Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Mwakyembe anawatafutia matatizo wanasheria wa serikali ......... maana watatakiwa kuileta ile mikataba ili ionekane nani alisaini. Wamesahau Mkapa aliitwa kutoa ushahidi kesi ya Mahalu!!

Hii kesi inaweza kuexpose badala ya kuficha ukweli!!

Labda wailelekeze Mahakama itupilie mbali hiyo kesi bila kuisikiliza!!
Point,

ngojea waende mahakamani.
Pia ni aibu kwa serikali hii kwa kuwalinda waharifu wa uchumi kwa kuangalia kinga ya wastafu (marais), hii inaonesha haya yanayofanywa na rais ni maigizo kwani wahusika wanajulikana lakini rais hataki waguswe kwa kuwa wanatoka nyumba moja ccm.

Kama kweli rais anania ya kweli, kinga ya kutoshtakiwa wastafu ifutwe ili ile kauli ya "all people are equal before the law " iwe ni ya kweli na siyo selective kwa wapinzani na maskini
 
Hapa ndipo serikali inapokosea. Sababu iliyotumika kulifungia hili gazeti ni dhaifu mno.
Tukutane mahakamani!!!!!!

Tundu lissu upande huu na mparuka nywele upande ule!!!

Mahakama itawaita hao wapumzishwa
 
Viongozi wa afrika awapendi kuambiwa ukweli
Kama unavyoona Rais Magufuli hataki kuambiwa ukweli siku zote anawashambulia watu wote wanapomwambia ukweli. Anataka watu wote waseme 'Ndiyo Mzee' hata kama anaongea vitu visivyoingia akilini. Swala la sheria za madini huwezi kuliongelea bila kuwahusisha marais wa awamu ya 3 na ya 4. Sababu wao ndiyo walikuwa wasimamizi wakati sheria zinatungwa.
 
Msimu huu ni kuwindana tu......teh teh....
 
Very bad!
hivi wataalam wa uandishi, ukiandika habari ukaonesha nani aliyeisema wewe uliyeandika bado utaonekana kuwa na hatia? nini maana ya kuacknowledge habari? Kama aliyesema ni Lisu, gazeti limenukuu tu hapo kosa la gazeti ni lipi?
 
Ndo kazi pekee ambayo mawaziri wa habari na michezo wanaiweza kwa hapa Tz.
 
Freedom of expression ...watch it not to that extent .... Africa bado sana aisee ...
Mbona adhabu ndogo? They deserved more than that oh my God only 24months? I can't believe!

Jana Mbona Imetoka taarifa ya Serikali ya Kuyakataza Magazeti Leo Tarehe 15.06.2017 wamekuja na Habari Zilizokatazwa? Mmmh! Tuheshimu Mamlaka!
View attachment 524518
 
Hapa yule aliyepukutika kama unga wa muhogo mwilini mwake anatuchora na anapongezwa!!!
 
Bado haiondoi ukweli kua Ben na Mrisho walizingua hata hao wanaopigiwa kelele kua ni wezi watapona tu.Ccm hawasafishiki wote wezi tu.La muhimu ni kupiga kazi watoto wetu wale siasa za bongo ni kuumizana vichwa tu.Nashauri hata kina lisu kaeni kimya tu mnapigania wajinga kwa kupambana na wezi ila nani anawaona kwenye hili kundi la vipofu?
 
Haki ya asili imezingatiwa lakini!!? Je wamepewa muda wa kusikilizwa kabla ya adhabu kutolewa!? Maana wamefungiwa mara kadhaa lakini wakienda court wanafunguliwa. Mihemuko!
 
Haya, walianza na makinikia vizuri, mambo yanaenda smooth. Sasa wameanza kuboronga tena, huu ndiyo upuuzi gani? Miaka 2? hehehe what a joke
Huyo Dkt mzima na akili zake anachukua decisions za namna hii.
Tanzania viongozi simply don't care, wao hata kwa jambo dogo wakiamua kufunga a billion dollar business wanafunga.
 
so tuwajadili wahusika wengine tu ila hawa wawili waachwe. Hivi mawaziri watakaopandishwa kizimbani wakajitetea kwamba ulikuwa uamuzi wa pamoja wa baraza la mawaziri (ambalo Rais ndio Mwenyekiti) itakuwaje? Magufuli hadi leo akibanwa sakata la uuzaji wa nyumba za serikali anajibu "it was collective decision by cabinet".
 
Back
Top Bottom