General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Moshi tena kuna kiwanda cha kikubwa cha kuchana mbao na kuchemsha nguzo za umeme mkabala na Kibo Breweries marehemu nacho vipo maeneo ya machinjioni uwiiiiiii nchi yangu
 
Daaah Mungu aturehemu kweli naamini Tz ni pango la wahalifu
 
Nakumbuka miaka ya 85 hadi 95 tulikuwa tukipeleka kuuza kahawa KNCU tunapeleka kama ni gunia 20. Unapewa dawa bure na magunia mapya toka kiwanda cha moshi bure
Hiyo imebaki history
 
Katika kumbukumbu nilizo nazo za utotoni ni mwaka 1985 wakati huo nikiwa darasa la 5 kijijini, kulikuwa na kipindi shule inapanga kwenda kutembea (kutalii)...katika sehemu tulizotembelea ilikuwa general tyre na hifadhi ya momela...bado ile harufu ya mipira pale general tyre naikumbuka...ilikuwa ni ndoto kudhania kitu kama kile kingekuja kufa kirahisi vile!!!....nakumbuka pia bites nilizopewa kwa ajili ya safari yalikuwa mahindi ya kukaanga then yakalowekwa kwenye maji yenye magadi!!!. Siku hizi utasikia..dadiii!! Kesho tunafunga shule tumeambiwa tuende na chama, cheuro, biscuits na juisi ya seres!!! Daah maisha haya!!!....kwa mara ya kwanza mwaka huu napiga kura. . Na ni against cc..m
 
Hakipo siku hizo ukipita hapo ni kama gofu fulani vile mkabala na Kiltex kulikuwa na kiwanda kingine sikumbuki vizuri kama kilikuwa kinatengeneza bidhaa gani siku hizi ni kanisa la kiNigeria watu wanaimba na kumwabudu Mungu uzalishaji hakuna kabisa.

Ngongo

Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??
 
Machine tools, coffee curing, zzk, ufi, kiltex, mwatex, kncu, kaudo,kauma, kamata, nmc, sukita,ndc na mashirika na viwanda vingine lukuki!!...hivi tungekuwa wapi leo!! Ni nani mwenye dhamira ya dhati ya kuturudishia Tanzania yetuu jamani!!!!
 
FaizaFoxy anachungulia tu huu uzi hata hachangii
 
Last edited by a moderator:
Ngongo

Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??
Kulikuwa na kiwanda kingine kilichoitwa KILITEX pia, kilikuwa Gongolamboto. Nasikia kilipofilisika wafanyakazi waligawana vyerehani, wakafikia hatua hadi ya kung'oa bati za paa. ....
 
Kama hilo llilikuwa shirika la umma vipi msishangae mashirika ya umma yote yaliyokufa mshangae hilo tu?

Ni nini kinatafutwa? Tanganyika Packers vipi?
 
Back
Top Bottom