Gen Z wa Tanzania wapewe ajira maana ukosefu wa ajira ni chanzo cha maandamano tunayoshuhudia Kenya na sasa Uganda

Maandamano ya General Z wa Tanzania hayana sababu za msingi ajira zinatangazwa Kila kukicha na Serikali na sekta binafsi lakini yote kwa yote Serikali haina uwezo wa kuajiri vijana wote wa Tanzania hii isipokuwa watu kujiajiri wenyewe na ukizingatia Serikali inatafuta masoko ya mazao Kila leo mfano kusini watu wanapiga pesa ya korosho,ufuta na mbaazi,wakulima wa mahindi Zambia wanahitaji Tani 650,000/= NFRA wananunua kilo moja ya mahindi shs.700 kwa mjini na vijijini 600 ,ardhi imejaa tele nchi nzima,mvua za uhakika halafu kijana anaililia Serikali eti maisha magumu vijana wa Kenya wangekuwa na ardhi kama hii yetu tusingewaona kwenye maandamano zaidi ya kuwepo mashambani.
 


Ajira zinatokana na uwekezaji. Uwekezaji unakuja kama kuna mazingira mazuri ya biashara na mfumo imara. Tanzania haina mazingira mazuri ya biashara na mifumo mizuri. Tukipigania hapa mabadiliko ya mifumo bora na mazingira mazuri ya biashara mnatakiwa kuelewa tunapigania vijana wetu lakini wengi wenu hamuelewi na kuishia kubeza beza tu na wajinga jinga sana. Kazi haziokotwi na serikali inapata pesa kutoka kwenye kodi kazi yake sio kuajiri watu bali watu wachacha tu watekelezaji. Ajira zinatoka sekta binafsi.
 
Bora yaje tuanze upya, kuna koo Tanzania hazizidi 10 zinaishi kwenye sayari nyingine tofauti na sisi yaani zinaogelea kwenye utajiri na raha kwa kodi za watanzania wanyonge
 
Wasingoje ajira za serikali tu, waingie mitaani kwenye sekta binafsi.
wewe mbona hukuingia kwenye hiyo sekta binafsi? acheni ujinga, familia zenu zimejazana serikalini na mitaji mnayo ya kuwapa watoto wenu tena mikubwa, mbona hamuwapi hiyo mitaji watoto wenu waingie sekta binafsi?
 
MTU akikunyima ELIMU BORA

Akakupa simba na yanga

Ukaanza kufatilia connection

Na mwisho ukaamini umerogwa
 
Kwanza kwa nchi masikini kama Tanzania hapakupaswa kuwa na mtumishi wa umma wa ngazi yoyote ile anayelipwa zaidi ya milioni 3 kama kweli ni uzalendo na siyo wizi wa mali za umma, badala ake kuna watu wanalamba mpk milioni 50 kwa mwezi nje na posho kibao, milioni 50 ingeweza kulipa graduate zaidi ya 60, nje na matumizi makubwa na ya anasa + wizi wa mali za umma.
 
Kila mmoja anaboda yake
 
Wewe ni mchochezi
 
wewe mbona hukuingia kwenye hiyo sekta binafsi? acheni ujinga, familia zenu zimejazana serikalini na mitaji mnayo ya kuwapa watoto wenu tena mikubwa, mbona hamuwapi hiyo mitaji watoto wenu waingie sekta binafsi?
Sijawahi kuajiriwa na serikali.
 
Tupo katika wakati ambao vijana wetu wengi wanapitia hali ya sintofahamu hatima ya maisha yao kutokana tatizo kubwa ukosefu wa ajira.

Ni vyema watu wote wenye mamlaka wajue wanatatua vipi tatizo wanahaidi Nini na hatua gani watakazoenda kuzichukua
Hali kwa sasa inaonekana ni shwari mana watawala wameshajihakikishia ulinzi kutoka kwa polisi

Itafika muda ambao vijana watakuwa hawana Cha kupoteza vijana wengi wamekosa matumaini itafika mahali ambapo ata mtu ataona yeye akifa hana atakalolipoteza
 
Watawala wanajiaminisha kuwa vijana wa TZ bado sana hawajitambui ndio maana wana promote boda boda kama kipaumbele cha ajira.
 
Mimi kama muwakilishi wa Generation Z nasema ya kwamba HATUTO ANDAMANA WALA KUFANYA VURUGU UNAYOIHAMASISHA!! KAMA wewe kweli unataka ufanye VURUGU nenda ofisi ya serikali iliyokaribu ukajitokeze kuliko kujificha nyuma ya keyboard
 
Mimi kama muwakilishi wa Generation Z nasema ya kwamba HATUTO ANDAMANA WALA KUFANYA VURUGU UNAYOIHAMASISHA!! KAMA wewe kweli unataka ufanye VURUGU nenda ofisi ya serikali iliyokaribu ukajitokeze kuliko kujificha nyuma ya keyboard
Mkuu umesoma na kuelewa kilichoandikwa? Au umerukia gari kwa mbele? Soma kwa kutafakari na kutulia sijaona alipohamasisha vurugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…