Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Raisi si mwanasheria na si mtaalam wa sheria na kazi ya mikataba ni kwa ajili ya wanasheria na rais anategemea sana utaalam wa watu hao kulingana na viapo vyao
 
Mkulu kuwapa kinga maraisi wastaafu, amejipa kinga yeye mwenyewe na watendaji woote serikalini waliohusika na mikataba isionufaisha Taifa. Hakuna kitu watendaji ( mawaziri, wanasheria wakuu nk) walifanya pasipo ufahamu wa hao marais wastaafu!
.
 
ndivyo zilivyo nchi zetu za ulimwengu wa tatu hii pia ni moja ya setback ya maendeleo
 
Sheria sio dhaifu hili gazeti pendwa kwa wapenda mabadiliko litapata kash kash Sana hayo nimatakwa ya sharia ila yakiwa na shinikizo flani kutoka Mahala, anyway ktk vita ya kiuchumi huwa haiwaachi watu salama
 
yeah! maamuzi ya serikali yapo sawa kabisa.
 
Raisi si mwanasheria na si mtaalam wa sheria na kazi ya mikataba ni kwa ajili ya wanasheria na rais anategemea sana utaalam wa watu hao kulingana na viapo vyao
Je,wa sasa anayoyasema,kuagiza n.a. kutenda watakuja kulaumiwa washauri wake kisheria? Maana ni "haambiliki" n.a. anajua Katiba inampa jeuri hiyo.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Nilitegemea serikali kupitia wizara ya katiba na sheria ianze namna ya kubadirisha sheria kwa kufuta kinga ya rais wastaafu,waanze kushtakiwa (if we are very serious kupambana na ufisadi). Uhitaji kuwa na phd kujua uhusika wa JK na Mkapa katika saga la madini,kwa wanao ona mbali,waliotajwa katika ripoti 'are free' hata kabla ya hukumu.
 

= kurejesha

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Sizonje aliwahi kusema hatafukua makaburi. Lakini kila uchwao anayafukua. Ufukuaji huo unawahusu moja kwa moja namba 2, 3 na 4.
Unapofukua Makinikia na Escrow, unakuwa umewataja hao 2,3&4. Unaposimama na kuzuia wasitajwe unakuwa unajipinga mwenyewe.

Sizonje amua moja, ondoa Kinga tuwashtaki haki itendeke.
 
wenye Akili ndo tunakuelewa wale kijani wao kuandamana na kupongeza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…