Hivi hilo deni na mimi nahusika kulilipa au watalilipa wenyewe. Maana mimi najihangaikia mwenyewe wala sijatumia hata senti tano ya deni la taifa. Kila kitu najinunulia kuanzia chakula, matibabu hadi elimu. Makazi yangu ya mbavu za mbwa nimejijengea mwenyewe na kabiashara kangu wanachukua kodi kila mwaka. Sasa hapo nadaiwaje wakati kila huduma nalipia na kisha niwalipe kodi kwa pesa ninayohangaika kuitafuta mimi mwenyewe? Mimi simo na silipi!