General Muhoozi akishika madaraka tutafata Tanzania baada ya kuwa DRC wameisha, tujipange

Soma historia, kabla ya 610 AD Uarabuni mpaka India na north Africa yote ilikuwa ni ukristo. Uislam ulipoanza waliuwa WAKRISTO wote wa maeneo hayo au kuwasilimisha kwa nguvu ili waendelee kuishi. Wenyeji WAKRISTO kwa wapagani walikuwa na uchaguzi mmoja tu. Kufa au kusilimu ili ubaki hai, lakini sio kuwa huru na ukristo au upagani wako.
Wakristo wanapendaga tu kusema hivyo ili kuitukuza dini yao kwamba ni ya amani mbele ya waislamu ambao inawachoresha kama watu wa upanga ila

Siyo kweli hawakuuliwa walikuwa assimilated. Iko hivi waislamu walivyoanzisha himaya zao za mwanzoni. Waliteka maeneo mengi ikiwemo the arabian gulf (siku hizi ni eneo la saudi arabia, yemen, oman, UAE, bahrain, kuwait) waliteka nchi takatifu yaani Israeli au wengine wanaiita palestina sambamba na syria. Pia waliteka eneo lote la Afrika kaskazini (siku hizi ni Morocco, Libya, Algeria, Tunisia na Misri) waliteka pia Uajemi (siku hizi Iran) na pia waliteka the Iberian peninsula (siku hizi ni Hispania na Ureno).

Katika muktadha wa kisasa unaweza kuhisi labda himaya kujitanua hivyo ilikuwa ni kitu cha ajabu. Lakini enzi hizo ilikuwa ni kawaida, taifa lolote lenye nguvu kubwa za kijeshi lilikuwa linajitanua kutengeneza himaya kubwa. Nadhani unasomaga biblia sasa hipo hivi Israeli wale unaowasomaga hawakuwahi kuwa na himaya kubwa kwasababu ya udhaifu wao siyo kwasababu walikuwa hawapendi. Ila mataifa mengine kama uajemi (soma kitabu cha Ezra, Esther, Nehemiah n.k), babeli (soma kitabu cha wafalme wa pili) na ugiriki (soma kitabu cha wamakabayo wa kwanza na wa pili) walifanikiwa kutengeneza himaya kubwa. Hata hivyo hizo himaya zote zilianguka kama ambavyo zile caliphate zilianguka. All empires fall.

Sasa ili kutengeneza himaya walikuwa wanafanyaje. Wanakuja na jeshi wanaenda eneo fulani wanasema kuanzia sasa eneo hili liko chini ya mtawala flani mtamlipia kodi na kufuata sheria zake. mkileta ubishi maana ake ni vita atakaeshinda anateka eneo. Msipobisha hakuna atakaewagusa, ata kuwafinya tu hakuna. Kwa hiyo wakisha teka eneo moja wanaenda jingine hivyo hivyo mpaka wanatawala himaya kubwa kweli.

Kwa waislamu lengo lao la kwanza la operesheni zao za kijeshi ilikuwa kutanua himaya yao kama ilivyokuwa desturi ya himaya nyingine enzi hizo. Lengo lao halikuwa kuwasilimisha watu au walau kuwalizimisha wawe waislamu. Hasa hasa kwa wakristo na wayahudi walikuwa hawawalazimishi katu kuwa waislamu. Tena dini ya kiislamu inawatambua wakristo na wayahudi kama watu wa kitabu. Ndio maana mpaka leo takribani asimilia 10 ya watu wamisri ni wakristo wa madhehebu ya coptic. Madhehebu hayo ni madhehebu ya kikristo ya kale sana walijitenga na askofu wa roma mnamo mwaka 451AD kabla uislamu haujaanza. Siyo kama nyie wapentekoste dhehebu lenu halina hata miaka 300. Lebanon ina wakristo takribani asilimia 35 wa madhehebu ya greek orthodox hao walijitenga na kanisa la roma mnamo 1054AD. Lebanon wapo pia wakristo wanaomtii askofu wa roma kama huku Tanzania tunawafahamu kwa jina hili kanisa katoliki la roma.

