Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Ni wakati sasa muanze kupambana kama ANC na Nelson Mandela. Anzeni kuzikaidi hizi amri za kijinga na kikaburu. Kaburu utamshinda kama tu utakaidi amri zake.
 
Baba jesca anawaonea haya jk na bm anataka kudl na tudagaa km alkua haiwez vta her angekaa kmya kulko kuanza kubagua nan umchukulie hatua nan umuache japo alshlk, unakotupeleka sio dereva wa lorry tushakuchoka
 
Kwani yeye Mwakyembe ana uhakika gani kama Mkapa na Kikwete hawajahusika na jambo hili la kuibiwa kwa madini yetu?
Kamanda akisema mguu upande, mguu upende. Mguu sawa, mguu sawa. Hapa sio la Mwakyembe, mimi, wewe, Mawio au mwingine yeyote kujua kama wastaafu hawa wanahusika au la. Kama ulipitwa na matukio, hili ni agizo alilolitoa mwenye mamlaka ya mwisho ktk nchi hii, Amiri Jeshi mkuu ambae si mwengine bali ni Rais Magufuli siku alipokutana na M'kiti wa Barrick. Kwa hiyo Mwakyembe hapa kazi yake ni kuitekeleza agizo la Mkuu tena kwa spidi kali. Au unataka yamkute yaliyowakuta wale askari wa Bunge? Kwa ufafanuzi wa Rais ni kuwa yeye amekubaliana na kutoka amri kwa vyombo vyake husika vya dola kutekeleza mapendekezo yote kama yalivyopendekezwa na tume. Tusiongeze nukta wala kupunguza nukta. Mimi sijaipitia hiyo ripoti, lakini kutokana na rais ni kwamba maraisi wote wastaafu na mawaziri wote wastaafu hawakuhusishwa na tume zake. Labda mimi kwa ushauri wangu ni kwamba yeyote mwenye utafiti/ hoja au vielelezo vyovyote vinavyowahusisha wakuu hawa katika kashfa hii, wampelekee bwana mkubwa kwa uamuzi wake. Kinyume cha hapo unajipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa mamba.
 
Hakuna uchochezi hapo, kwani Mkapa na Kikwete ndio miungu wetu? Sakata linawahusu hawana kuepuka, msema kweli mpemzi wa Mungu atageuka kuwa shetani mkubwa muda si mrefu akiendelea kuwatetea, mbona Lissu anasakamwa kwa kusema ukweli, kwani yeye sio mtu?
 
Serikali mbona haijamchulia hatua chenge...ambaye alisema yeye si mjinga kwenda kusign...basi wengine wasihukumiwe maana wakisema walitumwa na raisi itakuwa kazi bure
 
Ni wakati sasa muanze kupambana kama ANC na Nelson Mandela. Anzeni kuzikaidi hizi amri za kijinga na kikaburu. Kaburu utamshinda kama tu utakaidi amri zake.
Unawahimiza wenzio huku wewe umejificha?
 
Anataka kuwaficha kwenye vichaka vya njugu, Chenge ameishasema ukweli, haiwezekani wapumzike kwa amani wakati wamelisababishia taifa hasara kubwa sana.
 
Watafungua gazeti jipya kumekucha na Zengwe newspaper.. Maisha hayawezi kusimama.

Zile sheria za nape za kumfungia mhariri peke yake ndio Mwakyembe kazitupa? Sasa hao wafanyakazi awachukue na kuwalisha
 
Lakin mkapa na kikwete walifanya kweli chanzo cha yote haya ni wao iweje wasitajwe waache wapumxike kwa kazi gani ngumu waliyofanya ya kukumbukwa zaidi ya hii inayofanya watu wadharauliane wafungiane magazeti !
 
Kazi tukufu awamu hii inayotekeleza kwa weledi wa kutisha ni kuharibu mali za wapinzani wao wa kisiasa rejea Bilicana na hivi karibuni shamba huko Machame,na zaidi sana kuwabambikia washindani wao kesi za uchochezi.
 
Kama kweli Waheshimiwa Mkapa na Kikwete hawahusiki kwa moja kwa moja katika sakata hili la madini, Basi wahusishwe japo kwa uzembe (Negligence) iliyopelekea nchi kuingia katika mikataba yenye utata na hasara kubwa kwa nchi wakati wakiwa waajiriwa namba 1 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…