GEITA: Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizohonga, amuua

GEITA: Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizohonga, amuua

Kwani hizo pesa alikuwa anamuhonga bure?!

Mapenzi aliyokuwa akipewa mpaka akatoa hizo pesa anajifanya hakumbuki?!

Mpuuzi sana...

Unamdai mtu ulichompa kwa kukolewa na penzi?!

Mpaka hapo huyo jamaa keshaonesha udhaifu aliokuwa nao..
 
Kwani hizo pesa alikuwa anamuhonga bure?!

Mapenzi aliyokuwa akipewa mpaka akatoa hizo pesa anajifanya hakumbuki?!

Mpuuzi sana...

Unamdai mtu ulichompa kwa kukolewa na penzi?!

Mpaka hapo huyo jamaa keshaonesha udhaifu aliokuwa nao..
 

Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua​


WhatsApp-Image-2021-06-29-at-13.09.24-660x400.jpeg
Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.

Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu.

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe’’ Kamanda Mwaibambe.

Aidha amesema mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.
Hapa Rapcha ajifunze kitu
 
Uamuzi wa kijinga sana huu,ndoa hailazimishwi,ndoa ni hisia,but mapenzi yanauma,kama mtu huna nia nae ni bora ukamwambia mapema ili kuepusha majanga kama haya,

Jamaa anaenda kuozea jela kisa makaratasi! bila shaka kwa muda huu anajutia sana maamuzi yake But it's too late,

Siku zote usichukue maamuzi ukiwa na hasira wala usitoe ahadi ukiwa na furaha.
To every action there's an equal and opposite reaction. Ndio maana mm huwa sihudumii kabla sijaoa. Upo kwa wazazi wako waliokuzaa hawawezi kushindwa kukuhudumia kama hutaki sepaaaaaaaaa, kwendraaaaaaaaaaa. Zaidi utapewa zawadi tu ya kijihela kidogo cha kukusukuma.
 
Uamuzi wa kijinga sana huu,ndoa hailazimishwi,ndoa ni hisia,but mapenzi yanauma,kama mtu huna nia nae ni bora ukamwambia mapema ili kuepusha majanga kama haya,

Jamaa anaenda kuozea jela kisa makaratasi! bila shaka kwa muda huu anajutia sana maamuzi yake But it's too late,

Siku zote usichukue maamuzi ukiwa na hasira wala usitoe ahadi ukiwa na furaha.
Siku yakikukuta ndio utajua.
 
Lakini Wazazi wa binti,mnapigiwa simu kuwa binti yenu anadaiwa kutumia fedha za "mwanaume asiyempenda" mnakaa kimya(yaani mnapotezea tu wakati hali ya utafutaji ni ngumu)...
Jamaa kumbe alikuwa mstaarabu namna hii mpaka kufuata wazazi wa binti!
 
Kuna jamaa wa eneo hilo nimemcheki
Anasema mwamba alikua anadai Tsh 45,000 na simu ndogo ya tecno aliyomnunulia manzi

Jamaa mishe zake ni kuchoma mahindi ya miamia
Dah kmmmk walai 😂😂😂
 
Tuwe waaminifu wajameni, wengi naona wanamshambulia jamaa kwa maamuzi yake na kufurahia adhabu atayopewa lakini hatugusii huyu aliupoteza uhai wake walau hata hiyo jela jamaa anaendelea kuishi...
Waambie hawa tena wanavyojua kuangusha bill sasa, nywele, kodi, shopping ya nguo, simu hapo yote hayo malipo ni bao moja tena bila ushirikiano!
 
Mshamba mmoja. Kumla amemla sana na kumuua juu.Pole kwa mama aliyezaa kwa utungu na uchungu.Wanakheri wasiopenda mahusiano na kuamua kuishi kivyao kufa kivyao pia.AMINA
 
Back
Top Bottom