Sasa kilichokuwa kinatokea ni hiki, ukiishi katika dola ya kiislamu na ukiwa muislamu unaenjoy some privileges, kwa hiyo wengi tu walikuwa wanasilimu siyo kwasababu wameshikiwa panga shingoni waache ukristo, hapana bali mtu anaona yanini kulipa lipa makodi yasiyo na ishu bora nisilimu yaishe. Ndio hivyo baba usije ukafikiri kila mtu ana imani kubwa hivyo
 
Sasa ngoja nikwambie kuhusu kampeni za wakristo enzi hizo. Tusome historia

Kwanza kulikuwa na kampeni za kuikomboa Hispania na Ureno kutoka kwenye utawala wa waislamu hiyo kampeni waliiita reconquista. Wakaanzisha vita dhidi ya watawala wakiislamu maeneo hayo na wakafanikiwa waliiteka cordoba mwaka 1236 kisha wakaiteka sevilla mwaka 1248 walipata support ya baba mtakatifu Innocent wa tatu. Vita vilikuwa vikiendelea tu mpaka mwaka 1492 ndipo watawala wakiislamu walipo salimu amri kabisa wakristo wakatengeneze ufalme wakikatoliki katika maeneo hayo.

Pili mwaka 1069 wakristo walitamani kuiteka nchi takatifu yaani palestina mikononi mwa waislamu. Na wakaanzisha vita vya kidini yaani vita vitakatifu dhidi ya watawala wakiislamu. Kampeni hizo za kijeshi zilikuwa zinaitwa kwa kiingereza crusades. Siku hizi neno crusades walokole mnalitumia kwenye kampeni zenu za uinjilishaji ila asili ya hilo neno ndio hilo. Mwaka 1099 crusaders walifanikiwa kuukamata mji wa Yerusalemu. Na crusaders walikuwa wametumwa na si mwingine bali Baba mtakatifu Urbano wa pili kuikomboa palestina kutoka kwa wapagani. Kipindi waislamu walikuwa wanawaheshimu sana wakristo na kuwaita watu wa kitabu, wao waroma walikuwa wanawaita wenzao wapagani. Vita hivyo vitakatifu viliendelea mpaka mwaka 1291, tofauti na kule hispani huku waislamu walishinda na kuitamalaki nchi takatifu. The crusaders walirudi nyumbani.

Takbir

Mimi ni mkristo by the way ila napendaga tu hiyo salamu.
 
Vitu vyote muhimu,kwa jeshi, silaha za kisasa, teknolojia mpya, mavazi, chakula, ustahamilivu, mapenzi ya nchi na kubwa zaidi ni ujasiri sina hakika na wanajeshi wetu wa sasa wale wazee wetu walikuwa jasiri kweli kweli. Angalia Congo wanajeshi wanatupa silha alafu wanakimbia wanasema Kamanyola kila mtu acheze anavyojua. Lakini pia uongozi bora na imara yaani jemedari mkuu wa majeshi na kiongozi anayepiganisha vita. Sababu za kumpiga tunazo, nia ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao.....Hii ni hotuba ya kuhamasisha watu wapigane jee bado tunayo
Kwa sasa ubinafsi na kiburi kilichokithiri kwa kundi dogo la viongozi na machawa wao dhidi ya raia nina hakika mpasuko huo upo mpaka huko kwenye majeshi sema ni vile tu hatuwezi kuyafahamu ya huko ndani kwao.

Kunakuwa na kundi dogo linaneemeka in expense of others. Mpasuko ukiwa mkubwa ndio yatatokea hayo ya kutupa silaha kana kwamba napigana kwa faida ya nani😂?
 
Kulinganisha na wabongo na waganda eh? Yes they are better ndio maana mkiambiwa fungueni mipaka ya East Africa mnahara oh eti watachukua ardhi yenu! Kama hujui hili na wewe upo kulekule
kwayo hicho ndio kigezo unachotumia kuwaona wakenya wako smart? una uwezo duni sana wa kufikiri...

Haya hao hao wakenya huwa hawawependi waethiopia na wasomali, kwa hiyo tuseme hao waethiopia na wasomali nao ni smart kuliko wakenya?

Akili zako duni we jamaa na pia una inferiority complex
 
Kwa sasa ubinafsi na kiburi kilichokithiri kwa kundi dogo la viongozi na machawa wao dhidi ya raia nina hakika mpasuko huo upo mpaka huko kwenye majeshi sema ni vile tu hatuwezi kuyafahamu ya huko ndani kwao.

