 10,90 mfukoni,mara 200,zinatumika 20,180 kwa wajanja. Jamani,jamani hii nchi ni bure kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…