General Tyre [EA] Ltd kuanza uzalishaji mwaka 2013

kama sehem kubwa ya share itabaki kwa serikali nadhani itakuwa good move,what we need ni 50+ ya SHARE iwe kwa serikali ili kama Taifa tunufaike na hasa kwenye ajira.

Hope mkuu,utaendelea kutupa UPDATE za nini kinaendelea kwa kuwa u-mjumbe mzuri,Karibu sana kaka!
 
Sawa Ngongo ila serikali hii unayoipongeza ndiyo iliua GT husasan Waziri wa sasa Abdalah Kigoda; watu wamekosa kazi miaka 10. Serikali imekosa mapato.

Nina wasiwasi kama wewe. hili jitu lijiitalo dr kikalio bado ni waziri la viwanda na biashara. sijui, napendekeza govt iuze shares kwa watz ili wawe na sauti katika uendendeshaji wa kampuni letu.
 
Mkuu Mgaya D.W ni kweli serekali haiatawekeza ila imeipatia fedha NDC kuandaa mazingira mazuri [Matengenezo] ya kuvutia wawekezaji huku serekali ikibakiza hisa nyingi mikononi mwake.Tayari makampuni ya Ujerumani,Malasia,Brazil na Uturuki yameshatoa offer kwa NDC namna gani watakavyowekeza iwapo watachaguliwa.NDC wapo katika hatua za mwisho za kumpendekeza mbia mwenye kukidhi vigezo wanavyovitaka ikiwemo technology ya kisasa,uwezo wa mtaji.

Serekali pia itayatoa mashamba ya mpira yaliyoko Tanga na Morogoro kama sehemu ya mtaji wake.

Mkuu Ngongo ama kwa hakika hii ni hatua nzuri kwakweli maana watanzania waliokuwa wamepoteza ajira angalau sasa watapata tena ajira, na wengine pia wasiokuwa na ajira watajipatia ajira hapo. Na kikubwa zaidi kiwanda hicho kitachangia sana pato la taifa kwakuwa tairi ni bidhaa adimu na tukikumbuka ubora wa tairi za General tyre bila shaka itaweza kukidhi viwango na ubora wa soko la afrika mashariki na kati.

Wasiwasi wangu ni mmoja tu, NDC wasije wakafanya yale mambo yetu ya uswahili-10% na kutuletea mbia/muwekezaji asiyekuwa na uwezo.
 
Last edited by a moderator:
Heshima kwenu wanajamvi,

Wakuu General Tyre inafanyiwa ukarabati mkubwa wa majengo na mashine/mitambo kwaajili ya kuanza uzalishaji mwakani Mungu akipenda.NDC wamekabidhiwa kazi ya kuifufua General Tyre tayari mafundi umeme wameshaanza kazi ya kubadilisha nyaya za umeme chakavu.Jengo la utawala limeshamaliziwa kupigwa rangi na matengenezo madogo madogo yanafanyika kwa kasi ya ajabu.

Inatarajiwa kabla ya mwakani kati ya mwezi wa tatu hadi mwezi wa tano mitambo mipya na yenye technology ya kisasa itafungwa katika eneo lilojulikana kama New bay.Mitambo iliyokuwa ikitumika zamani na bado ina ubora wa sasa ni ile iliyokuwa ikizalisha tairi ndogo Grabber AP 215 R 15 / 205 R 16 / 31 X 10.5 R 15 LT / 165 R 13 / 175 R 14 / 185 R 15/14.Pia mould za matari size 750 - 16 HCT 8PLY,10PLY & SHCT 12PLY itaendelea kutumiwa kwakuwa tairi zake bado zinahitajika sokoni hasa magairi aina ya Land Rover & Land Cruiser kwa safari za porini[Utalii].

Naipongeza serekali kwa hatua nzuri ilizoanza kuzichukua naamini ongezeko kubwa la magari Tanzania ni soko la uhakika kwa matairi ya General Tyre.Tusisahau pia soko la EA bado liko wazi sana pamoja na kampuni ya kuzalisha matairi ya KENYA kuiba technology ya General Tyre hasa tyre 750 - 16 HCT 10 ply bado halijafikia ubora wa tairi la Genral Tyre nina hakika siku uzalishaji ukianza YANA ya Kenya watafunga virago Tanzania.