Kunakuwa na kundi dogo linaneemeka in expense of others. Mpasuko ukiwa mkubwa ndio yatatokea hayo ya kutupa silaha kana kwamba napigana kwa faida ya nani😂?
"Napigana kwa faida ya nani"

Aisee umenikumbusha siku moja niko zangu kwenye gari za Kawe, njiani akapanda mjeda mmoja akaa karibu yangu, tukajikuta tunazoeana ghafla tu, jamaa alianza kufunguka mambo mengi sana tena kwa uchungu, akisema huko mipakani kuna mambo mengi sana ya ovyo yanaendelea, huko mipakani magari yanapita bila kukaguliwa kwa amri za mabosi wa...
 
😁....Mboga Mboga FC
 
kwayo hicho ndio kigezo unachotumia kuwaona wakenya wako smart? una uwezo duni sana wa kufikiri...

Haya hao hao wakenya huwa hawawependi waethiopia na wasomali, kwa hiyo tuseme hao waethiopia na wasomali nao ni smart kuliko wakenya?

Akili zako duni we jamaa na pia una inferiority complex

Hilo tu, we ukiwa na uwezo mkubwa si unatosha? Akili za kukariri darasani, wakati huna result yoyote ya maana inanifikirisha mie?! Ukweli unaujua unaleta akili za jiwe hapa, mnawaogopa kwa kila namna anyway. Mnaliwa left right na watawala mnajilinganisha na wakenya? Wanajitambua ukanda wote wa Africa sio East tu
 
Sasa ngoja nikwambie kuhusu kampeni za wakristo enzi hizo. Tusome historia

Kwanza kulikuwa na kampeni za kuikomboa Hispania na Ureno kutoka kwenye utawala wa waislamu hiyo kampeni waliiita reconquista. Wakaanzisha vita dhidi ya watawala wakiislamu maeneo hayo na wakafanikiwa waliiteka cordoba mwaka 1236 kisha wakaiteka sevilla mwaka 1248 walipata support ya baba mtakatifu Innocent wa tatu. Vita vilikuwa vikiendelea tu mpaka mwaka 1492 ndipo watawala wakiislamu walipo salimu amri kabisa wakristo wakatengeneze ufalme wakikatoliki katika maeneo hayo.

Pili mwaka 1069 wakristo walitamani kuiteka nchi takatifu yaani palestina mikononi mwa waislamu. Na wakaanzisha vita vya kidini yaani vita vitakatifu dhidi ya watawala wakiislamu. Kampeni hizo za kijeshi zilikuwa zinaitwa kwa kiingereza crusades. Siku hizi neno crusades walokole mnalitumia kwenye kampeni zenu za uinjilishaji ila asili ya hilo neno ndio hilo. Mwaka 1099 crusaders walifanikiwa kuukamata mji wa Yerusalemu. Na crusaders walikuwa wametumwa na si mwingine bali Baba mtakatifu Urbano wa pili kuikomboa palestina kutoka kwa wapagani. Kipindi waislamu walikuwa wanawaheshimu sana wakristo na kuwaita watu wa kitabu, wao waroma walikuwa wanawaita wenzao wapagani. Vita hivyo vitakatifu viliendelea mpaka mwaka 1291, tofauti na kule hispani huku waislamu walishinda na kuitamalaki nchi takatifu. The crusaders walirudi nyumbani.

Takbir

Mimi ni mkristo by the way ila napendaga tu hiyo salamu.
Kama WAKRISTO walianzisha kuikomboa Asia na ulaya ni sawa. Kukomboa maana yake uliporwa kabla. Ukweli tunaokubaliana ni kuwa uislam haukuwahi kuwepo kabla ya 610 AD. Waliua kueneza dini. Mohamed alizaliwa 570 AD.
 
