Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa anaye fahamu sababu ya kuiba vinu vya kutengeneza matairi ya ubora wa hali ya juu kutoka kiwanda maarufu Nchini na Duniani kilichokuwepo Arusha juzi juzi tu cha General tyres na kuvihamishia Kenya ambapo wanavitumia kutengenezea matairi ya Yana tyres then wanakuja kutuuzia hayo matairi huku Tanzania, nini chanzo?
============================
==========================================
==================================
=====================================
Mkuu Mimi niliwahi kufanyakazi General Tyre so kila hatua ya kuifisadi na kuizika niliiona kwa macho yangu mawili.
Kwanza nakunusha kwa sauti kubwa hakuna mold (kinu) cha kupika tyre kilichohamishiwa Yana Kenya.
Hii kauli ya Ngongoo inaonesha kuwa umedanganya, mengine porojo zake.
Haaa haaa Bibie wa Lumumba unapenda ligi.Kwa faida yako na wengi nilikuwa Finance Division so nilikuwa naona transactions nyingi sana mambo yalipozidi kuharibika nikatimua mbio mwaka haukumalizika mlango ukarudishiwa ajira zikazikwa na serekali ikakosa kodi mbali mbali eg VAT,PAYE,Corporate tax,withholding tax & Import duty.
Nimezungumzia direct employment bado kulikuwa na indirect employment eg makampuni ya usafirishaji tyres,makampuni ya kutoa huduma za chakula kwa wafanyakazi,makampuni ya usafi,makampuni ya clearing & forwarding,makampuni ya kushona nguo za wafanyakazi,viatu (magereza Moshi)makampuni ya ndani yaliyokuwa yakiuza raw material kwaajili ya ya kuzalisha tyres eg chokaa,mpira wa Morogoro na Tanga na nk.
Ulikuwa mmoja wao saa unataka kujisafisha tu, sema kweli tu, kwanini huku whistle blow siku hizo uje kuyasema leo?
Ng'ongo umenikuna!
Nilfanya kazi pia hapo.
Deven Ndio alikiuua hiki kiwanda. Alianzisha branch ambazo haikuwa na mbele wala nyuma Ili aendelee kula Bata. Kila branch alikuwa Na totoz!
Jamal alipenda starehe! Na akajaza watu wake waliokimalizia kiwanda Kabisa.
Faiza .....Ngongo yupo Sahihi
Inasikitisha sana
Ungesoma magazeti ya mwanahalisi ya wakati huu labda ungenielewa.Mimi ndio nilimfanya Devendrah akakimbia Tanzania nasema mimi tena bila kificho.Mimi ndio niliandika barua Tanzania Investment Bank Rose Soloka akatimuliwa.Tangu atimuliwe kahakikisha ajira yake inakuwa siri yake na mumewe.
General Tyre ilikuwa na wafanyakazi 300 makao makuu kwa nafasi yangu nilitetea ajira ya wafanyakazi ambao wengi kwa uelewa mdogo walikuwa wakilaani sana kila article ya kuponda uongozi wa GT ilipotoka kwenye magazeti mbali mbali ilifika hadi chama cha wafanyakazi kikawa kinajibu hoja zangu.
System ya nchi ilikuwa imelala laiti wangechukua hatua mapema hakika leo tungekuwa tunatembelea magari yetu na tyre general.
Unajisifu kuuwa kiwanda?
Unanchekesha!
Mkuu Kimsingi umekubali sema huwezi kuwa wazi humu
Wenyewe wanasingizia Glabalization; ati tatizo hili lipo kila pahala duniani. watakupa tshert Ilioandikwa chagua CCM. safari hii tutapigia deki Tshert za kinani leteni tu mana watu hawako bungeni bize kuweka mikakati.Ccm inamakandokando mengi sana
Pale juu ya Kiltex (Kiwanda cha Kiko- Mitemba) kuna Kanisa jipya limefunguliwa. Wanachama wake wengi wao wako viziri
... ........ wakiristo wanatafuta wakumshushia ziko la mavii !
Ngongo
Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??