Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Kama kweli Waheshimiwa Mkapa na Kikwete hawahusiki kwa moja kwa moja katika sakata hili la madini, Basi wahusishwe japo kwa uzembe (Negligence) iliyopelekea nchi kuingia katika mikataba yenye utata na hasara kubwa kwa nchi wakati wakiwa waajiriwa namba 1 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Raisi si mwanasheria na si mtaalam wa sheria na kazi ya mikataba ni kwa ajili ya wanasheria na rais anategemea sana utaalam wa watu hao kulingana na viapo vyao
 
Mkulu kuwapa kinga maraisi wastaafu, amejipa kinga yeye mwenyewe na watendaji woote serikalini waliohusika na mikataba isionufaisha Taifa. Hakuna kitu watendaji ( mawaziri, wanasheria wakuu nk) walifanya pasipo ufahamu wa hao marais wastaafu!
.
 
ndivyo zilivyo nchi zetu za ulimwengu wa tatu hii pia ni moja ya setback ya maendeleo
 
Sheria sio dhaifu hili gazeti pendwa kwa wapenda mabadiliko litapata kash kash Sana hayo nimatakwa ya sharia ila yakiwa na shinikizo flani kutoka Mahala, anyway ktk vita ya kiuchumi huwa haiwaachi watu salama
 
Raisi si mwanasheria na si mtaalam wa sheria na kazi ya mikataba ni kwa ajili ya wanasheria na rais anategemea sana utaalam wa watu hao kulingana na viapo vyao
Je,wa sasa anayoyasema,kuagiza n.a. kutenda watakuja kulaumiwa washauri wake kisheria? Maana ni "haambiliki" n.a. anajua Katiba inampa jeuri hiyo.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Nilitegemea serikali kupitia wizara ya katiba na sheria ianze namna ya kubadirisha sheria kwa kufuta kinga ya rais wastaafu,waanze kushtakiwa (if we are very serious kupambana na ufisadi). Uhitaji kuwa na phd kujua uhusika wa JK na Mkapa katika saga la madini,kwa wanao ona mbali,waliotajwa katika ripoti 'are free' hata kabla ya hukumu.
 
FB_IMG_1497624090830.jpeg

Hili nalo vp?
 
Halafu wenye mtindio wa ubongo wanatuhimiza tushikamane na rais eti anachukua hatua za kizalendo kulejesha Rasilimali zetu,sasa kama hataki hata tuwataje viongozi waliokuwepo madarakani wakati mikataba hii ya kinyonyaji inasainiwa kile kinachoitwa uzalendo kiko wapi?

= kurejesha

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Sizonje aliwahi kusema hatafukua makaburi. Lakini kila uchwao anayafukua. Ufukuaji huo unawahusu moja kwa moja namba 2, 3 na 4.
Unapofukua Makinikia na Escrow, unakuwa umewataja hao 2,3&4. Unaposimama na kuzuia wasitajwe unakuwa unajipinga mwenyewe.

Sizonje amua moja, ondoa Kinga tuwashtaki haki itendeke.
 
wenye Akili ndo tunakuelewa wale kijani wao kuandamana na kupongeza tu
 
Back
Top Bottom