Wakristo wanapendaga tu kusema hivyo ili kuitukuza dini yao kwamba ni ya amani mbele ya waislamu ambao inawachoresha kama watu wa upanga ila

Siyo kweli hawakuuliwa walikuwa assimilated. Iko hivi waislamu walivyoanzisha himaya zao za mwanzoni. Waliteka maeneo mengi ikiwemo the arabian gulf (siku hizi ni eneo la saudi arabia, yemen, oman, UAE, bahrain, kuwait) waliteka nchi takatifu yaani Israeli au wengine wanaiita palestina sambamba na syria. Pia waliteka eneo lote la Afrika kaskazini (siku hizi ni Morocco, Libya, Algeria, Tunisia na Misri) waliteka pia Uajemi (siku hizi Iran) na pia waliteka the Iberian peninsula (siku hizi ni Hispania na Ureno).

Katika muktadha wa kisasa unaweza kuhisi labda himaya kujitanua hivyo ilikuwa ni kitu cha ajabu. Lakini enzi hizo ilikuwa ni kawaida, taifa lolote lenye nguvu kubwa za kijeshi lilikuwa linajitanua kutengeneza himaya kubwa. Nadhani unasomaga biblia sasa hipo hivi Israeli wale unaowasomaga hawakuwahi kuwa na himaya kubwa kwasababu ya udhaifu wao siyo kwasababu walikuwa hawapendi. Ila mataifa mengine kama uajemi (soma kitabu cha Ezra, Esther, Nehemiah n.k), babeli (soma kitabu cha wafalme wa pili) na ugiriki (soma kitabu cha wamakabayo wa kwanza na wa pili) walifanikiwa kutengeneza himaya kubwa. Hata hivyo hizo himaya zote zilianguka kama ambavyo zile caliphate zilianguka. All empires fall.

Sasa ili kutengeneza himaya walikuwa wanafanyaje. Wanakuja na jeshi wanaenda eneo fulani wanasema kuanzia sasa eneo hili liko chini ya mtawala flani mtamlipia kodi na kufuata sheria zake. mkileta ubishi maana ake ni vita atakaeshinda anateka eneo. Msipobisha hakuna atakaewagusa, ata kuwafinya tu hakuna. Kwa hiyo wakisha teka eneo moja wanaenda jingine hivyo hivyo mpaka wanatawala himaya kubwa kweli.

Kwa waislamu lengo lao la kwanza la operesheni zao za kijeshi ilikuwa kutanua himaya yao kama ilivyokuwa desturi ya himaya nyingine enzi hizo. Lengo lao halikuwa kuwasilimisha watu au walau kuwalizimisha wawe waislamu. Hasa hasa kwa wakristo na wayahudi walikuwa hawawalazimishi katu kuwa waislamu. Tena dini ya kiislamu inawatambua wakristo na wayahudi kama watu wa kitabu. Ndio maana mpaka leo takribani asimilia 10 ya watu wamisri ni wakristo wa madhehebu ya coptic. Madhehebu hayo ni madhehebu ya kikristo ya kale sana walijitenga na askofu wa roma mnamo mwaka 451AD kabla uislamu haujaanza. Siyo kama nyie wapentekoste dhehebu lenu halina hata miaka 300. Lebanon ina wakristo takribani asilimia 35 wa madhehebu ya greek orthodox hao walijitenga na kanisa la roma mnamo 1054AD. Lebanon wapo pia wakristo wanaomtii askofu wa roma kama huku Tanzania tunawafahamu kwa jina hili kanisa katoliki la roma.

Sasa kilichokuwa kinatokea ni hiki, ukiishi katika dola ya kiislamu na ukiwa muislamu unaenjoy some privileges, kwa hiyo wengi tu walikuwa wanasilimu siyo kwasababu wameshikiwa panga shingoni waache ukristo, hapana bali mtu anaona yanini kulipa lipa makodi yasiyo na ishu bora nisilimu yaishe. Ndio hivyo baba usije ukafikiri kila mtu ana imani kubwa hivyo
Story ndeefu. Fupisha tu kwa kusema, uislam uliteka na kuua kueneza dini.
 
