Uchaguzi 2020 Geita Mjini: Mbinu chafu dhidi ya Upendo Peneza

Uchaguzi 2020 Geita Mjini: Mbinu chafu dhidi ya Upendo Peneza

nkuwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2013
Posts
4,806
Reaction score
5,347
Wasalaam,

Upendo Peneza najua unapita hapa au wasaidizi wako wanapita hapa, kuna Mbinu chafu kuzuia ushindi wako Kesho na haya yanafanywa na msimamizi wa uchaguzi Geita Mjini akushirikiana na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.

Semina zilizofanyika Juzi na Jana wasimamizi wa vituo wamepewa maelekezo kuhakikisha kanyasu na magufuli wanashinda Kwa namna yeyote, wanakiri kabsa kuwa hali ni mbaya Kwa kanyasu na Kwa magufuli pia.

Mbinu watakazotumia
1. Maeneo ambayo hasa ndio ngome yako wameambiwa wahakikishe wanam-frustate wakala wako, akipaniq wataagiza polisi amuondoe Kwenye kituo halafu kitakachofuata kura za kimamluki zitapigwa Kwa Kanyasu na Magufuli

(Namna ya kushughulika na hili wakala atulie asipaniki hata kama atachokozwa)

2. Maeneo mengi ambayo kuna watu hawajui kusoma na kuandika mf. Kaseni, Bwihegule, Nyaseke, Gamashi,, Bumanji na vijiji vya ndani kabsa wataweka MTU wa CCM kuwasaidia kupiga kura Kwa Kanyasu na Magufuli, Sheria inasema MTU mmoja asaidie mtu mara moja lakini tumeelekezwa lazima MTU wa CCM ambaye amepangwa kuwasaidia wewe kama msimamizi wa kituo umtambue na umruhusu kufanya hivyo ili kuokoa chama.

3. Mawakala kukabidhi simu Kwa msimamizi wa kituo. Hii ni Mbinu Yao, hakuna Sheria inayolazimisha wakala kutokuwa na simu kwenye kituo, tulichoagizwa sisi wasimamizi wakala akigoma kukabidhi simu agiza polisi akamatwe na atiwe ndani asitoke,

(namna ya kushughulikia hili mawakala wako wasiingie Kwenye huu mtego watatolewa wote alafu kura zitaibiwa, watulie ni Bora wanyang'anywe simu ila wao wabaki Kwenye vituo kulinda kura)

4. Hizo zote juu zikikwama, matokeo yatabadilishwa Kwenye vituo vya kata Kwa msimamizi msaidizi

(namna ya kushughulikia hili hakikisha Una wakala anayejielewa Kwenye kila kituo cha kata Kwenye majumuisho ya kura, usiwaamini na kuwaachia madiwani pekee)

4. Hakikisha unaweka kituo chako cha kukusaidia kukusanya matokeo (nakala za matokeo za mbunge na rais pindi yanapobandikwa) hili unaweza kulifanya Kwa kanda, kanda ya kasamwa uwe na kituo na pia kanda ya Geita uwe na kituo ili kufikia SAA 2 usiku uwe na nakala zote za matokeo ya ubunge na urais, (nasisitiza nakala za matokeo vituoni uwe nazo wewe na uzitunze vizuri)

5. Vituo vilivyopo Kwenye shule za Nyankumbu girls, Geseco, kasamwa secondary kuwa navyo makini wanafunzi wenye Kadi za kupigia kura wanalazimishwa kumpigia kanyasu na magufuli Kwa nguvu, na wanaweza hata kutumia wanafunzi wasiona Kadi kupiga kura za maruhani

Baada ya hapo unaweza kujumlisha matokeo yako ukiwa umeshinda anzeni kusheherekea ushindi ukimsubiri ndugu apolinary akutangaze, ukishindwa kuwa na nakala za matokeo yako na rais mapema umeliwa mdogo wangu

Tumeapa kutenda haki na sio kusaidia wizi Kwa CCM

Tunakupenda Sana, kila lililo ovu juu yako halitafanikiwa!
 
Mkuuu hayo uliyoandika ndoo hayo hayo tuliolezwa na kulazimishwa kuyafanya huku Tanga,mm bora kazi wanifukuze kuliko kutenda dhuluma ya wazi wazi na kujitafutia laana ya wananchi.Anaejua maisha ya mwanadamu ni Mungu peke yake,hata hawa wanao tutishia kuwa hata kazi watatufukuza hawajui hata hiyo j'5 kama watafika.Mungu awalaaani wenye kufanya dhuluma na awape misuko suko kwenye maisha yao wasipate raha kwenye viti hivyo wanavyo vitafuta kwa nguvu
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Mkuuu hayo uliyoandika ndoo hayo hayo tuliolezwa na kulazimishwa kuyafanya huku Tanga,mm bora kazi wanifukuze kuliko kutenda dhuluma ya wazi wazi na kujitafutia laana ya wananchi.Anaejua maisha ya mwanadamu ni Mungu peke yake,hata hawa wanao tutishia kuwa hata kazi watatufukuza hawajui hata hiyo j'5 kama watafika.Mungu awalaaani wenye kufanya dhuluma na awape misuko suko kwenye maisha yao wasipate raha kwenye viti hivyo wanavyo vitafuta kwa nguvu
Shikilia msimamo wako Mungu atakujazi
 
Chadema ni watu wa vurugu na uongo

Mnasingizia baada ya kukataliwa na Watanzania
L
Heri chadema watakaokataliwa na watanzania kuliko wewe utakaekataliwa mbinguni kwa ajili ya upumbavu sugu
 
Mkuuu hayo uliyoandika ndoo hayo hayo tuliolezwa na kulazimishwa kuyafanya huku Tanga,mm bora kazi wanifukuze kuliko kutenda dhuluma ya wazi wazi na kujitafutia laana ya wananchi.Anaejua maisha ya mwanadamu ni Mungu peke yake,hata hawa wanao tutishia kuwa hata kazi watatufukuza hawajui hata hiyo j'5 kama watafika.Mungu awalaaani wenye kufanya dhuluma na awape misuko suko kwenye maisha yao wasipate raha kwenye viti hivyo wanavyo vitafuta kwa nguvu
Usithubutu mkuu ukibaijika familia yako inaweza chomwa, ukweli ni kwamba hakuna atakayekufukuza kazi Ila ukisikia mambo ya ccm utaliwa na watu
 
Sisi mbona huku hatujaambiwa hayo bali tuliambiwa tufuate sheria na taratibu za uchaguzi.

Back
Top Bottom