Nakala: Ritz PakaJimmy TUMBIRI Matola Crashwise sweke34 mayega Mimibaba Jasusi Mtambuzi Mwita Maranya zumbemkuu Dotworld Nyange OSOKONI Mzee Mwanakijiji Richard Molemo BAK Mzee wa Rula Bigirita zomba Nyumbu Pasco Kubwajinga Mchambuzi Nguruvi3 Invisible samora10 Arushaone kitalolo Roulette The Boss MpendaTz Mkusa Mag3 MVUMBUZI na wengine wote

Naomba kuwasilisha.

Kama kweli hicho kiwanda kitaamka we will be making one step in the right direction.
 
ni habari njema, hasa nakumbuka kale katangazo ka ''General Tyre na gari lake'' ndo ninalokumbuka tu maana redio yetu ilikuwa inashika RTD tu,
 
Katika majembe ambayo CDM imetuletea watanzania, Zitto ni mmoja wao, nilidhani alikuwa anapigana an uphill battle, ila naona mwishowe wametoa penzi. Nasubiri kiwira na mchuchuma ..... what a good fight.

Naongea kama mtanzania.
 
Key Stakeholders kwa hili ni Sekta ya Usafiri; Mimi huwa najiuliza - kwanini mkazo ni mkubwa sana kufufua General Tyre badala ya kulipa nguvu zaidi shirika letu la reli? Wapi kuna faida zaidi kiuchumi? Kwa maana nyingine - between a well functioning TRC/TRL and a well functioning General Tyre, wapi tuna add more value in terms of economic growth, employment and inflation on a macro scale?

Miaka ya 1970s, TAZARA ilipingwa kwa nguvu zote na kada hii hii inayoipigia debe kufufuka kwa General Tyre, na walipinga ujio wa TAZARA kwa hoja nyingi nyepesi nyepesi na za ovyo lakini baadae ikaja kubainika kwamba kumbe ni kwasababu TAZARA ingeua soko la matairi ya mabasi na malori kutoka kiwanda cha Firestone, Kenya;

With all due respect kwa efforts za kukufua Kiwanda hiki, hasa kutoa ajira kwa ndugu zetu wa Arusha, sioni General Tyre itasaidiaje uchumi wa taifa ikifananishwa na TRL in terms of - economic growth, employment, na tatizo la mfumuko wa bei; Hakuna taifa lililosonga mbele na linalo survive leo bila ya a well functioning railways system; Sasa kwa vile Kiwanda cha GT kinalenga sekta ile ile ya usafiri wa mizigo, bidhaa za kilimo, wananchi n.k, tuendelee nayo lakini tusiache TRL;
 
Nadhani tatizo ni gharama za kufufua reli zetu kulinganisha na viwanda (baadhi).
 
Sawa Ngongo ila serikali hii unayoipongeza ndiyo iliua GT husasan Waziri wa sasa Abdalah Kigoda; watu wamekosa kazi miaka 10. Serikali imekosa mapato.

Miaka 10 iliyopita "serikali hii" haikuwepo madarakani.
 
Ni hatua nzuri hiyo serikali imetimiza wajibu wake, ila lazima tuelezwe sababu zilizopelekea General tyre ikafa kwanza na serikali ilipata hasara kiasi gani na hatua zipi zilichukuliwa kwa waliohusika, hii itasaidia hii general tyre mpya iweze ku operate smoothly isije kufa tena baada ya miaka michache!asante kwa taarifa mkuu Ngongo!
 
Halafu mkiambiwa Kikwete anafanya kweli mnaanza kuingia viwanda vya kufuwa uongo.
 
Wakuu wawekezaji wote tayari wameshatembelea General Tyre na kujionea wenyewe hali halisi.Jambo moja kubwa lililowashangaza sana ni hali ya utunzaji wa thamani na mashine.Computers,printers,photocopy machine,meza,viti,viyoyozi na mashine zote vilikuwa katika hali nzuri.

