GEITA: Afisa ardhi Agustino Sibeye mbaroni kwa kuwagonga na gari na kuwaua wanafunzi wanne wa shule ya msingi Ibambilwa

GEITA: Afisa ardhi Agustino Sibeye mbaroni kwa kuwagonga na gari na kuwaua wanafunzi wanne wa shule ya msingi Ibambilwa

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Afisa ardhi wilaya ya Nyangwale Agustino Sibeye kwa kuwagonga na gari wanafunzi wanne wa shule ya msingi Ibambilwa na kufariki dunia wakati wakivuka barabara kuelekea shuleni.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Hanry Mwaibambe amesema afisa huyo wa ardhi aliyejulikana kwa jina la Agustino Sibeye alisababisha vifo hivyo akiwa kwenye mwendo kasi eneo la makazi ya watu bila kuchukua tahadhari.

Wakati huo huo jeshi hilo linamshikilia Vestina Michael mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Mariamu Msalaba wakati akimtoa mimba nyumbani kwake kama anavyobainisha kamanda huyo.

 
Namfahamu huyu Afisa isee. Pole sana kwa familia waliopoteza watoto wao. Pole sana Afisa ardhi.
 
Buseresere kuzuri sana kule...samaki kama wote


Bottom line

RIP wanafunzi[emoji26]
 
Mwendo kasi ni mwendo upi? Sheria itahitaji kutafsiri mwendo kasi kwenye makaz aliokuwa nao mtuhumiwa ni UPI, na shahidi upande wa mashitaka itabidi atoe vielelezo kuosha Hiyo speed!
Mwisho mtuhumiwa anaweza kudai alikuwa speed ya 40kph lakijini watoto wakasukumana njiani akawagonga bahari mbaya!
Hivyo ataonbwa leseni na kulipa fine isiyozid laki mbili CASE CLOSED
 
Pole yao sana wafiwa... Na huyo aliyeua kwa kutoa mtu mimba kazi anayo...



Cc: mahondaw
 
Pole kwa wafiwa na mungu awalaze mahala pema watoto..
Injinia mtoa mimba Sorry pambana na hali yako


Kichwa BoX
 
Back
Top Bottom