Wadau Asalam aleykum.
Wanasema mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Nawashauri viongozi wangu mlioko kwenye vyombo vya kutunga sera, mfanye kuwaajiri vijana walioko mtaani wenye ujuzi na wasio na ujuzi pia watafutiwe kazi za kufanya.
Hii itawafanya kuwa bize na hivyo kuwasahaulisha na ugumu wa maisha wanaokabiliana nao sasa.
Viongozi wangu, msijiamini kupitiliza kwamba nyinyi mna mifumo imara kuliko huko kunakofuka moto sasa.
Wanasema mwenye njaa mara zote huwa na hasira.
Pia wanasema kama huna kazi ya kufanya, basi chochote kinachokuja mbele yako unaweza kujikuta unakifanya! Shetani huwatumia sana wasio na kazi kutimiza agenda zake ovu.
Maandamano ni kama ugonjwa wa kuambukiza. Mara nyingi nchi nyingi zenye matatizo kama vile Libya, Tunisia, Misri, Sudan, na sasa Kenya na Uganda, maandamano huwa yanaanza kidogo kidogo na baadaye kusambaa nchi nzima!
Kama hali ikiendelea hivi ilivyo, basi tusishangae kuwaona Gen Z wetu nao wakiingia barabarani kuandamana.
Naomba kuwasilisha.