Geita: Amchoma Mtoto kisu tumboni na kisha kujiua baada ya kugundua ana UKIMWI ila Mkewe hana

Hivi mbona haiingii akilini aisee huyo taahira kamuingizaje mtoto kwenye huo utopolo wake ?

Aiseee napendekeza serikali ianzishe program ya kupima watu wote magonjwa ya akili maana kwa Hilo tukio sidhani Kama linaingia akilini yani haaaaaaaaa khaaakhaaaaa

Mshenzi kweli huyo jamaa
Aaaaghhhhh lishaniharibia mood Hilo jamaa hivi watu wa hio kanda mnamatatizo gani lakini?
😥😥😥😥
 
Mkazi wa Nyantorotoro mkoani Geita, Shija Mwanzalima (30) amemjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni mwanae wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu kisha kujiua kwa kujinyonga.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea mwishoni mwa wiki nyumbani kwa mama wa mtoto huyo Nyantorotoro.

Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo baada ya mwanaume huyo pamoja na mkewe kwenda hospitali kupima afya na kuonekana ameathirika huku mkewe akiwa mzima licha ya kuishi pamoja.

Amesema baada ya majibu walirudi nyumbani na kumtuma mkewe dukani kununua dawa na kisha yeye kufanya unyama huo. Kwa mujibu wa kamanda mtoto alipata majeraha makubwa na amelazwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.

Kamanda ameishauri jamii kutatua matatizo ya kifamilia kwa njia ya majadiliano badala ya kuchukua maamuzi ambayo ni dhambi na ni kinyume na haki za binadamu.

Mwananchi
Na pengine yeye huyo marehemu ndy chanzo cha kulazimisha kupima.

Eboo!!
 
Huyo jamaa bora alivyokufa tu maana mawazo yake ni ya kijinga. Damu ya mwanaume mwenzio/huyo mtoto unaidhulumu vipi kwa ukimwi aliojitakia mwenyewe.
 
Mkazi wa Nyantorotoro mkoani Geita, Shija Mwanzalima (30) amemjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni mwanae wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu kisha kujiua kwa kujinyonga.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea mwishoni mwa wiki nyumbani kwa mama wa mtoto huyo Nyantorotoro.

Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo baada ya mwanaume huyo pamoja na mkewe kwenda hospitali kupima afya na kuonekana ameathirika huku mkewe akiwa mzima licha ya kuishi pamoja.

Amesema baada ya majibu walirudi nyumbani na kumtuma mkewe dukani kununua dawa na kisha yeye kufanya unyama huo. Kwa mujibu wa kamanda mtoto alipata majeraha makubwa na amelazwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.

Kamanda ameishauri jamii kutatua matatizo ya kifamilia kwa njia ya majadiliano badala ya kuchukua maamuzi ambayo ni dhambi na ni kinyume na haki za binadamu.

Mwananchi
Wasukuma tabia hii wameanza leo.
 
Inawezekana mkewe huyo hakumpa faraja baada ya hayo majibu,si unajua tena wake zetu hawa.

Inawezekana alimshushua ,ukome na umalaya wako mwaka huu utajibeba kwa raha zako.
Labda..yawezekana..
 
huyo alikuwa kashiba daku tu na si lingine
Imagine ukute alichanganya majina akatoa false
 
Labda..yawezekana..
Nahisi hivyo mkuu,kuna wakati niliingia biashara Fulani nikapigwa na wajanja kama m hvi,dah nikamshirikisha wife ila dah nilijawa na uchungu ila sikupata faraja nikaonekana nimekula na malaya.
 
Inawezekana mkewe huyo hakumpa faraja baada ya hayo majibu,si unajua tena wake zetu hawa.

Inawezekana alimshushua ,ukome na umalaya wako mwaka huu utajibeba kwa raha zako.
Wala asisingiziwe mkewe
 
Nahisi hivyo mkuu,kuna wakati niliingia biashara Fulani nikapigwa na wajanja kama m hvi,dah nikamshirikisha wife ila dah nilijawa na uchungu ila sikupata faraja nikaonekana nimekula na malaya.
Kama anakujua ni mwingi wa kuchepuka kukuamini ni ngumu sana.
 
Nahisi hivyo mkuu,kuna wakati niliingia biashara Fulani nikapigwa na wajanja kama m hvi,dah nikamshirikisha wife ila dah nilijawa na uchungu ila sikupata faraja nikaonekana nimekula na malaya.
Pole sana..lakini kusije kukawa kuna kahistoria fulani way back...yaani aanze tu kukurushia maneno ya kimo hicho? Au saa nyingine mnakosea padogo tu kwa kumshirikisha tayari mambo yakiwa yashakorogeka. Information angekuwa nayo hatua kwa hatua labda asingeyatamka hayo.
 
Back
Top Bottom