Bingwa wa mionzi na ugonjwa wa kirusi wapi na wapi.
Hususan daktari aliyeko USA ambako wao wana "a bigger fish to fry." Angejikita na ubingwa wake kusaidia huko huko USA wanakoongoza dunia kwa maafa ya janga hili.
Sayansi yako ya viral mutation ni potofu. Kama Watanzania hawapimwi, hawana chanjo, hawatibiwi, basi kirusi kama kipo kitasambaa, kuambukiza na kustawi kwa urahisi zaidi na hivyo hakutakuwa na shinikizo la kubadilika, evolutionary pressure, ya kuzalishwa jamii mpya ambayo ingepambana na mazingira magumu ya maisha ya kirusi katikati ya chanjo, dawa, barakoa, na umbali wa kimwili.
Na hata kama ingezalishwa jamii mpya ya kirusi bado huna hakika kama itakuwa hatari zaidi.
Nataka kuamini uliyoyasema hujayapata kwa bingwa wa mionzi.
Tanzania bado iko vizuri kwenye janga hili kinyume na bashiri na matarajio ya wengi.