Geita iwe Kanda maalum ya Kipolisi kama ilivyo Dar es salaam na Mara

Geita iwe Kanda maalum ya Kipolisi kama ilivyo Dar es salaam na Mara

Watu wameshituka na baadhi ya matukio ya kusikitisha yanayotokea Geita kama mauaji ya Mirembe, Eneck, Albino n.k, Kwa tuliowahi kuishi Geita haya ni matukio ya kawaida mno

Geita Kuna uharifu wa kutisha, ubabe, ukatili, unyanganyi, ujambazi wa hali ya juu, yaani habari zingine Huwa hazifiki mitandaoni

Ni kawaida watu kuvamia gulio, minada ya mifuko na masoko kuiba na kuondoka

Ukifika Katoro, Runzewe, Bukombe Mganza, Geita Mjini na Nyang'wale, Biharamlo, na Mganza huo umafia upo na watu washazoea

Albino, vikongwe, watoto au wazazi Kwa Imani za kishirikina ni matukio mengi ya kawaida

Geita polisi hawana nguvu, nakumbuka nikiwa Katoro 2014 Kuna muhuni alikamatwa Kwa ubakaji, basi wahuni usiku wakamtafuta mkuu wa kituo nyumbani kwake wakamuamrisha amutoe mahabusu na akatii akamfungulia yule bwana akatoroka

Mkoa wa Geita unatisha, sema ndo hivo haisikiki, kama mtu atabisha akaishi Geita hata wiki 1 litapigwa tukio atabaki mdomo wazi

Uharifu unaofanyika Geita hata Dar es salaam na Mara hazijafika nusu

Serikali ikiweka Kanda maalum ya Kipolisi itapunguza uharifu kama walivyodhibiti mkoa wa Mara, Sasa umetulia Wakurya wamekuwa wapole

Wasukuma wana mambo ya ajabu ajabu sana.

Kaa nao huku vijijini ndio mtaelewa
 
Back
Top Bottom