Gen Z amkabia trafiki kwa juu. Ambana Trafiki kwa kumrekodi muda wote ili asipokee rushwa

Gen Z amkabia trafiki kwa juu. Ambana Trafiki kwa kumrekodi muda wote ili asipokee rushwa

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu


Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Ezra Kachelo amezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya kumfukuza afisa wa polisi wa usalama barabarani (trafiki) aliyekuwa akituhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa madereva wa matatu katika Kaunti ya Kiambu.

Katika video iliyosambaa kwa kasi mtandaoni, Ezra anaonekana akitembea sambamba na afisa huyo wa polisi aliyekuwa amevaa fulana ya njano ya usalama, huku akirekodi kila hatua kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ezra alikuwa akiwapigia kelele madereva wa matatu na magari binafsi yaliyokuwa yakipita akisema, "Piteni! Hakuna pesa mnayopaswa kumpa mtu yeyote hapa leo!"



 
Vijana wa kenya washukuru hakuna maswala ya
1789546914355.jpeg
 
Back
Top Bottom