Hilo tu, we ukiwa na uwezo mkubwa si unatosha? Akili za kukariri darasani, wakati huna result yoyote ya maana inanifikirisha mie?! Ukweli unaujua unaleta akili za jiwe hapa, mnawaogopa kwa kila namna anyway. Mnaliwa left right na watawala mnajilinganisha na wakenya? Wanajitambua ukanda wote wa Africa sio East tu
Unaandika kama vile teja ambaye ana alosto ya madawa ya kulevya, sijajua mshabiano wowote wa kimantiki kati ya hayo maneno yalipo kwenye bold na comment yangu iliyopita

Wewe ni limbukeni tu wa siasa za fujo huna lolote kichwani, hao wakenya kama wanajitambua au wako smart kuna nini cha maana walicholifanyia taifa lao kuleta tofauti na mataifa mengine ya afrika? Umewahi kufika huko kwao ukajionea maisha yao kwanza wanavyoishi??? Umewahi kuona makazi yao?

Bila shaka wewe utakuwa ni likenya au wale watanzania mliozoea kujikomba komba kwa hao manyang'au... niambie hao wakenya wamelifanyia nini taifa lao mpaka kuwaona wao wako smart kuliko waafrika wengine?? Kama ni kuliwa hata wao pia serikali yao inanuka rushwa na wanaliwa sana tu licha ya maandamano ya mara kwa mara kupinga miswada kandamizi...

Narudia tena wewe ni limbukeni wa siasa za fujo na akili zako ni duni sana japo hujui hili.
 
Sawa this is good for your mental health, tchao, usijpata breakdown buree wkt mi nipo kwa entertainment ya wajinga kama nyie nikapige zangu mkwanja baada ya hapa! Bitterness haitamaliza shida zako tho
 
Usikatae, hata hii comment yako inaonyesha furaha,, eti wanawasaidia FDLR kuivamia Rwanda. Kwani wewe kama ni Mtanganyika kama mimi Rwanda inakuuma nini kama sio mtusi.
DRC hawajawahi kusaidia FDLR.
Sio kweli Kuna kipindi kiongozi wa FDRL aliuwawa na jeshi la Congo
 
Usikatae, hata hii comment yako inaonyesha furaha,, eti wanawasaidia FDLR kuivamia Rwanda. Kwani wewe kama ni Mtanganyika kama mimi Rwanda inakuuma nini kama sio mtusi.
DRC hawajawahi kusaidia FDLR.
Sio kweli Kuna kipindi kiongozi wa FDRL aliuwawa na jeshi la congo
 
Enzi zile TPDF ilikuwa ni jeshi lilikuwa na maaskari wazalendo na ndio maana lilikuwa ni tishio katika Afrika tofauti na sasa hivi ambapo hata sare tu nzuri za kisasa hawana ukiachilia mbali silaha za kisasa.
Kwa sasa kuja aina flani hivi ya share za jeshi ambazo ndo zinaenda na siraha na vifaaa vya jeshi
 
Nyuzi zake nyingi nasoma huyu jamaa inawezekana ni wa nje
Umeanza kuzisoma lini?

Mtu wa nje atawashauri mboreshe Jeshi lenu liwe la kisasa? Kama ni hivyo basi si ndo inabidi awe raia maana hakuna mtu humu Jamii Forums kawahi kuweka uzi wa kutoa tahadhari kwa Jeshi letu kama mleta mada(mimi).
 
Jeshi la Tanzania hata MRAP hakuna
Patrol zinafanywa kwa kutumika Toyota land cruiser. Aibu kwa jeshi la serikali kutumika hizo.

T14 Armata
 
Kansa ya Wizi ya matumizi mabaya ya fedha za wananchi imeshaziambukiza taasisi zetu tulizoziamini sana kama JWTZ. Na hii inasabishwa na Jeshi letu kuanza kumezwa na Wanasiasa. Ni vizuri wafahamu kuwa Pesa nyingi inapaswa kununua vifaa vya kisasa vya mapambano na kwenye mafunzo ya kutumia vifaa hivyo.

Wanatakiwa wabadilike. Jeshi ndo taasisi pekee ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiogopwa na Wanasiasa hasa CCM na ndo mana Jeshi letu liliweza kuwa imara kwa muda mrefu.

Nao wakiwa kama TISS kuwa makondoo wa CCM basi wajue ipo siku inakuja nchi yetu nayo itaanza kumegwa kama Congo.

Wanatakiwa wasimame kama walivyosimama wenzao kwenye Mutiny ya 1964 na wale wengine waliombeep Nyerere mwaka 1981/82 hadi Nyerere mwenyewe kuamua kung'atuka na kumuachia Mwinyi Urais mwaka 1985.
 
Back
Top Bottom