Mkuu Mchambuzi ni kweli reli ni muhimu katika ujenzi wa uchumi imara lakini gharama za kuifufua ni kubwa mno inabidi serekali ijipange sawa sawa.Gharama za kuifufua General Tyre ni ndogo sana utashangaa sana baadhi ya mitambo mingi itahitaji kupakwa grease tu ?.Mould za kupika matairi za saizi mbali mbali zipo haziitaji matengenezo kabisa zaidi ya kusafishwa,bambari inafanyakazi,boiler zipo mbili zote nzima kabisa,sehemu ya kufunga mashine mpya ipo sana sana itahitaji kuoshwa na kufutwa utando wa bui bui.

Bwana L Mgoyo,Bwana Palangyo ,Bwana Urassa na Bwana Athumani wanastahili pongezi za dhati kwa uaminifu wao wa kutunza kumbukumbu za vifaa vyote bila kuchakachua.
 
Last edited by a moderator:
Great news, wasiwasi wangu upo kwenye Sustainability, je serikali imejipanga vip kuibeba general tyre inayotaka kufufuka huku kukiwa na ushidani wa hali ya juu kwa bidhaa toka china?
 
Key Stakeholders kwa hili ni Sekta ya Usafiri; Mimi huwa najiuliza - kwanini mkazo ni mkubwa sana kufufua General Tyre badala ya kulipa nguvu zaidi shirika letu la reli? Wapi kuna faida zaidi kiuchumi? Kwa maana nyingine - between a well functioning TRC/TRL and a well functioning General Tyre, wapi tuna add more value in terms of economic growth, employment and inflation on a macro scale?

Mkuu waswahili tuna msemo "yarabi nafsi yangu"; kwa sisi tulio Arusha GT ilikuwa zaidi ya kitega uchumi cha taifa. Pamoja na umuhimu wa TRC/TRL kwetu sisi Arusha kufa kwa GT tumeishuhudia ilivyoathiri jamaa zetu. Bravo Lema kwa kuikomalia ifufuliwe.

Miaka ya 1970s, TAZARA ilipingwa kwa nguvu zote na kada hii hii inayoipigia debe kufufuka kwa General Tyre, na walipinga ujio wa TAZARA kwa hoja nyingi nyepesi nyepesi na za ovyo lakini baadae ikaja kubainika kwamba kumbe ni kwasababu TAZARA ingeua soko la matairi ya mabasi na malori kutoka kiwanda cha Firestone, Kenya;

Sawa ni serikali hii iliyoshirikiana na manyang'au kufanya unayosema. Na nyuma ya Kenya kuna multinationals ambazo watoa maamuzi wetu wana bei rahisi tu na sisi kuvuna mabua kwa kupokea ushauri mbovu. Kwa hiyo wanapokirudi hatuna sababu ya kuwapongeza, kwanza wamechelewa sana kujirudi. Halafu kifo cha TRC/TRL na GT kimetokea katika awamu/wakati mmoja kwa hiyo ni imani yangu TRC/TRL nazo zitafufuliwa kama GT wakati huu huu.

With all due respect kwa efforts za kukufua Kiwanda hiki, hasa kutoa ajira kwa ndugu zetu wa Arusha, sioni General Tyre itasaidiaje uchumi wa taifa ikifananishwa na TRL in terms of - economic growth, employment, na tatizo la mfumuko wa bei; Hakuna taifa lililosonga mbele na linalo survive leo bila ya a well functioning railways system; Sasa kwa vile Kiwanda cha GT kinalenga sekta ile ile ya usafiri wa mizigo, bidhaa za kilimo, wananchi n.k, tuendelee nayo lakini tusiache TRL;

Heshima mkuu sikubaliani nawe na kulinganisha kwako kiuchumi. Pia naomba niwe honest WHO CARES ABOUT TAIFA? CCM na genge la mafisadi NO! NO! NO! Nakukumbusha takwimu zinaonesha ni kweli uchumi wetu unakua lakini ni uchumu wa akina nani? Ni wa watawala wakati uchumi huo haushuki chini mifukoni kwetu; sana sana kuna walioweka pesa Uswizi. Hapa kwa uhalisia GT inachangia sana uchumi wa wakazi wa Arusha.

