Gazeti la Mwanahalisi: Makonda afadhiliwa na mataikuni wenye maslahi Ngorongoro. Atumia 6.2M ya malazi kwa siku

Lucas Mwashambwa njoo huku jemedali wa siasa paulo makonda
 
Analala hotel gani? Kuna shida gani kwenye nyumba ya mkuu wa mkoa?
 
Majungu tu hamna uhalisia kama hatumii hela ya serkali kuna shida gani?
 
tupe mchanganuo, ila kama anatatua kero za watu hamna shida, hivi helcopta ya mbowe si inatumia hizo hela kwa saa
 
Acheni uzushi wenu,acheni kumpaka matope Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara.natambua kuwa mnaumia sana mnapoona akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya wana Arusha na kuendelea kukubalika,kuungwa mkono na kuwaletea maendeleo makubwa.najuwa hali hiyo inawaumizeni sana kwa sababu ninyi mlisema hawezi kuongoza jiji la Arusha.

Sasa mnashangaa namna jiji lilivyotulia na kusifika kwa kasi na mipango ya maendeleo.mpaka kufikia hatua viongozi mbalimbali kumpongeza Mwamba kwa uchapakazi wake uliotukuka.

Ndio sababu ya kuanza kutunga vihabari vya uzushi na uongo.hata hivyo hamuwezi kumkwamisha Mwamba Mwenyewe Paul Makonda wala kumkatisha Tamaa.
 
MKuu tupe ufafanuzi wenye mantiki kuhusu iyo bajeti, anyway kama ni kweli basi hayo ni matumizi mabaya ya pesa za umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…