Wakristo wanapendaga tu kusema hivyo ili kuitukuza dini yao kwamba ni ya amani mbele ya waislamu ambao inawachoresha kama watu wa upanga ilaSoma historia, kabla ya 610 AD Uarabuni mpaka India na north Africa yote ilikuwa ni ukristo. Uislam ulipoanza waliuwa WAKRISTO wote wa maeneo hayo au kuwasilimisha kwa nguvu ili waendelee kuishi. Wenyeji WAKRISTO kwa wapagani walikuwa na uchaguzi mmoja tu. Kufa au kusilimu ili ubaki hai, lakini sio kuwa huru na ukristo au upagani wako.
Siyo kweli hawakuuliwa walikuwa assimilated. Iko hivi waislamu walivyoanzisha himaya zao za mwanzoni. Waliteka maeneo mengi ikiwemo the arabian gulf (siku hizi ni eneo la saudi arabia, yemen, oman, UAE, bahrain, kuwait) waliteka nchi takatifu yaani Israeli au wengine wanaiita palestina sambamba na syria. Pia waliteka eneo lote la Afrika kaskazini (siku hizi ni Morocco, Libya, Algeria, Tunisia na Misri) waliteka pia Uajemi (siku hizi Iran) na pia waliteka the Iberian peninsula (siku hizi ni Hispania na Ureno).
Katika muktadha wa kisasa unaweza kuhisi labda himaya kujitanua hivyo ilikuwa ni kitu cha ajabu. Lakini enzi hizo ilikuwa ni kawaida, taifa lolote lenye nguvu kubwa za kijeshi lilikuwa linajitanua kutengeneza himaya kubwa. Nadhani unasomaga biblia sasa hipo hivi Israeli wale unaowasomaga hawakuwahi kuwa na himaya kubwa kwasababu ya udhaifu wao siyo kwasababu walikuwa hawapendi. Ila mataifa mengine kama uajemi (soma kitabu cha Ezra, Esther, Nehemiah n.k), babeli (soma kitabu cha wafalme wa pili) na ugiriki (soma kitabu cha wamakabayo wa kwanza na wa pili) walifanikiwa kutengeneza himaya kubwa. Hata hivyo hizo himaya zote zilianguka kama ambavyo zile caliphate zilianguka. All empires fall.
Sasa ili kutengeneza himaya walikuwa wanafanyaje. Wanakuja na jeshi wanaenda eneo fulani wanasema kuanzia sasa eneo hili liko chini ya mtawala flani mtamlipia kodi na kufuata sheria zake. mkileta ubishi maana ake ni vita atakaeshinda anateka eneo. Msipobisha hakuna atakaewagusa, ata kuwafinya tu hakuna. Kwa hiyo wakisha teka eneo moja wanaenda jingine hivyo hivyo mpaka wanatawala himaya kubwa kweli.
Kwa waislamu lengo lao la kwanza la operesheni zao za kijeshi ilikuwa kutanua himaya yao kama ilivyokuwa desturi ya himaya nyingine enzi hizo. Lengo lao halikuwa kuwasilimisha watu au walau kuwalizimisha wawe waislamu. Hasa hasa kwa wakristo na wayahudi walikuwa hawawalazimishi katu kuwa waislamu. Tena dini ya kiislamu inawatambua wakristo na wayahudi kama watu wa kitabu. Ndio maana mpaka leo takribani asimilia 10 ya watu wamisri ni wakristo wa madhehebu ya coptic. Madhehebu hayo ni madhehebu ya kikristo ya kale sana walijitenga na askofu wa roma mnamo mwaka 451AD kabla uislamu haujaanza. Siyo kama nyie wapentekoste dhehebu lenu halina hata miaka 300. Lebanon ina wakristo takribani asilimia 35 wa madhehebu ya greek orthodox hao walijitenga na kanisa la roma mnamo 1054AD. Lebanon wapo pia wakristo wanaomtii askofu wa roma kama huku Tanzania tunawafahamu kwa jina hili kanisa katoliki la roma.
Sasa kilichokuwa kinatokea ni hiki, ukiishi katika dola ya kiislamu na ukiwa muislamu unaenjoy some privileges, kwa hiyo wengi tu walikuwa wanasilimu siyo kwasababu wameshikiwa panga shingoni waache ukristo, hapana bali mtu anaona yanini kulipa lipa makodi yasiyo na ishu bora nisilimu yaishe. Ndio hivyo baba usije ukafikiri kila mtu ana imani kubwa hivyo