Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

Kama mkoa wa Chato utaanzishwa ningeshauri makao makuu yawe Nyakanazi itakuwa rahisi kwa watu wa Biharamulo,Ngara na Kakonko kufika kirahisi ....Maana Chato ipo kushoto Sana kuwa makao makuu ya mkoa huo mpya.
 
Hizo ulizotaja zilikuwa na sbabu za msingi kabisa. tofauti na geita, kigoma kumegwa ili kumfurahisha magufuli
Inavyoelekea hapo jina Magufuli ndio halijakupendeza.

Issue hapa ambayo ipo contested ni unequal distribution ya hizo source of resources.

Mfano kwa Arusha kulikua na umuhimu gani kupeleka machimbo ya Tanzanite mkoa mpya wa Manyara na kuupoka Mkoa mama wa Arusha?? Hiyo haikuwa fair, Ila walioamua kipindi hicho walifanya Kwa utashi wao.
 
mkuu kuna ujinga mwingi sana hii nchi. Umaacha kuigawa Moro au Tabora halafu unaenda kuokoteza wilaya kwa sababu za utashi wa marehemu
Kugawa mkoa kuna vigezo vingi vya kiidadi ya watu, huduma za kiutawala, kiuchumi nk
 
Ngara iliwekeza Sana kwenye shule zilizopo bukoba zilipoletwa shule za Kata ikapigwa na sasa unaenda kupigwa ianze moja. Kwani niwemugizi yeye anasemaje
Mkuu majimbo ya kanisa RC hayazingatii mipaka ya kiserikali.
Kwa mfano Jimbo la Morogoro linachukua mpaka chalinze na bagamoyo ambapo ni Mkoa wa Pwani kiserikali.

Kwa hiyo Kugawanywa upya hiyo mikoa hakutaathiri Sana uwekezaji uliofanywa na Diocese
 
Kwa hiyo sifa ya mkoa ni kujengwa kwa misingi ama viashiria vya ukabila? Makabila mawili au zaidi hayawezi kuwa chini ya mkoa mmoja?

Sioni sababu za msingi za kuugawa mkoa wa Geita wenye idadi ya watu China ya idadi ya 1.8 mln! Huku ni kupoteza rasilimali!
Zanzibar Ni Nchi japo Ina watu kidogo chini ya 2m. Sembuse Chato yenye International Airport. Wacha Iwe Mkoa na Jina Liwe Magufuli.
 
Kama nchi bado hatujajua vipao mbele vyetu kabisa.
Geita bado Mkoa mchanga halafu inagawanywa tena.
Yani ni Sawa na mtoto kupigwa mimba azae mtoto mwenzake
 
Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Zaidi, soma; News Alert: - Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato
Kuwa na mkoa wa chato ni sawa na MME was imani ya kikiristo kuwa na wake wawili akilazimisha wote afunge nao ndoa...
 
Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Zaidi, soma; News Alert: - Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

Iyo sawa tu maana ni moja ya njia ya kuleta maendeleo
 
mkuu kuna ujinga mwingi sana hii nchi. Umaacha kuigawa Moro au Tabora halafu unaenda kuokoteza wilaya kwa sababu za utashi wa marehemu
Morogoro ina vigezo vyote bila hata kuokota okota na kuomba omba wilaya mkoa jirani.

Asee bila katiba hii nchi itaongizwa kama ina mmiliki
 
Mkuu majimbo ya kanisa RC hayazingatii mipaka ya kiserikali.
Kwa mfano Jimbo la Morogoro linachukua mpaka chalinze na bagamoyo ambapo ni Mkoa wa Pwani kiserikali.

Kwa hiyo Kugawanywa upya hiyo mikoa hakutaathiri Sana uwekezaji uliofanywa na Diocese
Hilo nalijua mkurugenzi .nilimaanisha shule zilizopo bukoba zilijengwa na mkoa mzima wakafaidi walangira na kuna miundombinu kibao inejengwa na wananchi WA mkoa mzima kinachosikitisha ngara inajiunga kwenye mkoa mchanga kabisa
 
Vile kivuli cha Kayafa kinahakikisha kuwa Chato inakuwa mkoa!
4jHF.jpg
 
Buriani Geita. Ni ushamba kuna ulazima gani? Mbona Morogoro haigawiki?
Morogoro inastahili kabisa kugawanywa! Siyo kwa ukubwa ule! Hata ukiiangalia tu kwenye ramani ya Nchi, unaona kabisa Morogoro ni Mkua mkubwa sana! Yaani mtu atoke Ulanga, Malinyi au Mlimba, mpaka afike Moro mjini yalipo Makao Makuu ya Mkoa, ni safari ya kutwa nzima!!!

Ila ndiyo hivyo tena! Chato inakuwa Mkoa kwa lengo tu la kuienzi Legacy ya magufuli! Moro imekosa kabisa mtu wa kuisemea! Inatia huruma sana.
 
Pay master wa wizara ya fedha ambaye ni mchaga amekwapua billioni 1.5 ndani ya miezi miwili.
 
Morogoro inastahili kabisa kugawanywa! Siyo kwa ukubwa ule! Hata ukiiangalia tu kwenye ramani ya Nchi, unaona kabisa Morogoro ni Mkua mkubwa sana! Yaani mtu atoke Ulanga, Malinyi au Mlimba, mpaka afike Moro mjini yalipo Makao Makuu ya Mkoa, ni safari ya kutwa nzima!!!

Ila ndiyo hivyo tena! Chato inakuwa Mkoa kwa lengo tu la kuienzi Legacy ya magufuli! Moro imekosa kabisa mtu wa kuisemea! Inatia huruma sana.
Jambo la aibu ni jinsi wanavyolazimisha kuunga unga hizo wilaya. Morogoro ni muda mrefu sana inaliliwa lakini wapi
 
Utakuwa ni mkoa unaofikika kiurahisi toka pande zote za Tanzania maana unafikika kwa barabara, maji na ndege.

Makao makuu ya mkoa yatakuwa Chato na hapa kuna kila aina ya fursa, utalii,kilimo na uvuvi.

Hivyo ni kipindi cha watanzania waende kuwekeza Chato kwenye kila sekta kama kilimo, uvuvi na viwanda.

My take: Chato kuwa mkoa ni sehemu ya kuenzi kazi kubwa aliyoifanya JPM kwa taifa letu
 
Itakua ajabu kama huu mkoa utawahi zaidi ya morogoro na tanga ambazo zishamaliza mchakato muda ila kwa kifupi naona kama haitowezekana.... Ukiwezekana pia itapendeza
 
Back
Top Bottom