Gazeti la Kizayuni: Kiyama kitaishukia Israel kama Iran na Hizbullah zitashambulia kwa pamoja

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Gazeti moja la Kizayuni limetangaza kuwa, kiyama kitaishukia Israel iwapo Iran na Hizbullah zitaamua kufanya mashambulio ya pamoja dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronot limetangaza habari hiyo katika toleo lake jipya kabisa na kusisitiza kuwa, utabiri wa mashirika ya kijasusi unaonesha kuwa Iran na Hizbullah bado zina nia thabiti ya kujibu mashambulizi ya Israel.

1723116642593.jpeg

Limeongeza kuwa, kuna uwezekano Iran ikatumia mamia ya makombora kuipiga Israel na kusisitiza kwamba, kwa mujibu wa utabiri wa mashirika ya kijasusi ya Israel, Hizbullah ndiyo itakayoanza kushambulia.

Gazeti hilo la Kizayuni limesema kuwa, huenda Hizbullah ikafanya mashambulizi ya majaribio kusini mwa Haifa na kuna uwezekano mashambulizi hayo ya Hizbullah yakaendelea kwa saa na siku nyingi.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronot pia limeandika kuwa, shambulio la mara hii la kulipiza kisasi la Hizbullah, litakuwa kubwa zaidi dhidi ya utawala wa Kizayuni tangu baada ya kumalizika vita vya mwaka 2006.

Gazeti hilo la utawala wa Kizayuni limeongeza kuwa, Marekani hivi sasa inaendelea kuzungumza na nchi waitifaki kukabiliana na shambulio la Iran na Washington ina woga mkubwa kuhusu shambulio hilo hasa kutokana na shambulizi lililopita la Iran dhidi ya Israel.

Limeongeza kuwa, Wamarekani wanaamini kwamba Iran itaitumia vizuri sana Hizbullah na waitifaki wake wengine kuhakikisha mashambulizi yake yanapenya kwenye anga ya utawala wa Kizayuni na kupiga shabaha zilizokusudiwa.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, mateso wanayopata Wazayuni kwa kutojua lini kambi ya Muqawama itatoa majibu, ni mateso makubwa zaidi kuliko hata kushambuliwa.
 
View attachment 3064568

Msije pia mkaleta kiyama dhidi ya lebanon muangalie upande wa pili baada ya israel kushambuliwa na yeye akijibu mapigo je maana uwezo anao pia
 
Mmeuliwa rais wenu
Ameuliwa kiongozi Wa magaidi
Bado sijui mnangoja nini kuipiga Jerusalem...
Mosad can never let u alive

Mambo mzayuni wa hapo buza, naona upo Kwa mtogole unasoma gazeti la kizayuni
Au Leo umekwenda Yombo vituka??
 
Wewe Maralia 2 ni hizborah????

Ndo maana mi najipendeaga vita za zamani. Wapiganaji wanalengana wenyewe kwa wenyewe. Si hawa wa sasa,hasira wanamalizia kwa raia wasio na hatia.
Mnachotakiwa kuzingatia pia,kuna mtu anamuinda mmarekani,na hawezi kumkuta kwake. Huenda nae hii ikawa fursa. Na ikumbukwe nae ni hatari
 
Back
Top Bottom