Cha ziada reli TRC inafika Arusha lakini kwa hoja yako hiyo hiyo ilikufa kwa manufaa ya biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara. Mimi ni mtaalamu wa uchukuzi na najua kelele za wananchi kuhusu reli zinaingia sikio moja na kutoka sikio la pili kwa sababu wafanyabiashara wa kutumia barabara kwa kuiua reli ni watawala na viongozi wa chama tawala. Hawatafanya maamuzi ya kujinyonga.

Dunia nzima ya kikabaila na ya kijamaa wanajua jinsi reli inavyo stabilise na kusustain bei za bidhaa kwa sababu ya uwezo wake wa kusafirisha bidhaa kwa wingi na kwa bei isiyobadirika badirika, na zaidi matengenezo ya mara kwa mara ni kidogo sana. Watawala wetu kwa ubinafsi wao wanatumia raslimali nyingi ya Taifa kwenye barabara kwa sababu ya manufaa ya biashara zao za usafirishaji kwa njia hiyo.

Kifupi GT ni kwa manufaa yanayojidhihirisha kwa watu wa Arusha. Kama kuna usafirishaji wa barabara unaowanufaisha watawala basi na sisi watu wa Arusha tutanufaika kwa kuwazalishia matairi.
 
Mkuu Mgaya D.W ni kweli serekali haiatawekeza ila imeipatia fedha NDC kuandaa mazingira mazuri [Matengenezo] ya kuvutia wawekezaji huku serekali ikibakiza hisa nyingi mikononi mwake.Tayari makampuni ya Ujerumani,Malasia,Brazil na Uturuki yameshatoa offer kwa NDC namna gani watakavyowekeza iwapo watachaguliwa.NDC wapo katika hatua za mwisho za kumpendekeza mbia mwenye kukidhi vigezo wanavyovitaka ikiwemo technology ya kisasa,uwezo wa mtaji.

Serekali pia itayatoa mashamba ya mpira yaliyoko Tanga na Morogoro kama sehemu ya mtaji wake.

Unaonaje sasa sisi wajasiriamali tuanze kulima huo mpira :biggrin:
 
Key Stakeholders kwa hili ni Sekta ya Usafiri; Mimi huwa najiuliza - kwanini mkazo ni mkubwa sana kufufua General Tyre badala ya kulipa nguvu zaidi shirika letu la reli? Wapi kuna faida zaidi kiuchumi? Kwa maana nyingine - between a well functioning TRC/TRL and a well functioning General Tyre, wapi tuna add more value in terms of economic growth, employment and inflation on a macro scale?

Miaka ya 1970s, TAZARA ilipingwa kwa nguvu zote na kada hii hii inayoipigia debe kufufuka kwa General Tyre, na walipinga ujio wa TAZARA kwa hoja nyingi nyepesi nyepesi na za ovyo lakini baadae ikaja kubainika kwamba kumbe ni kwasababu TAZARA ingeua soko la matairi ya mabasi na malori kutoka kiwanda cha Firestone, Kenya;

With all due respect kwa efforts za kukufua Kiwanda hiki, hasa kutoa ajira kwa ndugu zetu wa Arusha, sioni General Tyre itasaidiaje uchumi wa taifa ikifananishwa na TRL in terms of - economic growth, employment, na tatizo la mfumuko wa bei; Hakuna taifa lililosonga mbele na linalo survive leo bila ya a well functioning railways system; Sasa kwa vile Kiwanda cha GT kinalenga sekta ile ile ya usafiri wa mizigo, bidhaa za kilimo, wananchi n.k, tuendelee nayo lakini tusiache TRL;

Mchambuzi,

Our wish ni kuona viwanda vyote vinafufuka lakini hiyo haiwezekani kwa sasa.

Angalia kiasi gani fedha za kigeni nchi inatumia kuagiza matairi kutoka nje?

Nadhani ni zaidi ya kutoa ajira kwa wana Arusha labda baadae tutaachana na DUNLOP na MICHELLIN
 
Sawa nyani haoni kundule

Serikali hii inafanya vyema zaidi ya Serikali yeyote ya kabla yake. Kama unalo japo moja tu ambalo Serikali hii haijafanya zaidi ya Serikali zote zilizopita, litaje.

Nakuhakikishia utachemsha!
 
Back
Top Bottom