Key Stakeholders kwa hili ni Sekta ya Usafiri; Mimi huwa najiuliza - kwanini mkazo ni mkubwa sana kufufua General Tyre badala ya kulipa nguvu zaidi shirika letu la reli? Wapi kuna faida zaidi kiuchumi? Kwa maana nyingine - between a well functioning TRC/TRL and a well functioning General Tyre, wapi tuna add more value in terms of economic growth, employment and inflation on a macro scale?
Miaka ya 1970s, TAZARA ilipingwa kwa nguvu zote na kada hii hii inayoipigia debe kufufuka kwa General Tyre, na walipinga ujio wa TAZARA kwa hoja nyingi nyepesi nyepesi na za ovyo lakini baadae ikaja kubainika kwamba kumbe ni kwasababu TAZARA ingeua soko la matairi ya mabasi na malori kutoka kiwanda cha Firestone, Kenya;
With all due respect kwa efforts za kukufua Kiwanda hiki, hasa kutoa ajira kwa ndugu zetu wa Arusha, sioni General Tyre itasaidiaje uchumi wa taifa ikifananishwa na TRL in terms of - economic growth, employment, na tatizo la mfumuko wa bei; Hakuna taifa lililosonga mbele na linalo survive leo bila ya a well functioning railways system; Sasa kwa vile Kiwanda cha GT kinalenga sekta ile ile ya usafiri wa mizigo, bidhaa za kilimo, wananchi n.k, tuendelee nayo lakini tusiache TRL;