Geita: Wanaume kutosikilizwa kumechangia msongo wa mawazo na Vifo kwenye ndoa

Geita: Wanaume kutosikilizwa kumechangia msongo wa mawazo na Vifo kwenye ndoa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Imeelezwa kuwa wanaume wengi bado wanakosa nafasi ya kusikilizwa, hali inayochangia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao katika familia nyingi, jambo linalosababisha msongo wa mawazo mkubwa, ambao kwa baadhi ya wanaume umesababisha vifo.

Hayo yameelezwa kwenye kongamano la kujadili masuala ya ukatili ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa EPZA wilayani Geita, ambapo Mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Geita Christina Katana pamoja na Mwenyekiti wa wajane wilaya ya Geita, Mchungaji Nyamizi Muhangwa, wameelezea kuwa ukatili wa kingono, kimwili, kihisiana kiuchumi umekuwa changamoto kubwa, huku ukatili wa kiuchumi ukitajwa kutochukuliwa kwa uzito unaostahili kwa wanaume.

Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la Rafiki SDO, Elihud Mtelemwa amesema kuwa vitendo vya ukatili havichagui jinsia wala umri na vinaendelea kushika kasi kubwa.
 
nani kasema tunataka kusikilizwa..?
Hata kama tukisikilizwa hayatendewi kazi, na tukiongea tunaonekana hatuna vifua!!.
Ukiwasilisha jambo lako ati umedundwa na mkeo unachekwa kwanza!, then unapewa vyako!.
sanasana mwanaume ukileta za kuleta unaambiwa uache nyumba si yako ni ya familia! wewe ukatafute pakuweka mbavu zako!.

lazima ufe kikatili sana!.
 
Back
Top Bottom